• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0111

    (GMT+08:00) 2010-01-12 16:53:22

    Barua ya Msikilizaji wetu Bw.Amin Najmi

    "Rafiki kipenzi,
    Ni furaha iliyoje kuuona tena mwaka huu ukiuaga ulimwengu mzima. Mwaka mwingine unakuja na hata hivyo hakuna ajuaye kilichojificha katika mwaka huo.
    Basi tuwe na matumaini kwamba utakuwa mwaka uliojaa upendo, afya, bahati njema,furaha na matumaini na ni mwaka ambao urafiki wetu utazidi kukua na kuimarika.
    Heri ya mwaka mpya!"

    *****************************************************************************

    Wasikilizaji wetu wa Kahama CRI listeners Club S.L.P 1067 Shinyanga Tanzania, wanasema tunapenda kutumia fursa hii ili kuipongeza sana serikali ya China na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka 60 tangu China ianzishwe mwaka 1949, ambapo mwanzoni mwa mwaka 2010 huko jijini Dar es salaam pia kutakuwa na sherehe ya kukabidhi tuzo kwa washindi wa chemsha bongo ya miaka 45 tangu China na Tanzania zianzishe uhusiano wa kibalozi mwaka 1964, chini ya waliokuwa viongozi wetu mashuhuri hayati Mao tse Tung wa China na hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania. Kwa kweli sherehe hii ya kuadhimisha miaka 45 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Tanzania sote tunaiombea iwe sherehe njema na yenye mafanikio mema kwa serikali zote mbili. Mwisho tunawapongeza wafanyakazi wote wa Redio China Kimataifa kwa kazi nzuri mnayofanya, wasikilizaji wenu tulioandika barua hii ni Joseph Ng'wipagi, Barnabas.S. Kulwa, Joyce Magoye Kumalija, Pamba Lunyembeleka na Joshua Andrea. Ahsanteni . Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu wa Kahama CRI listeners Club kwa barua yenu ya pongezi, sisi tunawaomba msisite kutuandikia maoni na mapendekezo mbalimbali mliyonayo kupitia kipindi hiki cha sanduku la barua na mwisho tunaungana nanyi kwa kuitakia sherehe ya utoaji tuzo iwe njema na iwe na mafanikio mema. Msikilizaji wetu Stephan Magoye Kumalija wa S.L.P 1067, Kahama Shinyanga Tanzania anasema ni yangu matumaini makubwa kuwa wafanyakazi wote wa CRI mnaendelea vyema na kazi za ujenzi wa taifa, mimi naomba kutumia fursa hii ili kuwapa hongera sana viongozi wa nchi mbalimbali ambao wamefanya mpango wa kuwasiliana kwa barua pepe pamoja na simu na wananchi wao ili kutoa maoni mbalimbali yanayowakera, viongozi wenyewe ni hawa wafuatao, rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jackob Zuma wa Afrika kusini pamoja na waziri mkuu wa Japani Bw Yukiyo Hatoyama. Hivyo basi nawapongeza sana viongozi hawa wote waliofanya mpango kama huo wa kuwasiliana na wananchi wao. Na nawaomba viongozi wa nchi mbalimbali hapa duniani wafanye mpango kama huo wa kuwasiliana kwa simu na barua pepe na wananchi wao, ili wananchi waweze kutoa dukuduku na maoni yao mbalimbali yanayowakera. Mwisho ninawatakia wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI heri ya mwaka mpya wa 2010. Katika barua yake nyingine Stephen Kumalija anasema napenda kuwapongeza viongozi wa nchi na sehemu 120 waliohudhurua mkutano mkuu wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Pia nawapongeza sana rais Hu Jintao wa China, waziri mkuu mpya wa Japani Yukiyo Hatoyama pamoja na viongozi mbalimbali kutoka mashariki ya mbali kama vile Korea ya kusini, Indonesia,Philipins, India, Kambodia, Vietnam, Thailand n.k, wakijumuika na viongozi wenzao kutoka nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Marekani katika mkutano huo. Aidha ninaipongeza sana serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuendelea kujenga vyuo mbalimbali vya confusion ambavyo mpaka sasa vimefikia 300 katika nchi na sehemu 81 duniani. Mwisho naomba mnitumie magazeti ya China today na China pictorial kwani magazeti hayo yananifunza mambo mengi mbalimbali yakiwemo ya China na duniani kote. Shukrani za dhati msikilizaji wetu Stephan Magoye Kumalija kwa maoni yako kuhusu viongozi mbalimbali walioanzisha utaratibu wa kuwasiliana na wananchi wao kwa lengo la kusikiliza kero walizonazo, kweli ni jambo jema ambalo linafaa kuigwa na viongozi mbalimbali duniani, ingawa hivi sasa kuna njia nyingi tu za kuwawezesha viongozi kupokea maoni na kero za wananchi. Na kwa upande wa vyuo vya confusious ni kweli serikali ya China imejitahidi kujenga vyuo vingi duniani ili kurahisisha huduma hii ya mafunzo ya kichina kwa kuwa hivi sasa kichina kinaendelea kukua zaidi duniani. Msikilizaji wetu Jider S. Lukanda S.L.P 1067 Kahama Tanzania, anasema natuma barua yangu hii kwa mara pili baada ya kusubiri kwa muda mrefu majibu yangu kutoka kwenu, au barua yangu ya hapo kitambo haikufika? Ninawaomba sana wapendwa wangu nami niwe mwanachama wa Redio China Kimataifa, nitafurahi pia mkiniorodhesha jina langu kwa wale wanachamna wenu mnaowatumia karatasi za masuali ya chemsha bongo, pamoja na magazeti, bahasha zilizolipwa pamoja na kadi za salamu. Nitafurahi kama majibu nitayapata haraka kutoka kwenu. Mwisho nawatakia wafanyakazi wote kazi njema na yenye fanaka. Tunakushukuru sana msikilizaji wetu Jider S. Lukanda kwa barua yako, kubwa ni kukuambia kuwa usiwe na wasiwasi kwani maombi yako tayari tumeshayafikisha kwa wanaohusika na tayari jina lako limeshaorodheshwa kwenye majina ya wanachama wetu hivyo subiri wakati wowote utaweza kupokea bahasha pamoja na vitu vingine tunavyowatumia wanachama wetu. Na msikilizaji wetu Mussa A. Mustapher ametutumia shairi moja lisemalo: Zidumu balozi mbili China na Tanzania, anasema, nitakuwa tayari kuja kughani na nikasikika moja kwa moja kupitia Radio China kimataifa, Idhaa ya Kiswahil. Hii ni kwa sababu fani hii iko damuni mwangu kuanzia kutunga na kughani. Nasubiri uamuzi toka kwenu tu. Na kutokana na taabu ya kuja kughani shairi hilo yeye mwenyewe, hapa tunapenda kusoma shairi lake hilo. Yarabi wetu mwenyezi, uliyeumba dunia Ahsante kwa kutuenzi, salama kutujalia Tudumishe ubalozi, China nasi Tanzania Zidumu balozi mbili China nasi Tanzania! Nawaomba viongozi, wa China na Tanzania Daima wawe wawazi, katika hii dunia Wasifanye ubaguzi, wa watu kutubagua Zidumu balozi mbili China nasi Tanzania! Zama za utandawazi, ndugu ninawausia Tutafuteni ujuzi, pande zote za dunia China mpaka Uholanzi, huko kote tembelea Zidumu balozi mbili China nasi Tanzania! Sasa tuna wakufunzi, wengi China watokea Mambo mengi watujuzi, nasi tunazingatia Nawaombea mwenyezi, azidi kuwajalia Zidumu balozi mbili China nasi Tanzania! China wewe mkombozi, wengi umesaidia Wastahili pongezi, hapa kwetu Tanzania Rabi zidisha wapenzi, kwa China na Tanzania Zidumu balozi mbili China nasi Tanzania! Nawasifu viongozi, wa China na Tanzania Kwa kufanya uamuzi, wa mawazo kuchangia Bila ya kigugumizi, mambo twajiamulia Zidumu balozi mbili China nasi Tanzania! Rabi zidi kutuenzi, Wachina na Tanzania Lisizuke jinamizi, balozi zikajifia Tukakosa nguvu kazi, tukabaki jililia Zidumu balozi mbili China nasi Tanzania! Ni makubwa mapinduzi, tena ya kujivunia Tunafanya matanuzi, kwenda China kutembea Sababu ya ubalozi, wa China na Tanzania Zidumu balozi mbili China nasi Tanzania! Hapa naachia ngazi, safari nasubiria Kwenda kwenye matembezi, China nitafurahia Ninamuomba mwenyezi, afya njema tujalia Zidumu balozi mbili China nasi Tanzania! Tunamshukuru sana Bw. Mussa A. Mustapher kwa shairi lake linalotutia moyo. Asante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako