• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwandishi wa habari wa Ujerumani ashuhudia mabadiliko ya China katika miaka 30 iliyopita

    (GMT+08:00) 2010-01-14 16:37:17

    Mwaka 1976 kijana mmoja wa Ujerumani Bw. Martin Kummer, ambaye alipokuwa na umri wa miaka 27, alikuja nchini China akiwa mwandishi wa habari wa gazeti la Hamburg la Ujerumani, ambapo alitumia macho yake kuiona China yenye historia ndefu; mwaka 2006 yeye na mkewe waliitembelea tena China, na kutumia kamera kurekodi mabadiliko ya China na watu wa China katika miaka 30 iliyopita. Tarehe 25 Novemba, alifanya maonesho ya picha mjini Beijing, ili Wachina waweze kukumbusha mchakato wao wa maendeleo kwa kupitia mtizamo wa mtu kutoka nchi ya magharibi.

    Bw. Martin Kummer alianza kuifuatilia China alipokuwa mwanafunzi, wakati huo alijaribu kupata habari nyingi zaidi kwa njia mbalimbali. Mwezi Aprili mwaka 1976, akiwa mwandishi wa habari alitimiza ndoto yake. Aliambatana na ujumbe mdogo wa Ujerumani kuja nchini China, na kutembelea miji ya Beijing, Shanghai, Guilin na Hongkong. Alisema,

    "Wakati ule niliiona na kuisikia China kwa kupitia magazeti, televisheni na radio tu, lakini baada ya kuja nchini China niliweza kuiona China halisi. Niliwasiliana na watu wa sekta mbalimabli, wakiwemo waandishi wa habari, maofisa na watu wa kawaida, nikaona China niliyoiona ni tofauti na ile niliyoifahamu kwa kupitia habari zilizotolewa na vyombo vya habari."

    China machoni mwa Bw. Martin Kummer ilikuwa na sura halisi: watu walivaa nguo sare, bidhaa katika maduka hazikuwa nyingi, na vifaa katika hoteli nzuri kabisa havikuwa vya kisasa. Lakini Wachina walimvutia zaidi, waliwaheshimu Mao Zedong na Zhou Enlai, walikuwa na urafiki lakini walikuwa hawataki kuongea sana, na walitaka kujua mengi kuhusu hali ya nje ya China. Alisema,

    "Wakati ule watu hawakuwa na mtimazo ulio wazi na hawakutaka kuongea sana, lakini walikuwa na urafiki. Wakati ule nchini China hakukuwa na watu wengi kutoka nchi za Ulaya, hata Wajerumani. Nilipomaliza kupiga picha na kukaa kwenye kiti, watoto wengi walinikimbilia na kuangalia nafanya nini, na kuangalia nimeshika nini mkononi mwangu. Sio tu watu walitaka kuona pua yangu ndefu, bali pia walitaka kusikia hali ya Ujerumani na ya nchi za Ulaya."

    Kwa hiyo, Bw. Martin Kummer alitaka kurekodi yote aliyoona nchini China. Aliwapiga picha wanaume na wanawake, wazee na watoto, wakulima na madaktari. Katika picha zake, watoto walicheza katika shule ya chekechea, baadhi ya watoto watundu waliinua vichwa vyao kutazama kamera; na wakulima wakitabasamu. Baiskeli zilizowekwa kwa utaratibu barabarani na aiskrimu za vijiti zilizouzwa sana, picha hizo zote zinawafanya Wachina wengi wa leo wacheke wanapoziona. Katika safari ile ya zaidi ya kilomita elfu 10 kutoka Beijing hadi miji ya kusini ya China, Bw. Martin Kummer alipiga picha zaidi ya 1,000.

    Mwaka 2006 Bw. Martin Kummer aliitembelea China tena, pamoja na mkewe walitembelea vivutio mbalimbali alivyotembelea mwaka 1976, walitaka kurekodi na kulinganisha mabadiliko makubwa ya China baada ya kuanza kutekeleza sera za mageuzi na kufungua mlango. Walitembelea tena miji ya Beijing, Shanghai na Guilin, lakini picha alizopiga zinaonekana ni tofauti na sehemu alizokumbuka: majengo marefu yanaonekana hapa na pale, watu wanatembea kwa haraka barabarani wakiwa wenye imani, na magari yamekuwa vyombo vya kawaida vya mawasiliano badala ya baiskeli. Ilikuwa vigumu kwa Bw. Martin Kummer na mkewe kutafuta sehemu zilezile yalipo majengo, vivutio na barabara walizopiga picha hapo awali.

    Bw. Martin Kummer alisema, safari hii pia ilikuwa majaribio mapya kwake ya kupiga picha. Aliwahi kuwapiga picha watu wengi maarufu, na aliwahi kwenda katika nchi nyingi kupiga picha na kuandika, lakini siku zote moyoni mwake ana hisia kubwa kuhusu China, anataka sana kuielewa nchi hii na watu wake. Alisema,

    "Zamani nilikwenda Marekani, Ufaransa na Uingereza kupiga picha mara kwa mara. Niliwapiga picha malkia Elizabeth wa Uingereza, marais wa zamani wa Marekani Bw. Reagan na Bw. Clinton, lakini hii ni mara yangu ya kwanza kupiga picha za aina hii ili kulinganisha hali ya hivi sasa na ya zamani nchini China. China inanivutia, kwa sababu baada ya kufariki kwa Mao Zedong, China ilianza kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, hii ni hali pekee duniani. Unaweza kuona mabadiliko ya tabia za Wachina, wao wanafanya kazi kwa bidii, na kushikilia kutafuta maisha yenye furaha."

    Katika safari yake hiyo, hisia zinazoonekane kwenye nyuso za watu katika picha alizopiga ni za hali mbalimbali, wapendanao wakikumbatiana na kubusiana hadharani, zamani hali hii haikuweza kuonekana nchini China.

    Bw. Martin Kummer aliona furaha wakati aliposafiri. Alipiga picha mara kwa mara, mwishoni aliondoka nchini China akiwa na picha zaidi ya elfu 10. Yeye na mkewe walionesha picha hizo kwa watu wa Ujerumani, na kufanya maonesho maalum mijini Hamburg na Berlin, pia walianzisha tovuti maalum, ili watu waweze kuifahamu China zaidi. Alisema,

    "Hivi sasa vyombo vya habari vya Ujerumani vinatoa habari nyingi kuhusu China, lakini habari hizi hazitoshi, vinajulisha majengo marefu zaidi, au maafa ya kimaumbile, au habari kuhusu uchumi, lakini havitoi habari nyingi kuhusu watu, lakini China ina watu zaidi ya bilioni 1.3, na Ujerumani ina watu milioni 10 kadhaa tu. Ninafuatilia sana maisha ya watu wa kawaida wa China, na hali yao ya kazi na kadhalika."

    Katika maonesho ya picha mjini Beijing, picha alizopiga Bw. Martin kummer zilipendwa na watazamaji wa China. Bibi Sun Qinhang alisema,

    "Picha hizo zinaonesha mabadiliko makubwa ya China baada ya kuanza kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, na upeo wa macho ya wageni ni tofauti na ule wa Wachina. Kabla ya miaka 30 iliyopita, nilikuwa mtoto, sina kumbukumbu nyingi kuhusu hali ya mambo, lakini picha zake zinanikumbusha nilipokuwa mtoto. Sasa ni miaka 30 imepita, China imekuwa na mabadiliko makubwa, ambayo yananifanya niwe na imani kubwa kwa nchi yangu China."

    Bw. Martin Kummer alisema, yeye ni mwandishi wa habari, hivyo hatasita kuwaza na kurekodi. Sasa yeye na mkewe walitaka kufanya maonesho kuhusu maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, ambayo yataonesha picha alizopiga tarehe 1 Oktoba mwaka jana mjini Beijing. Alikuwa na matumaini kuwa maonesho hayo yatakapofanyika mwaka huu mjini Hamburg, yatafuatiliwa na watu wengi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako