• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji ulioko kwenye mlima Changbaishan

    (GMT+08:00) 2010-01-18 17:06:14

    Sehemu inayojiendesha ya kabila la Wakorea ya Yanbian iliyoko mkoani Jilin, kaskazini mashariki mwa China, iko kwenye makutano ya mipaka ya nchi tatu za China, Korea ya kaskazini na Russia. Sehemu hii pia inajulikana kama "sehemu ndogo ya pembe tatu za dhahabu ya kaskazini mashariki mwa China". Ina mandhari nzuri ya mlima mkubwa wa Changbaishan na vivutio vingi vya utamaduni na jadi za kabila la Wakorea. Kutalii kwenye sehemu ya Yanbian kuangalia barafu na theluji katika majira ya baridi kunavutia zaidi.

    Sehemu ya Yanbian ina mlima Changbaishan, ambao ni mmoja kati ya milima kumi mikubwa na maarufu ya China, sehemu hii ina mandhari nzuri ya ngazi ya 5A ya taifa ikijulikana duniani kwa kuwa na bwawa la Tianchi kwenye mdomo wa volkeno, rasilimali nyingi ya wanyama na mimea pamoja na mandhari nzuri ya barafu na theluji. Misitu minene, ardhi iliyofunikwa na theluji, maporomoko makubwa ya maji na maziwa makubwa vimekuwa ni vivutio vikubwa kwenye sehemu ya kaskazini ya China. Bw Xu Haoran wa kituo cha utamaduni wa kamati ya usimamizi wa mlima Changbaishan alisema, "Mlima Changbaishan ni mlima wenye mandhari nzuri na vivutio vingi unaochukua nafasi ya kwanza kwenye sehemu ya kaskazini mashariki, sifa yake inalingana na milima mitano maarufu ya China. Volkeno ya mlima Changbaishan ni moja kati ya volkeno tatu kubwa hai nchini China, kilele chake kikuu kina mawe matupu, ambayo yanaonekana katika majira ya joto, na kinafunikwa na theluji katika majira ya baridi. Mlima Changbaishan ni chimbuko la maisha ya wakazi wa makabila mbalimbali wa sehemu ya kaskazini mashariki ya China na kabila la Waman, na unachukuliwa kuwa ni mahali patakatifu katika enzi ya Qing.

    Katika majira ya baridi Mlima Changbaishan unavutia sana, hususan kwa theluji nyeupe, anga ya buluu na mwangaza mzuri wa jua. Zamani watalii walidhani kuwa mlima Changbaishan unafungwa katika majira ya baridi kutokana na theluji nyingi inayoanguka huko, na ugumu wa kuona mandhari nzuri ya theluji ya mlima Changbaishan. Lakini hivi sasa kutokana na kuboreshwa kwa zana za utalii kila siku inayopita, watu wanaweza kuburudishwa kwa mandhari yake nzuri.

    Mtu anayefika kwenye mlima Changbaishan anatakiwa asikose kulitembelea bwawa la Tianchi. Bwawa hilo lililoko kwenye mdomo wa volkeno ya kilele kikuu cha mlima Changbaishan, na ni bwawa la mdomo wa velkeno linalochukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa nchini China, na limewekwa katika rekodi ya dunia ya Guinness kuwa ni ziwa la kwanza la volkeno lililoko kwenye mwinuko wa juu zaidi duniani. Pembezoni mwa ziwa hilo kuna vilele vya milima, maji ya ziwa hilo ni maangavu kabisa, ambayo ni chanzo cha mito mitatu ya Songhua, Tumen na Yalu, ziwa hilo pia ni mpaka kati ya China na Korea ya kaskazini. Ziwa hilo ni kama jade ya kijani kati ya vilele virefu vya mlima Changbaishan. Bw Xu Haoran alisema, kuna hadithi moja ya kusisimua kuhusu chanzo cha ziwa la Tianchi. "Inasemekana mungu Wangmu alikuwa na mabinti wawili warembo sana, na hakuna mtu aliyeweza kusema nani ni mrembo zaidi kati yao. Siku moja kwenye tafrija ya mapichi ya mbinguni, mungu Taibaijinxing alimpa zawadi ya kioo cha ajabu mungu Wangmu, na kumwambia kioo hicho kinajua nani kati yao ni mzuri zaidi. Hatimaye kioo kilisema yule ndogo ni mrembo zaidi, baada ya kusikia hayo dada yake mkubwa alikasirika, akatupa kile kioo duniani, kioo kilianguka kwenye mlima Changbaishan na kubadilika kuwa ziwa Tianchi."

    Kuna hadithi nyingi kuhusu ziwa Tianchi la mlima Changbaishan, wakazi wa kabila la Waman waliojiendeleza huko, na wakazi wa kabila la Wakorea wanachukulia ziwa Tianchi kuwa ni mahali patakatifu na mlima Changbaishan ni mlima wa mungu. Si rahisi kwa watalii kuona sura kamili ya ziwa Tianchi, kwa kuwa hali ya hewa ya huko inabadilika mara kwa mara, tena kilele cha mlima cha huko kinazungukwa na mawingu kila wakati. Lakini vitu hivyo vimeongeza uzuri wa ziwa Tianchi, na kuwa na vivutio vingi kwa watalii.

    Volkeno ya mlima Changbaishan ni volkeno hai, hivyo huko kuna chemchemi nyingi za maji moto, mtu kuweza kujiweka katika maji moto ya chemchemi katika majira ya baridi ni jambo lisilo la kawaida na ni burudani kwa watu. Bw Xu Haoran alisema, Kichwa kinawekwa kwenye theluji nyeupe iliyoko chini ya mtelemko wa mlima, mwili unakuwa kwenye maji moto ya chemchemi, macho yanaangalia theluji inayoanguka, na kuacha theluji ianguke kwenye ngozi, wakati huu mawazo ya mtu yanabadilika badilika kuendana na theluji inayoanguka; kuangalia dunia yenye theluji na barafu zilizoko pembezoni mwake, kuhisi hewa baridi na maji moto kwa pamoja, tena kuna vijiti na matawi ya miti kwenye upande karibu na chemchemi za maji moto, mtu anasikia raha sana kuoga katika chemchemi ya maji moto, kuangalia upande wenye miti katika siku za baridi inapoanguka theluji, jambo hilo ni la kuburudisha zaidi kwa watu wanaotembelea mlima Changbaishan katika majira baridi."

    Kijografia, sehemu ya Yanbian iliyoko kwenye mpaka wa nchi tatu za China, Korea ya kaskazini na Russia, ni sehemu yenye utamaduni na desturi zenye umaalumu. Sehemu yenye mandhari nzuri ya Fangchuan ya Yanbian iko kwenye sehemu ya kusini mwa mji wa Huichun, karibu na mdomo wa mto Tumen unaoungana na bahari ya Japan, sehemu hii inapakana na tarafa ya Hasang, Russia kwa upande wa mashariki, na inakabiliana na Korea Kaskazini kwa kutenganishwa na mto Doumanjiangli. Kama mtu akitazama mbali kwenye mwinuko wa ardhi hii iliyoko kwenye mpaka wa nchi tatu, anaweza kuona mandhari zote za nchi hizo tatu. Naibu mkurugenzi wa idara ya utalii ya Huichun Bw Jin Feng alisema, "Sehemu yenye mandhari nzuri ya Fangchuan imethibitishwa na serikali kuwa sehemu yenye mandhari nzuri ya ngazi ya taifa, sehemu hii ina milima na mito, inasifiwa na watu kuwa ni sehemu ambayo "bata bukini wa mwitu akilia, watu wa nchi tatu wanaweza kuisikia, na Chui milia akiunguruma basi mlio wake unaweza kuwashtua watu wa nchi tatu". Mahali maalumu na rasilimali kubwa ya wanyama na mimea vimeunda mandhari nzuri ya sehemu ya Fangchuan."

    Sehemu inayojiendesha ya kabila la Wakorea ina 80% ya watu wa kabila hilo wa nchini China. Wakazi wa sehemu hiyo ni wenye maadili mazuri, wakarimu na ni hodari kwa kuimba nyimbo na michezo ya ngoma. Hususan michezo ya mieleka, kurushwa juu kwenye ubao, kubembea, kuvutana kwa kamba, mbio ya vyelezo, mchezo wa ngoma ndefu, mchezo wa ngoma wa vinyago na mchezo wa furaha ya wakulima inaonesha zaidi umaalumu wa utamaduni wa wakazi wa kabila hilo dogo. Naibu mkurugenzi wa idara ya utalii ya sehemu inayojiendesha ya kabila la Wakorea ya Yanbian Bi Yuan Xiaoyun alisema, kwa watu wanaokwenda kutembelea sehemu ya Yanbina, hakika wataona utamaduni maalumu wa kabila la Wakorea. Alilsema:

    "Umaalum wa kabila la Wakorea wa sehemu ya Yanbian ni tofauti sana na wa makabila mengine, iwe kwa mavazi, lugha au chakula, watu wanajiona kama wako ugenini. Licha ya hayo, tuna sehemu moja, ambayo watu wakiwa huko wanaweza kuona mandhari za nchi tatu, tena kwenye njia ya kuelekea kwenye mlima Changbaishan watu wanaweza kuona miti yenye umande kwenye umbali wa kilomita 50 hivi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako