• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutalii karibu na Panda mjini Chengdu

    (GMT+08:00) 2010-01-25 16:53:15

    China ni nchi inayochukua nafasi ya kwanza kwa kuwa na Panda wengi duniani, ambao wanaitwa "tunu ya taifa" nchini China. Idadi ya Panda wanaoishi porini mkoani Sichuan, kusini magharibi mwa China, inachukua zaidi ya robo tatu ya Panda walioko nchini China. Mkoa wa Sichuan umeanzisha hifadhi kadhaa za Panda, na kuongeza idadi ya Panda kwa kuwazalisha kwa njia isiyo ya asili. Hifadhi za Panda za Chengdu licha ya kuwa na uwezo wa kufanya utafiti wa kisayansi, idadi kubwa ya Panda wanaoishi huko imewavutia watalii kwenda kuangalia Panda.

    Hewa ya nje ya nyumba kwenye mji wa Chengdu katika majira ya baridi ni baridi, lakini baridi haipunguzi shauku ya watalii wanaotaka kuangalia Panda wanaoishi katika hifadhi za huko. Toka asubuhi mapema, watu walikuwa wamejipanga kwenye msururu wenye urefu wa mita zaidi ya kumi. Baadhi ya wakazi wa huko walikwenda kuangalia Panda wakiwa pamoja na watu wote wa familia, vilevile kuna watalii kutoka sehemu nyingine, na wengi zaidi walikuwa wanafunzi wa shule mbalimbali. Wanafunzi kadhaa wa chuo kikuu kimoja cha mkoa wa Sichuan walikuwa wakijadili:

    "Panda wanatoka nje wakiwa na furaha, nina matumaini kuwa leo wanafurahi, tutaweza kuona wengi kidogo.

    Ninaomba wakati tunapofika huko wasiwe wamelala. Hawapendezi wakiwa wamelala, ninataka kuona wakiwa wanakula.

    Ninapenda kuwaona wakicheza au kurukaruka.

    Ninapenda kuwapapasa, lakini haiwezekani."

    Baada ya kuingia kwenye hifadhi, kulikuwa na mianzi mingi ya rangi ya kijani. Kwa kuwa sehemu hii iko mlimani na imeinama chini, kwa hiyo hifadhi hiyo inaonekana kama bustani kubwa ya mlimani. Katika eneo hilo kuna sehemu kadhaa za kuishi Panda. Mwelezaji wa hifadhi na utafiti wa Panda Bi Huang Jie alisema, Panda hawapendi kuishi katika sehemu moja iliyozungukwa kwa uzio, wanapenda mazingira mapya. Kwa hiyo wafanyakazi wanabadilisha nyumba zao kila baada ya muda maalumu, zaidi ya hayo wanabadilisha vitu vya kuchezea ili visiwachoshe… 2

    "Katika hali ya kawaida, wakitunzwa katika eneo moja lenye sehemu ndogo kwa muda mrefu kidogo, vitendo vyao vitakuwa si vya kawaida, hivyo wafanyakazi wanabadilisha nyumba zao mara kwa mara ili wajione kama wako ugenini kila mara, tena wanawawekea fremu za mbao, bembea na mipira, ilimradi kuboresha maisha yao, na kuwapatia vitu vya kuchezea."

    Ingawa ni majira ya baridi, lakini watu wanaweza kuwaona Panda karibu katika kila sehemu wanapoishi Panda. Panda wengine wanapanda miti taratibu na kuonesha watu makalio yao; wengine wanakumbatiana. Baadhi ya watalii waliuliza, Panda wanawezaje kutoka kwenye hali ya baridi, mbona hawaogopi baridi? Mwelezaji Bi Huang Jie aliwafahamisha akisema "Panda wanapenda hewa baridi, wanyama hao wanaishi kwenye misitu ya mianzi yenye mwinuko wa mita 1,500 hadi mita 3,400 ya milima mikubwa, huko hali-joto ni kiasi cha nyuzi 20 kwa mwaka mzima, Panda wana ngozi nene na manyoya mengi, tena ngozi yao haitoki jasho, kwa hiyo Panda hawaogopi baridi, hata katika nyakati za baridi kali, Panda si sawasawa na wanyama wengine, ambao wanalala katika majira ya baridi, kinyume chake wanatoka nje kutafuta chakula."

    Watu waliowahi kuwaona Panda wanafahamu kuwa sababu ya wanyama hao kuwa wanono ni kutokana na kuwa wanapenda sana kula na kulala. Watalii wengi wanaona Panda wanapenda sana kulala chini, huku wakijisetiri kwa mianzi, na kutafuna mianzi kwa hamu kubwa. Bi Huang Jie alisema, Panda mmoja anatumia zaidi ya saa 16 kula na kutafuta chakula kila siku, na wanalala katika saa 8 zilizobaki. Huenda watu wengi wanajiuliza, kwa nini Panda wanakula kwa muda mrefu sana, na kila siku wanakula mianzi kiasi gani?

    Kumbe Panda walikuweko duniani kabla ya miaka milioni 8 iliyopita wakiwa wanyama wanaokula nyama. Katika miaka mingi iliyopita Panda walibadilika na kuanza kupenda kula mianzi, ambayo inaota haraka na inaota kwenye sehemu nyingi, lakini Panda wamebakiza mfumo wa kuyenyusha chakula wa wanyama wanaokula nyama, hivyo wanapaswa kula kila wakati ili kuhakikisha wanapata lishe ya kutosha, tena hawapendi kutembea sana ili kudumisha nguvu. Bi Huang Jie alisema"Panda mmoja anakula miazi kiasi cha kilo 10 hadi 15, ingawa wanakula miazi mingi, lakini ni 17% tu inayoingia mwilini, na nyingine zaidi ya kilo kumi zinatoka moja kwa moja. Kwa hiyo anapaswa kula kila wakati ili kuhakikisha anapata lishe ya kutosha, zaidi ya hayo anapaswa kutopoteza nguvu kadiri awezavyo. Mianzi anayokula Panda haina lishe bora, lakini anaweza kunenepa sana, huu ni mtindo wa maisha yake, na ni moja ya sababu za kuweza kuishi duniani hadi hivi sasa kwa wanyama hao."

    Bi Huang Jie alisema, Panda ni wanyama wenye akili sana, wanajua mwanzi upi ni mzuri zaidi kwa chakula katika majira mbalimbali, na sehemu gani ya mwanzi ni laini zaidi. Hivyo anapoteza mianzi mingi wakati anapokula, katika hifadhi ya Panda, mtunzaji kila siku anamwekea Panda mmoja kilo 50 za mianzi ili iwe ya kutosha wakati Panda anapokula.

    Wafanyakazi kuwalisha Panda wachanga pia ni moja ya kazi zao muhimu. Chumba cha kutunza Panda wachanga hakifunguliwi kwa watazamaji, isipokuwa wanaweza kuwaona nje ya madirisha ya kioo. Bi Huang Jie alisema, katika miezi michache iliyopita watalii wanaokuja kuwaangalia Panda wachanga wanaongezeka kila siku kutokana na kuwepo kwa Panda wachanga wawili waliozaliwa Septemba mwaka uliopita, ambao hivi sasa wanatunzwa ndani ya chumba hicho. Wakilinganishwa na Panda wakubwa, Panda watoto ni watukutu. Panda wachanga hao wawili mara wanashuka kutoka kwenye "kitanda cha watoto wachanga", mara wanapanda juu, mfanyakazi anasimama pembeni mwao, na aliwapapasa mara kwa mara. Bi Huang Jie alisema, Panda wachanga huwawia shida wakati wanapotoa kinyesi, hivyo mtunzaji anatakiwa kupapasa matumbo yao mara kwa mara ili kuwasaidia chakula kiyeshushwe kwa urahisi. Alisema

    "Panda wachanga ni wadhaifu, kwa mfano yule aliyezaliwa mwezi Septemba, mtunzaji anapapasa tumbo lake ili aweze kutoa kinyesi bila matatizo. Kwa kuwa Panda wachanga hawawezi kutoa kinyesi wao wenyewe, endapo mama yao anawaangalia, basi analamba tumbo la Panda mchanga kwa ulimi wake; ikiwa anatunzwa na mfanyakazi, mfanyakazi huwa anapapasa tumbo lake kwa mikono."

    Mtalii kutoka mkoa wa Hubei Bi Zhang Man alisema, aliwahi kuona Panda wengi wakubwa katika mazizi ya miji mbalimbali, lakini hii ni mara ya kwanza kwake kuwaona Panda wachanga. Kutokana na mazingira bora wanayopewa ya kuishi nje, Panda wa huko ni wachangamfu zaidi. Alisema "Zamani Panda tuliowaona, walikuwa wanafugwa katika mazizi, na si wachangamfu kama wa hapa. Safari hii tumeona Panda wachanga sana pamoja na Panda wakubwa, hapa wafanyakazi wanawatunza kwa uangalifu mkubwa sana, Panda wa hapa wanapendeza sana."

    Mtalii kutoka Marekani Bw Jordan Mariuma alitembea bustani hii kubwa ya Panda asubuhi nzima, aliona Panda zaidi ya 20, alifurahi sana. "Panda ni wanyama wazuri sana, wanatunzwa vizuri nchini China. Ninawapenda sana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako