• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya ngoma ya Liyoresisi ya kabila la Wabuyi

    (GMT+08:00) 2010-02-04 14:42:23

    Kabila la Wabuyi lina watu zaidi ya milioni 2.5, na wengi wao wanaishi katika mkoa wa Guizhou ulioko kusini magharibi mwa China. Wabuyi ni hodari katika kuimba nyimbo na kucheza ngoma, na wanaweza kuonesha historia, utamaduni, mila na desturi zao kwa kupitia maonesho mbalimbali ya nyimbo na ngoma. Maonesho ya ngoma ya Liyoresisi ni moja kati ya maonesho hayo. Liyoresisi ni neno la lugha ya Kibui, na maana yake ni "kila mtu ana maisha mazuri marefu".

    Maonesho ya Liyoresisi yalibuniwa na wasanii wa mkoa wa Guizhou kwa mujibu wa hadithi za historia na mila na desturi za hivi sasa za kabila la Wabuyi. Maonesho hayo yanahusu mambo mbalimbali ya kabila la Wabuyi, na yanaeleza vizuri maoni ya watu wa kabila hilo kuhusu maisha.

    Kwa mujibu wa hadithi ya kabila la Wabuyi, katika kipindi cha mwanzo wa dunia, mvua kubwa mno ilinyesha, na kutishia maisha ya binadamu wote. Wakati huo samaki mkubwa alijitokeza na kubadilika kuwa mwanaume mwenye nguvu, na kuwaokoa binadamu. Ili kumshukuru samaki huyo, kiongozi wa binadamu alimwoza binti yake mkubwa kwa mwanaume huyo, na watoto wao ndio mababu wa kabila la Wabuyi. Mtemi wa kabila hilo alipanda mwanzi kuonesha dalili ya uhai mpya, na kwa kufuata mwanzi huo ulivyokua, wabuyi walichumbiana, kuoana, kuzaa watoto, kuvuna mavuno na kukua siku hadi siku. Katibu mkuu wa Shirikisho la wanatamthilia wa Guizhou Bw. Shi Jiayu alisema, "Kauli mbiu ya maonesho ya Liyoresisi ni uhai. Mtizamo muhimu wa watu wa kabila la Wabuyi kuhusu uhai ni kuwa uhai unadumu milele."

    Maonesho hayo yanaeleza mtizamo huo wa kabila la Wabuyi: mtemi mwenye umri mkubwa anafariki dunia, na mwanamke mjamzito anajifungua. Watu wanaovaa barakoa na majoho yenye rangi nyeusi na nyeupe wanazunguka mwili wa mtemi na kufanya shughulimaalumu, mtemi anafariki dunia kwa utulivu, wakati huohuo sauti ya kulia kwa mtoto mchanga inasikika.

    Maonesho hayo yanaitwa Yamian, ni mchezo maalumu wa sanaa wa kibuyi, na pia inaitwa Nuoxi. Nuoxi ilitokana na shughuli ya matambiko ya kuomba baraka na kufuka maafa. Maonesho ya Yamian yanatokana na halfa ya jadi ya mazishi, na yanaonesha matumaini ya watu wa kabila hilo kuwa watu waliofariki dunia watapata uhai mpya.

    Barakoa zinazotumiwa katika shughulihiyo yalitengenezwa kwa kutumia magamba ya mianzi michanga. Kwanza watu wanatembea kwa kuzunguka jeneza, baadaye wanasujudu mbele ya jeneza hilo wakionesha huzuni kubwa. Baada ya shughulihiyo, barakoa na zana nyingine zinachomwa, na washiriki wanaruka juu ya moto, ili kuepuka kusumbuliwa na pepo wabaya.

    Wachezaji wanafanya vitendo tu katika maonesho ya Yamian, na hawasemi kitu, hivyo maonesho hayo pia yanawekwa kwenye michezo ya kimya kimya.

    Wabuyi wanapiga ngoma ya shaba kwenye shughuli za mazishi na wanaposherehekea kuzaliwa kwa watoto. Bw. Shi Jiayu alisema, "Ngoma ya malaika ni ala ya jadi ya muziki ya kabila la Wabuyi. Kila kijiji cha kabila hilo kina ngoma moja hiyo. Wabuyi wanapiga ngoma ili mungu asikie sauti hiyo"

    Inasemakana kuwa ngoma ya shaba ni zawadi kutoka kwa malaika mbinguni, pia mababu wa kabila la Wabuyi waliipata kwa taabu sana. Hivyo ngoma hiyo ni tukufu na yenye thamani kubwa, na haiwezi kupigwa ovyoovyo na kuhifadhiwa vizuri, isipokuwa wakati wa shughuli ya mazishi na kutambika mababu.

    Bw. Su Shijin ni mwendeshaji mkuu wa maonesho ya Liyoresisi, na anavutiwa sana na utamaduni maalumu wa kabila la Wabuyi. Alisema, "Kwa mfano desturi ya kulia wakati wa kumwoza binti. Kwa mujibu wa desturi hiyo, wakati wa kumwoza binti, mama anapaswa kulia, na hata binti huyo anatakiwa kulia ili kuonesha kiu ya nyumbani, kwani ataondoka wazazi wake na nyumbani kwake. Huu ni utamaduni maalumu, na ulianzishwa kutokana na maisha ya wabuyi."

    Katika vijiji vya wabuyi, Bw. Su Shijin alihisi mazingira mazuri ya maisha yanayovutia watu. Alisema, "Kitu kinachonivutia zaidi ni utamaduni wa asili wa kabila hilo. Katika jamii ya kisasa inayojaa ushindani, wabuyi wanadumisha utulivu, na wanaishi maishi kwa kusikilizana na watu wengine na mazingira ya asili. Naona maskani yao ni kama bustani ya Eden."

    Kutokana na maendeleo ya jamii, utamaduni wa kabila la Wabuyi pia umeendelezwa sana. Katika maonesho ya Liyoresisi, kuna michezo ya jadi ya Yamian na kupiga ngoma, pia kuna michezo ya kisasa ya muziki na ngoma. Katika maonesho ya kusherehekea mavuno, vitendo vingi vya ngoma ya kisasa vinatumiwa. Bw. Su Shijin alisema, "Kitu cha kwanza ni usanii wa jadi wa kabila la Wabuyi, kwa mfano ni ngoma, muziki na nyimbo za jadi. Kitu cha pili ni mila na desturi ya kabila hilo. Maonesho yetu yanachanganisha vitu hivyo viwili na usanii wa kisasa duniani, ili kuonesha vizuri zaidi mtizamo wetu juu ya vitu vizuri vya zama zetu na moyo wa zama zetu za hivi sasa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako