• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Moyo wa uzalendo wa watu wa Macau kwa taifa la China

    (GMT+08:00) 2010-02-04 14:19:33

    Watu wakizungumzia kazi za usanii za China kuhusu Macau, inayojulikana zaidi ni Wimbo wa Macau uliotungwa na Wen Yiduo, mshairi mzalendo wa China. Kupitia wimbo huo, watu wengi kwa mara ya kwanza walisikia jina la "Macau" kwa Kireno, pia kwa kupitia wimbo huo, watu wengi wamefahamu zaidi uhusiano kati ya Macau na China na hisia kubwa walizonazo watu wa Macau kwa taifa la China.

    Ili kuhimiza utekelezaji wa sera ya "nchi moja mifumo miwili" katika mkoa wa utawala maalum wa Macau, na kutoa msingi wa kinadharia na maoni ya mikakati kwa serikali ya mkoa huo, ili iweze kutekeleza sera kwa mujibu wa sheria, katika nusu ya pili ya mwaka 2008 taasisi ya sera ya "nchi moja mifumo miwili" ya Chuo Kikuu cha sayansi na uhandisi cha Macau ilianzishwa. Katika miezi miwili iliyopita, taasisi hiyo ilikamilisha ripoti ya uchunguzi mpya mkubwa wa maoni ya raia.

    Mjumbe wa kamati ya sheria ya kimsingi ya Macau ya halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China Bw. Yang Yunzhong, ambaye pia ni mkurugenzi wa taasisi hiyo alifahamisha kuwa, ripoti hiyo inaonesha kuwa, maoni kuhusu "moyo wa uzalendo kwa taifa na kwa Macau" unakubaliwa na wakazi wengi wa mkoa wa utawala maalum wa Macau kuwa ni kitu muhimu cha kwanza chenye thamani kubwa. Bw. Yang alisema,

    "Tulitoa machaguo zaidi ya 10 kwa wakazi wa Macau, yakiwemo 'demokrasia, sheria, uhuru, haki za binadamu, usawa' na mengineyo, lakini 'moyo wa uzalendo kwa taifa na kwa Macau' unakubaliwa zaidi, ambapo asilimia 48.7 ya watu walikubali maoni hayo. Hii inaonesha dhahiri kuwa, wakazi wa Macau wanapenda sana taifa la China."

    Akiwa mmoja wa wataalam wa Macau wanaotafiti utaratibu wa "nchi moja mifumo miwili", Bw. Yang Yunzhong alisema, kukubaliwa kwa namna hii kwa "moyo wa uzalendo kwa taifa na kwa Macau", kunatokana na maendeleo makubwa yaliyopatikana katika shughuli mbalimbali tangu Macau ianze kutekeleza sera ya "nchi moja mifumo miwili".

    Mkoa wa Macau una watu laki 5 hivi, na eneo lake ni kilomita za mraba zaidi ya 20 tu, kwa hiyo ni vigumu kwake kupata maendeleo makubwa kwa kutegemea maliasili yake pekee. Hivyo baada ya Macau kurudi kwa taifa la China mwaka 1999, serikali kuu ya China ilitoa hatua mbalimbali kuusaidia mkoa wa utawala maalum wa Macau kukabiliana na athari mbaya za msukosuko wa fedha wa Asia na msukosuko wa fedha duniani, na kuunga mkono mkoa huo kuimarisha ushirikiano kati yake na sehemu mbalimbali nchini China, ili kusukuma mbele maendeleo ya uchumi wa Macau.

    Bw. He Houhua

    Wakati mkoa huo unapotekeleza sera za "nchi moja mifumo miwili", "Wamacau wajiendeshe Macau wenyewe" na "sera ya utawala wa kujiendesha kwa kiwango cha juu", ofisa mkuu wa zamani wa mkoa huo Bw. He Houhua aliwaongoza watu wa Macau kupiga hatua za kujiendeleza. Serikali ya mkoa huo ilitoa hatua mbalimbali zikiwemo kuendeleza shughuli za bahati nasibu na mpango wa kuwapa wakazi wa Macau kupata fedha, ambazo zimeufanya uchumi wa Macau upate maendeleo makubwa katika miaka michache tu. Bw. Yang Yunzhong alifahamisha kuwa, kuanzia mwaka 2000 hadi 2008 baada ya Macau kurudi kwenye taifa la China, takwimu kadhaa muhimu zimeonesha mabadiliko hayo makubwa. Alisema,

    "Thamani ya jumla ya uzalishaji wa bidhaa iliongezeka na kufikia Yuan bilioni 171.87 kutoka bilioni 49.742, ambayo ilikuwa ni ongezeko la asilimia 24.5. Ingawa kulikuwa na tatizo la mfumuko wa bei, lakini wastani wa ongezeko halisi ulikuwa ni karibu asilimia 15 katika miaka 9 kuanzia mwaka 2000 hadi 2008. Ongezeko hilo pia ni la juu sana kimataifa. Wastani wa pato la mtu uliongezeka hadi dola za kimarekani 39,036 kutoka dola za kimarekani 14,171. Kiwango kingine muhimu ni kuhusu maendeleo ya binadamu HDI, ambacho kiliinuka hadi 0.943 ya mwaka 2006 kutoka 0.864 ya mwaka 1998. 0.8 ni HDI ya nchi iliyoendelea duniani, na 0.9 ni nchi na sehemu iliyoendelea zaidi, lakini Macau imefikia 0.943."

    Jambo linalofurahisha ni kwamba, wakazi wa Macau wanaponufaika na maendeleo makubwa ya uchumi, wanalipenda zaidi taifa la China. Bw. He Houhua alisema, hisia hizo za wakazi wa Macau zinaoneshwa katika mambo mengi makubwa yanayohusiana na taifa. Bw. He alisema,

    "Katika miaka 10 iliyopita tumeona kuwa, mambo yaliyotokea nchini China, bila kuijali ni ya kufurahisha au ni ya fahari, watu wa Macau kama walivyo watu wa sehemu nyingine za China wanafurahia mafanikio iliyopata nchi yetu. Licha ya hayo, maafa ya kimaumbile yalipotokea, watu wa Macau pia walitoa misaada kwa njia mbalimbali ili kuwaunga mkono ndugu zetu waliokumbwa na maafa."

    Mkurugenzi mkuu wa bodi ya wakurugenzi ya Shirikisho la kuyafuatilia vitu vya mabaki ya kihistoria na kiutamaduni la Macau Bw. Zheng Guoqiang ni M-macau halisi. Alisema watu wanapozungumzia moyo wa uzalendo wa wakazi wa Macau, huona kuwa hii inatokana na kuimarishwa kidhahiri kwa nguvu ya ushindani ya taifa letu baada ya miaka 60 tangu China mpya ianzishwe, hasa miaka zaidi ya 30 tangu kuanza kutekeleza sera za mageuzi na kufungua mlango. Lakini mambo yanayosahauliwa na watu mara kwa mara ni kwamba, katika historia Macau ilikuwa sehemu ya wilaya ya Xiangshan ya mkoa wa Guangdong, na uzalendo wake kwa taifa ulikuwa wa jadi, na wilaya ya Xiangshan pia ni maskani ya watu wengi maarufu wakiwemo mtangulizi wa mapinduzi ya China Bw. Sun Yatsan na mfanyabiashara mwenye moyo wa uzalendo Bw. Zheng Guanying. Bw. Zheng Guoqiang alisema,

    "Historia ya Macau inaungana na ya taifa tangu enzi na dahari. Wazo la kuistawisha China lilitolewa mapema na Bw. Sun Yatsan, ambaye alitoka wilaya ya Xiangshan, na pia alikuwa ni m-macau. Kwa hiyo moyo wa uzalendo ni sehemu muhimu ya utamaduni wa Macau. Hivyo katika vipindi mbalimbali vya kihistoria, watu wa Macau siku zote wanaliunga mkono taifa, na kutoa mchango bila kusita katika mchakato wa kujipatia uhuru wa taifa letu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako