• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuangalia theluji na barafu mjini Harbin katika majira ya baridi

    (GMT+08:00) 2010-02-08 17:07:00

    Harbin ni mji wenye vitu vingi vya kuvutia, ambao unajulikana sana kutokana na vitu vya sanaa vya theluji na barafu. Hivi sasa ni majira ya baridi, na ni siku zenye baridi kali zaidi katika mwaka, lakini vilevile ni siku zenye furaha kubwa zaidi, kwani tamasha la theluji na barafu linafanyika hivi sasa.

    Ukitazama ramani ya China, utaona mkoa wa Heilongjiang ulioko kwenye sehemu ya kaskazini mashariki ya China, mfano wa batamaji wa shingo ndefu anayeruka angani. Harbin ni mji mkuu wa mkoa wa Heilongjiang, na unaonekana kama lulu moja inayong'ara chini ya shingo wa bara maji. Mji wa Harbin uko kwenye sehemu ya kaskazini na yenye baridi kali, katika majira ya baridi hali joto inaweza kushuka hadi nyuzi zaidi ya 20 au 30 chini ya 0, na siku zaidi ya nusu mwaka ziko katika majira ya baridi. Hali ya hewa baridi inaambatana na theluji na barafu, katika siku za baridi, wakazi wa Harbin wanapenda kulundika theluji na barafu pamoja na kujenga majengo ya barafu na kuchonga nakshi juu yake, hivyo wamevumbua utamaduni wa sanaa ya theluji na barafu kwa mawazo yasiyo na vizuizi.

    Mwezi Januari ya kila mwaka, watalii kutoka nchi mbalimbali wanavutiwa kwenda huko na kuburudishwa na baridi na vivutio vya michongo ya barafu. Baadhi ya watalii wanaotoka sehemu ya kusini, wanaona hali ambayo hawajawahi kuiona hapo kabla. Mtalii Lu Hao kutoka mji wa Guangzhou, ambaye ni mara ya kwanza kufika Harbin, alisema,

    "Harbin ni mji wa barafu, wenye baridi sana, zaidi ya nyuzi 30 chini ya 0, ambayo sijawahi kuisikia. Naona hapa ni kama ilivyo kwenye hadithi za watoto."

    Tamasha la theluji na barafu ya Harbin lilianzishwa katika miaka ya 60 ya karne iliyopita. Lilianza kufanyika mara ya kwanza katika bustani ya Zhaolin ya Harbin. Wasanii wa uchongaji wa barafu walitengeneza majengo ya barafu kwa kutumia barafu ya mto Songhua wa mji huo, kisha wanaweka taa za rangi ndani yake, majengo haya yakawa vitu vya sanaa. Katika mikono ya wasanii na mabingwa hao, barafu ya kawaida za mtoni ikawa ni vitu vizuri vya sanaa vinavyopendeza na kuvutia, bustani nayo ikawa dunia ya majengo ya barafu na bahari ya taa za rangi mbalimbali. Tamasha la sanaa za taa za barafu ya Harbin ina mabadiliko kila mwaka, watu wanaiita kuwa "hadithi mpya ya watoto isiyojirudia milele"

    Tamasha la taa za barafu linayofanyika kwenye bustani mjini Harbin ni maalumu zaidi, likishirikiana na kampuni ya Disney, ambayo inachukua nafasi ya kwanza katika mambo ya burudani duniani, imejenga dunia ya burudani ya theluji na barafu yenye umaalumu wa Disney, ambapo wahusika nyota wa katuni ya Disney wanajumuika kwenye misitu ya barafu na bahari ya theluji, watalii wanaweza kuingia katika nchi moja ya hadithi ya watoto iliyojengwa kwa theluji na barafu. Mkuu wa idara ya utalii ya mji wa Harbin Bi Yang Jie alisema "Mwaka huu, bustani ya Zhaolin itajenga dunia ya burudani ya theluji na barafu yenye mambo yaliyoko katika hadithi za Disney kwenye eneo la mita za mraba elfu 80, kwa kutumia theluji mita za ujazo elfu 10 na barafu ya mita za ujazo elfu 20, licha ya hayo tumeongeza michezo mingi ya theluji na barafu."

    Ama kuhusu dunia ya burudani ya theluji na barafu yenye umaalumu wa Disney kwenye mto Songhua, ambayo eneo lake litafikia mita za mraba laki 5 na itakuwa na vitu vya sanaa vya theluji na barafu zaidi ya 2,000, ambavyo ni pamoja na kasri la barafu, sanamu ya Firauni na Jumba la nchi ya kifalme la New York, licha ya hayo kuna sanamu za barafu za askari na farasi zilizotengenezwa kwa kufuata mifano ya sanamu za udongo wa mfinyanzi za askari na farasi zilizozikwa pamoja na mwili wa mfalme Qinshihuang wakati ule. Kila siku giza linapoingia, vitu hivyo vilivyotengenezwa kwa barafu vinang'arana kuwa maridadi sana katika mwangaza wa taa za rangi, na kuwavutia sana watazamaji.

    Mtalii kutoka Uingereza Bw Kevin alisikia mara kwa mara kuhusu dunia ya burudani ya theluji na barafu, safari hii alifika Harbin pamoja na watu wengine 5 wa familia yake kujionea. Alisema "Nzuri sana, hata mimi siamuni kama zimetengenezwa kwa barafu."

    Mke wake Bi Jean alisema, "Nzuri mno, kweli siwezi kuamini, vilijengwa kwa namna gani?"

    Mashindano ya vitu vya sanaa vya barafu yanafanyika kila mwaka katika tamasha la theluji na barafu la Haerbin, watalii wanaweza kuona vitu vya sanaa vya theluji na barafu vya kiwango cha juu kabisa katika dunia yetu. Kwenye bustani ya kisiwa cha Jua kilichoko kwenye mto Songhua, wasanii waliotoka nchi mbalimbali wa kutengeneza vinyago vya theluji walitengeneza vinyago vingi vya sanaa vya kiwango cha juu. Wakati wa mchana watalii wanapofika kwenye maonesho ya vitu vya sanaa vya theluji, wanaweza kuona vitu hivyo vya sanaa vya theluji vikimetameta katika mwanga wa jua.

    Msanii wa uchongaji vinyago kutoka mkoa wa Yunnan Bw Li Xingsuo hii ni mara ya pili kwake kushiriki kwenye maonesho ya vitu vya sanaa vya theluji, safari hii ameonesha sanamu iliyotengenezwa kwa theluji iitwayo "mtoto aliyeko juu ya ua la yungiyungi". Kuhusu sanamu hii aliyotengeneza Bw Li alisema"Uzuri wa sanamu iliyotengenezwa kwa theluji ni uzuri wa kimaumbile, sanamu ya theluji ni nyeupe kabisa na haina dosari yoyote. Sanamu hii ilitengenezwa kwa theluji ya kimaumbile kabisa, na inaonekana nyeupe kabisa. Watalii baada ya kufika hapa wasiwe na hofu, ingawa kuna baridi sana, lakini wataungana na mazingira ya vitu vya sanaa vya theluji na barafu, wamo humu humu ndani, licha ya kuweza kushuhudia theluji na barafu za sehemu ya kaskazini wataweza pia kufurahi kutokana na vitu hivyo vya sanaa."

    Mbali na kuweza kuburudishwa na vitu vya sanaa vya theluji na barafu vya Harbin, watalii wanaweza pia kuona maonesho ya watu wanaoogelea katika majira ya baridi, miongoni mwa watu hao waliokuwa wanaogelea kulikuwa na mzee mwenye umri wa miaka zaidi ya 80 na vijana wenye umri wa miaka chini ya 20. katika kipindi cha tamasha la theluji na barafu ya Harbin, watalii wanaweza kuona maonesho ya kuogelea katika majira ya baridi, na kushuhudia ujasiri na wamo wa kutoogopa shida wa wakazi wa sehemu ya kaskazini. Bw Yang Jie alisema"Kwenye mto Songhua, kila siku watalii wanaweza kuona maonesho ya watu kuogelea katika majira ya baridi, hali hii ni ya kushangaza sana. Maonesho ya kuogelea yanafanyika katika sehemu tatu za mto Songhua, kila siku kuna maonesho mara mbili za asubuhi na alasiri, tena kuna watu wanaopiga mbizi kutoka jukwaani, na mabondia wanaoshindana majini."

    Ni tofauti na sehemu nyingine za China, vijana wa Harbin wanapenda zaidi kufanya sherehe ya harusi katika mazingira meupe kabisa ya theluji na barafu. Katika tamasha la theluji na barafu la mwaka huu, jozi 28 zilifanya sherehe ya ndoa kwa pamoja katika dunia ya theluji na barafu isiyo na dosari. Bibi harusi Lian Yan alisema, anatarajia sana kufanya sherehe ya ndoa katika mazingira haya maupe sana akivaa nguo nyeupe ya bibi arusi, ili awe na sherehe tukufu zaidi ya ndoa. Alisema"nikifanya sherehe ya ndoa hapa nitakuwa na kumbukumbu nzuri sana, tulichagua hapa kwa makusudi, tunaona usafi na utukufu, ninajisikia vizuri sana."

    Mji wa Harbin una majengo mengi yenye mtindo wa kale wa kimagharibi pamoja makanisa mengi, hivyo watu huuita "Paris ndogo ya mashariki".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako