• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waluoluo wa kabila la Wayi wakaribisha mwaka wa chui

    (GMT+08:00) 2010-02-11 15:54:37

    Huu ni mwaka wa chui kwa mujibu wa kalenda ya kichina. Chui mkubwa ni mnyama mkali wenye milia anayefanana na chui wa kawaida. Wachina wanaona kuwa chui ni alama ya ushujaa na haki, na anaweza kuleta bahati nzuri, hata watu wa baadhi ya makabila madogo madogo nchini China wanaabudu chui. Luoluo ni moja kati ya matawi ya kabila la Wayi. Waluoluo wanaishi katika wilaya ya Shuangbai mkoa wa Yunan ulioko kusini magharibi mwa China, mpaka sasa wanadumisha desturi ya kuabudu chui na kucheza ngoma ya chui.

    Makabila mengi madogo madogo mkoani Yunnan yakiwemo Wayi, Wahani, Wanasi, Watujia na Wajingpo yanaabudu chui, lakini waluoluo wanaabudu chui kwa njia maalumu zaidi, kwani katika lugha yao, maana ya "Luo" ni chui . Mkurugenzi wa kituo cha utamaduni cha tarafa ya Fabiao ya wilaya ya Shuangbai Bi Li Yalan alisema, "Wakazi wote wa tarafa yetu wanajiita 'Waluluo'. Wanaume ni 'Luoluopo', na wanawake ni 'Luoluomo'. Maana ya maneno hayo mawili ni chui dume na chui jike. Waluoluo wanamchukulia chui kama ni babu yao, hivyo wanaabudu chui ."

    Hivi sasa katika wilaya ya Shuangbai, kuna ngoma tatu za jadi za kabila la Wayi. Ngoma hizo ni "Sheng ya Chui ", "Sheng ya Upatu" na "Sheng ya Chui Mdogo". Ngoma hizo tatu zinachukuliwa kuwa ni mabaki yenye thamani kubwa ya utamaduni wa jadi wa kabila hilo. Naibu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa utamaduni wa kabila la Wayi cha wilaya ya Chuxiong Bw. Xiao Huihua alisema, "Sheng" ni ala ya muziki ya makabila madogo madogo mkoani Yunnan, lakini hapa "Sheng" ni aina moja ya ngoma. Alisema, "Sheng ni aina moja ya ngoma ya kabila la Wayi. Sheng ya Upatu ni ngoma ya kupiga upatu, Sheng ya Chui ni ngoma ya kuiga chui , na Sheng ya Chui Mdogo ni ngoma ya kuiga chui mdogo."

    Kati ya ngoma hizo tatu, Sheng ya Chui ni maarufu zaidi, na pia inaonesha zaidi hali ya watu wa kabila la Wayi kuabudu chui . Ngoma hiyo ni ngoma ya jadi ya waluoluo wanaoishi katika wilaya ya Shuangbai, na kwa kawaida inachezwa kuanzia tarehe 8, Januari hadi tarehe 15, Januari kwa mujibu wa kalenda ya kichina. Kipindi hicho ni sikukuu ya mungu wa chui kwa waluoluo.

    Waluoluo wanaona kuwa babu wa pamoja wa binadamu ni chui, na vitu vyote duniani hata mbinguni vilianzishwa na chui. Kila mwaka wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, hafla mbalimbali za matambiko kuhusu chui ni shughuli maalumu katika wilaya ya Shuangbai. Mkurugenzi wa kituo cha utamaduni cha tarafa ya Fabiao ya wilaya hiyo Bi Li Yalan alisema,"Mwaka huu ni mwaka wa chui , hivyo ngoma ya Sheng ya Chui itakuwa kubwa zaidi kuliko zamani. Kucheza ngoma hiyo kunaweza kutuletea mavuno ya chakula, ustawi wa mifugo na usalama na maisha bora ya watu. Tunaona kuwa chui anatupatia mambo hayo mazurri, na kutubariki."

    Waluoluo huanza kutafuta wachezaji wa kuiga chui katika Sheng ya Chui kabla ya kufika kwa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina. Naibu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa utamaduni wa kabila la Wayi cha wilaya ya Chuxiong Bw. Xiao Huihua alisema, "Kila mwaka tunawachagua wachezaji tofauti kuiga chui . Wanaume wanaona fahari kubwa kwa kuchaguliwa kuwa wachezaji wa kuiga chui , kwani watu wa kawaida hawawezi kuiga chui , na kuna vigezo vikali."

    Sheng ya Chui inawahitaji wachezaji 17, wanaume wanane wenye nguvu wanaiga chui , wanavaa ngozi za chui zilizotengenezwa kwa vitambaa, na kupakwa milia za rangi tatu za nyekundu, nyeupe na manjano katika uso, mikoni na miguu. Kati yao mtu mmoja anayevaa nguo tofauti ni kama kiongozi wa chui . Mbali na wachezaji wakuiga chui , kuna wachezaji wawili wa kuiga malaika milimani wanaovaa vitambaa na kofia za majani, wachezaji wawili wa kuiga paka wanaovaa nguo nyeusi, watu wanne wa kupiga ngoma na mmoja mwingine wa kupiga upatu.

    Katika hafla mbalimbali za kutambika zinazofanyika kati ya tarehe 8, Januari hadi tarehe 15, Januari kwa mujibu wa kalenda ya kichina, wachezaji hao wanacheza ngoma siku baada ya nyingine kwa kuiga vitendo mbalimbali vya chui .

    Hafla kubwa zaidi inafanyika jioni ya tarehe 8, Januari kwa mujibu wa kalenda ya kichina, katika kiwanja ambapo moto mkubwa unawaka, watu wanne wanapiga ngoma, wachezaji wanne wanaoiga chui wanakaa kimpya katika pembe nne za kiwanja hicho, mchezaji wa kuiga kiongozi wa chui anaingia kiwanjani akiinua kijiti cha mwanzi na kutetemesha kibuyu cha kuwekea dawa za kuondoa pepo wabaya, ghafla anapiga mayowe "Chui ", na wachezaji wengine wanaruka na kuingia kwenye katikati ya kiwanja kwa kufuata sauti ya ngoma, baadaye wachezaji wanaoiga malaika wa milima na paka wanaingia kiwanjani kwa nyakati tofauti, na wachezaji wote wanaanza kucheza ngoma. Bw. Xiao Huihua alisema, "Sheng ya Chui inaeleza utamaduni wa jadi wa kuabudu chui wa kabila la Wayi. Ngoma hiyo pia ni kwa ajili ya kutambika malaika mbinguni wa chui ili kuomba ustawi na usalama wa waluoluo ambao ni watoto wa chui ."

    Sheng ya Chui ni usanii wa jadi unaochanganya nyimbo, ngoma na muziki, inaeleza hali ya waluoluo wanavyoabudu chui . Alisema, "Chimbuko la hafla na utamaduni wote wa jadi lilikuwa ni kwa ajili ya kumwomba mungu apatie binadamu maisha bora. Huu ni mtizamo wa awali wa binadamu, pia ni lengo lao la kufanya juhudi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako