• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw. John Rabe, mtu aliyeshuhudia historia ya China

    (GMT+08:00) 2010-02-11 15:49:23

    John Rabe

    Kutokana na kitendo chake kilichostahiki kusifiwa cha kuwaokoa wanajeshi na wananchi wa China wakati wa mauaji makubwa ya Nanjing mwaka 1937, pamoja na shajara yake iliyobaki, Mjerumani Bw. John Rabe aliheshimiwa na Wachina, na alichaguliwa kuwa ni mmoja kati ya "marafiki kumi wakubwa wa kigeni" kwa kura zaidi ya milioni 4. Siku chache zilizopita, mtalaam wa elimu ya majongwa ya wanawake wa hospitali ya Chuo Kikuu cha Heidelberg cha Ujerumani profesa Thomas Rabe akiwa mjukuu mkubwa wa Bw. John Rabe, alialikwa kuja hapa Beijing China, na Radio China Kimataifa ilipata fursa ya kufanya mahojiano naye.

    Bw. John Rabe alizaliwa mwaka 1882 mjini Hamburg, Ujerumani. Mwaka 1908 alikuja China, na kufanya biashara katika miji ya Shenyang, Beijing, Tianjin, Shanghai na Nanjing. Mwaka 1931 hadi 1938 alikuwa mwakilishi wa kampuni ya Siemens ya Ujerumani huko Nanjing. Mwaka 1937 kabla ya jeshi la Japan kuivamia Nanjing, John Rabe pamoja na wageni wengine waliokuwepo mjini Nanjing waliunda tume ya kimataifa katika eneo la usalama la Nanjing, ambapo alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa tume hiyo. Wakati wa mauaji makubwa ya Nanjing, kutokana na kutetea haki na kuwa na huruma, John Rabe na wageni wengine waliwaokoa watu zaidi ya laki 2 katika eneo la usalama lenye kilomita 4 za mraba tu. Watu wengi wanakumbuka kitendo hicho, na John Rabe pia anasifiwa kuwa ni "Oskar Schindler wa China" na "mtu mwema wa Nanjing".

    Bw. Thomas Rabe alisema, wakati alipokuwa mtoto, nyanya yake alimwambia mambo mengi kuhusu babu yake mjini Nanjing. Alisema kuwa kitendo cha babu yake mjini Nanjing kilionesha urafiki mkubwa kati yake na watu wa China. Alisema,

    "Naona kuwa kutoa misaada kwa marafiki wenye matatizo ni wajibu wa kibinadamu. Uamuzi wa babu yangu ulionesha moyo wa dhati kati ya marafiki wakati wa dhiki. Naona fahari kuwa mjukuu wa John Rabe."

    Alipozungumzia vitu vilivyomvutia zaidi John Rabe wakati ule, profesa Thomas Rabe alisema, China na wananchi wake walimvutia babu yake, na babu yake alipokuwa nchini China aliona kama yupo nyumbani. Bw. Thomas Rabe alisema,

    "Babu yangu alivutiwa na urafiki wa watu wa China, utamaduni wa jadi wa China na mazingira ya kuishi na kufanya kazi nchini China. Bila shaka, babu yangu alifahamu sana watu wa China, la sivyo, asingeamua kubaki mjini Nanjing ili kuwalinda wanajeshi na wananchi wa China."

    Profesa Thomas Rabe alisema, uzoefu wa babu yake nchini China uliathiri sana familia yake. Alisema,

    "Baba yangu alizaliwa mjini Beijing, na kuishi nchini China mpaka alipokuwa na umri wa miaka 14. Walikuwa wanazungumza kuhusu maisha yao nchini China mara kwa mara. Kwa sisi, China ni nchi yenye mambo mengi, ambayo watu wanatarajia kuyaona. Babu yangu aliwahi kusema kuwa, aliishi nchini China kwa miaka zaidi ya 30, na watu wa China wote walimtendea kwa kirafiki, hivyo alikuwa hana kisingizio cha kutofanya mambo yoyote wakati marafiki wa China walipokabiliwa na hatari. Kwa hiyo alitaka kuwasaidia Wachina. Sisi sote tunaona fahari kutokana na kitendo chake cha kishujaa."

    filamu ya John Rabe

    Kutolewa kwa Shajara ya Rabe na kuoneshwa kwa filamu ya shajara ya Rabe kulimfanya "mtu huyo mwema wa Nanjing" afuatiliwe zaidi. Safari hii John Rabe alichaguliwa kwa kura nyingi kuwa mmoja kati ya "marafiki kumi wakubwa wa kigeni", Bw. Thomas Rabe alifurahi sana akisema,

    "Mwanzoni tulishangaa sana. Wakati ule hatukujua hali ya shughuli hiyo. Baada ya kufahamu zaidi, tulifurahi sana. Hasa baada ya kujua kuwa babu yangu alichaguliwa kwa kura nyingi, sisi sote tunaona fahari."

    Sasa zaidi ya miaka 70 imepita, Bw. Thomas Rabe akiwa daktari pia anaichukulia kazi ya kuokoa maisha kuwa ni jukumu lake, kwake maisha na kazi ya kuokoa maisha zina maana kubwa zaidi. Alisema,

    "Filamu ya shajara ya Rabe ilisema: kuokoa maisha ya mtu mmoja ni sawa na kuokoa dunia. Hii ni sahihi. Babu ni mtu wa mfano kwangu, nataka kufanya juhudi ili kutoa mchango kwa amani kama alivyofanya. Naona maisha ni muhimu, hivyo watu wanapaswa kuthamini maisha. Nikiwa daktari, ninafanya mawasiliano na madaktari wa China mara kwa mara, na kusaidia kutoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi vijana."

    Kuheshimu maisha, kuokoa maisha na kuhimiza amani, hizo zote zilikuwa juhudi alizofanya babu yake, leo pia ni utafutaji unaotia mizizi moyoni mwa Bw. Thomas Rabe. Kwa hiyo Bw. Thomas Rabe na mkewe walianzisha "kituo cha mawasiliano cha John Rabe" huko Heidelberg, ili kuhimiza mawasiliano na maelewano kati ya tamaduni mbalimbali. Kwenye kituo hicho, licha ya kuonesha data muhimu za kihistoria, pia kinatoa misaada kwa wasomi wa nchi mbalimbali kufanya utafiti kuhusu historia. Profesa Thomas Rabe aliona kuwa, vijana wanapaswa kujifunza uzoefu wenye thamani kutokana na historia, ili kufahamu mambo ambayo bado hayajulikani. Alisema,

    "Vijana wa China wanapenda kutafiti historia, pia wanafikiria namna ya kukabiliana na historia na kujifunza kutokana na historia. Watu wanaweza kujua mwelekeo wa siku za usoni kwa kupitia kuuliza maswali, kuyajadili na kuyatatua matatizo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako