• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mgogoro wa kidiplomasia kati ya Libya na Uswisi kuhusu mateka wapata maendeleo

    (GMT+08:00) 2010-02-25 15:15:16

    Wizara ya mambo ya nje ya Uswisi tarehe 24 ilithibitisha kuwa, mfanyabiashara mwenye uraia wa Uswisi Bw. Rashid Hamdani, ambaye alishikiliwa nchini Libya kwa miezi 19 tarehe 23 alirudi nchini Uswisi, na Mswisi mwingine Bw. Max Goldi anatumika kifungo nchini Libya. Baadhi ya vyombo vya habari vinaona kuwa, mgogoro wa kidiplomasia kati ya Libya na Uswisi uliodumu kwa mwaka mmoja na nusu umepata maendeleo baada ya Umoja wa Ulaya kuingilia kati, lakini utatuzi wa mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili bado unahitaji nguvu kubwa ya usuluhishi wa Umoja wa Ulaya.

    Mgogoro huo ulitokana na tukio la polisi wa Uswisi kuwakamata Walibya tarehe 15 Julai mwaka 2008. Siku hiyo, polisi wa Uswisi waliwakamata mtoto wa rais Muammar Gaddafi wa Libya Bw. Hannibal Kadhafi na mkewe huko Geneva, kwa tuhuma za kuwatesa watumishi wa nyumbani. Tukio hili lilikasirisha familia ya Gaddifi, na kufanya akaunti ya makampuni ya Uswisi nchini Libya kufungwa. Baadaye Libya iliondoa mali zake kutoka benki za Uswisi, na kusimamisha utoaji wa mafuta kwa Uswisi. Libya pia iliwatia mbaroni Waswisi wawili nchini Libya Bw. Goldi na Bw. Hamdani kwa madai kuwa walifanya biashara haramu na kukiuka sheria za ukazi.

    Baadaye ili kutatua suala hili la mateka, serikali ya Uswisi ilifanya mawasiliano na serikali ya Libya mara kwa mara. Mwezi Agosti mwaka jana, mwenyekiti wa Shirikisho la Uswisi Bw. Hans-Rudolf Merz alifanya ziara nchini Libya, ambapo aliomba radhi kwa Libya kuhusu tukio la kukamatwa kwa Bw. Hannibal, na kufikia makubaliano ya kurudisha uhusiano wa kawaida kati ya nchi hizo mbili. Lakini baada ya Bw. Merz kuondoka, Libya iliwachukua Waswisi hao wawili kwenda sehemu isiyojulikana kwa zaidi ya siku 50 kwa madai kuwa walihitaji kuwaona madaktari. Ingawa baadaye mateka hao wawili walipelekwa katika ubalozi wa Uswisi nchini Libya, lakini muda si mrefu baadaye mahakama ya Libya iliwaadhibu Waswisi hao wawili kifungo cha miezi 16 na faini ya dola za kimarekani 1,500. Mapema ya mwaka huu, muda wa kifungo cha Bw. Goldi ulipunguzwa kuwa miezi minne, na Bw. Hamdani aliruhusiwa kuondoka, lakini mgogoro wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili haukutatuliwa, bali ulipamba moto.

    Wakati suala la Waswisi hao linaposhughulikiwa, mwezi Novemba mwaka jana Uswisi ilitangaza kufuta makubaliano kati yake na Libya, na kuweka vizuizi vya visa kwa Walibya. Kwa kuwa Uswisi ni nchi mwanachama wa Makubaliano ya Schengen, hivyo Walibya wanaowekwa na Uswisi kwenye orodha ya watu ambao hawawezi kupata visa ya Uswisi, pia hawawezi kupata visa ya nchi nyingine za Schengen. Kwa hiyo, Libya pia iliwawekea raia wa nchi za Ulaya kizuizi cha visa, kitendo ambacho kiliufanya mgogoro wa kidiplomasia upanuke kuwa suala la kuwapiga marufuku watu wa upande mwingine kuingia katika nchi yake. Hivyo nchi mbalimbali za Ulaya zilianza kufanya usuluhishi kati ya Libya na Uswisi. Tarehe 18 mwezi huu Uswisi, Libya na Umoja wa Ulaya zilifanya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje huko Madrid, na tarehe 22 Umoja wa Ulaya uliitisha mkutano wa mawaziri huko Brussels, ili kutafuta mpango wa kutatua mgogoro kati ya Uswisi na Libya.

    Kutokana na juhudi za pande mbalimbali, Libya ilirudi nyuma kidogo, na kumtaka balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Libya kuuhimiza ubalozi wa Uswisi kumkabidhi Bw. Goldi aliyehukumiwa na mahakama ya Libya, na Bw. Hamdani anaweza kuondoka nchini Libya.

    Kuhusu maendeleo hayo, vyombo vya habari vya Uswisi na wataalam husika wanachukua msimamo wa tahadhari. Gazeti la Tribune de Geneve lilisema, matokeo hayo yanawafanya Waswisi wawe na matumaini na pia wana wasiwasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako