• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutembelea "Potala ndogo" mjini Chengde

    (GMT+08:00) 2010-03-02 15:49:41

    Hekalu la "Potala ndogo"

    Katika mji wa Chengde, mkoani Hebei, sehemu ya kaskazini ya China kuna hekalu moja la dini ya kibudha ya kitibet linaloitwa Putuozongcheng, umbo lake linafanana sana na kasri la "Potala" la Tibet, isipokuwa ukubwa wake ni nusu ya kasri la Potala, kwa hiyo wakazi wa huko wanaliita "Potala ndogo", jengo hilo ni lenye mtindo wa majengo ya kabila la Wahan na kabila la Watibet.

    Hekalu hilo la Putuozongcheng lilijengwa wakati wa utawala wa mfalme Qianlong wa enzi ya Qing zaidi ya miaka 200 iliyopita. Hekalu hili lenye eneo la hekta zaidi ya 20 za mraba lilijengwa kwenye mtelemko wa mlima, na kuwa na lango kuu, kibanda chenye jiwe la kumbukumbu, lango kubwa la minara mitano, lango la mawe lenye vigae vya kauri, jukwaa kubwa jekundu na ukumbi mkubwa.

    Katika lugha ya Kitibet, Putuozongcheng maana yake ni "Potala". Upangaji wa majengo ya hekalu hili unafanana na wa kasri la Potala la Tibet, isipokuwa si la kifahari kama kasri la Potala. Je, kuna tofauti gani kati yake na kasri la hekalu la Putuozongcheng

    "Tofauti ya kwanza ni ukubwa, hekalu la Putuozongcheng ni nusu ya ukubwa wa kasri la Potala. Tofauti nyingine ni majukwaa makubwa mekundu, na jukwaa la Potala ni kubwa na la kifahari zaidi. Ya tatu, hekalu la Putuozongcheng ni la kifalme, ngazi yake ni ya juu zaidi kuliko kasri la Potala."

    Baada ya kuingia kwenye lango kuu la hekalu watu wanaweza kuona lango kubwa la mawe lenye mtindo wa jadi ya China, ambalo sehemu ya juu iliezekwa kwa vigae vya kauri vya rangi ya machungwa. Lango hilo lenye milango mitatu na nguzo nne, lilikuwa la kisasa kabisa kwa wakati ule.

    Lengo hilo lina maneno manne makubwa yaliyoandikwa na mfalme Qianlong, maana yake ni kuwa watu wakiwa na moyo wa unyenyekevu baada ya kupita kwenye lango hilo wataweza kumwona Buddha wa Guanyin. Lango hilo, ambalo maofisa wenye vyeo vya juu waliweza kupita, na wale wenye vyeo vya chini hawakuruhusiwa kuingia na kuabudu mle ndani.

    Mbele zaidi baada ya kupita hapo ni banda moja lenye mawe matatu ya kumbukumbu. Jiwe la katikati ni lenye maelezo kuhusu sababu na mazingira ya kihistoria ya kujenga hekalu hilo. Mwaka wa 36 wa utawala wa mfalme Qianlong, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 60, katika mwaka uliofuata mama yake alitimiza umri wa miaka 80 tangu azaliwe. Wakati ule viongozi wa makabila madogo walioko Tibet, Qinghai, Xinjiang na Mongolia walitakiwa kushiriki katika sherehe za siku ya kuzaliwa kwa mfalme na mama wa mfalme, na mfalme Qianlong alitilia maanani sana shughuli hizo, tena alizingatia dini ya Buddha ya kitibet waliyoamini, kwa hiyo aliamrisha kujenga hekalu hilo kwa kufuata mfano wa kasri la Potala. Kwa kuwa hekalu hilo ni dogo, kwa hiyo linaitwa na watu kuwa ni Potala ndogo."

    Hekalu la Potala mkoani Tibet

    Mwongoza watalii alisema, mawe hayo matatu yote yalichongwa maneno ya lugha za aina nne. Jiwe la kati lilichongwa maneno ya Kiman, mawe yaliyoko katika pande mbili zake yalichongwa maneno ya Kimongolia na Kitibet, na upande wa nyuma wa mawe hayo yalichongwa maneno ya Kihan, yakionesha umoja wa taifa.

    Kwenda mbele zaidi kwa kufuata njia yenye ngazi kwenye mwinuko, watu wanaona jukwaa jeupe na jukwaa kubwa jekundu, ambalo ni msingi wa hekalu hili. Majukwaa hayo yenye kimo cha mita 43 yako katika sehemu mbili za juu na chini, sehemu ya chini ni jukwaa la msingi, ambalo ni jeupe. Jukwaa jekundu lilijengwa juu ya jukwaa jeupe, ambalo ni sehemu kuu ya hekalu hilo. Kuta nene na kubwa za majukwaa hayo mawili zilizoko mbele ya mlima zinaonekana madhubuti kabisa, na rangi hizo mbili nyekundu na nyeupe zinaonekana nadhifu sana na za kuvutia.

    Sehemu ya katikati ya jukwaa kubwa jekundu inaingia ndani kidogo na kugawanyika katika sehemu 6 ndogo, ambapo kuna sanamu nyingi za Buddha. Juu ya jukwaa jekundu kuna ukumbi mkuu wa Wanfaguiyi. Ukumbi huo uko katikati ya majengo makubwa yaliyoko kwenye jukwaa kubwa jekundu, mapaa ya ukumbi ni marefu zaidi na yanajitokeza katika majengo yale na yakipigwa na mwanga wa jua yanang'aa kwa mwanga wa dhahabu. Ndani ya ukumbi mkuu kuna giza kidogo, mtu anapoingia ndani anaona mara moja hali ya ukimya na kutisha kidogo.

    Ukumbi mkuu ulikuwa ni mahali pa kufanya sherehe kubwa za kidini au mfalme kuonana na viongozi wa makabila madogo na mawaziri na maofisa wake. Sehemu ya mbele ndani ya ukumbi mkuu zimewekwa sanamu za Buddha za shaba nyeusi, ambazo zinaonekana kama Buddha hai. Kwenye dari la ukumbi mkuu kuna pambo la mbao lenye taswira maalumu. Mwongoza watalii alisema, "Pambo lililowekwa kwenye sehemu ya katikati ya dari ni la mbao na kupakwa rangi ya dhahabu, michoro iliyochorwa katikati ni dragon anayechezea lulu, ikimithilisha mfalme anayetawala nchi nzima. Chini ya pambo la mbao kuna zulia moja lililotundikwa, zulia hilo lilitengenezwa kwa nyuzi za dhahabu na fedha, ambalo lilikuwa zawadi iliyotolewa na mfalme Qianlong kwa ajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mama yake. Michoro iliyofumwa kwenye zulia hilo ni mahali pa peponi. Kwenye kitabu cha dini ya kibuddha kuna maelezo yanayosema, mawingu ya mbinguni peponi ni yenye rangi tano, na ardhini ni mchanga wa dhahabu, maua makubwa ya yungiyungi yanachanua kwenye mabwawa, na mitini ni lulu na matunda ya jade. Watu wote wa huko wanaishi maisha ya furaha sana."

    Chini ya zulia kunai kiti kikubwa cha rangi ya manjano, lakini mfalme Qianlong hakuketi kwenye kiti kile, kilikuwa ni kiti kilichowekwa kwa ajili ya Dalai lama wa nane. Wakati ule Dalai lama alikuwa na umri wa miaka 13 tu, kwa kuwa wakati ule alikuwa mdogo sana, na hakuweza kuja Chengde kushiriki kwenye sherehe ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mfalme kutoka Tibet iliyoko mbali sana, hivyo mfalme Qianlong alimwekea mahususi kiti kimoja.

    Dada Chen kutoka Singapore, alikwenda kutalii kwenye hakelu la Putuozongchen. Kwa kuwa yeye anafanya kazi ya usanifu wa majengo, kwa hiyo alikuwa na shauku kubwa kuhusu mtindo wa majengo ya hekalu hilo. Alisema, "Sijafika kwenye kasri la Potala, lakini kwa kiwango cha chini kabisa ninaweza kuliona hapa, baada ya kutembelea hapa nimekuwa na kumbukumbu, nikipata nafasi baadaye nitatembelea huko tena. Ninapenda kuona majengo, kwa kuwa ninafanya kazi zinazohusu mambo ya ujenzi. Watu wa zamani ni hodari sana, waliweza kutengeneza majengo mazuri kama haya kwa mikono tu, si kazi rahisi. Iwe kwenye mji wa Chengde au Beijing, naona wachina ni watu hodari sana."

    Wapendwa wasikilizaji, Putuozongchen ni hekalu lenye hadhi na mtindo maalumu kati ya mahekalu ya nchini China. Endapo mtapata nafasi, msikose kufika Chengde kuangalia hekalu hilo la kifalme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako