• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makala ya kwanza ya Mashindano ya chemsha bongo ya Maonesho ya kimataifa ya Shanghai: "Hai Bao" anakuongoza kutembelea Maonesho ya kimataifa ya Shanghai

    (GMT+08:00) 2010-03-02 19:57:33

    Leo tunawaletea makala ya kwanza isemayo: "Hai Bao" anakuongoza kutembelea Maonesho ya kimataifa ya Shanghai.

    Kabla ya kuwasomea makala hii, kwanza tunatoa maswali mawili ili wasikilizaji wetu myasikilize na kuyajibu baada ya kusikiliza makala.

    1. Kileta bahati cha Maonesho ya kimataifa ya Shanghai kinaitwaje?

    2. Taja majina ya majengo mawili yaliyopo kati ya jengo la mstari wa kati na majengo manne kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai.

    Sasa tunapenda kuwaelezea wasikilizaji wetu kuhusu kileta bahati cha Maonesho ya kimataifa ya Shanghai. Kileta bahati cha Maonesho ya kimataifa ya Shanghai kinaitwa Haibao, kina umbo la mtoto mdogo mwenye rangi ya buluu, macho mangavu ya tabasamu, na nywele zake zimesimama. Kileta bahati hicho kilichaguliwa kati ya vileta bahati zaidi ya elfu 20 vilivyobuniwa na watu kutoka sehemu mbalimbali duniani. Kati ya maneno yanayounda jina la "Haibao", "Hai" maana yake ya kichina ni bahari, na "Bao" maana yake ni hazina. Wachina wengi wanapenda kutumia neno Bao kuwa jina la watoto wao, ili kuwatakia watoto wao wawe na baraka. Jina "Haibao" la Kileta bahati cha Maonesho ya kimataifa cha Shanghai linamaanisha kuwa kileta bahati hicho ni hazina ya nchi zote, mashirika yote na watu wote wanaofuatilia, kuunga mkono na kushiriki kwenye Maonesho ya kimataifa ya Shanghai. Sasa tuambatane na Kileta bahari Haibao kwenda kutembelea eneo la Maonesho ya kimataifa ya Shanghai.

    Kwanza tutaingia kwenye Jengo la mstari wa kati wa Maonesho ya kimataifa ya Shanghai, Jumba la maonesho la China, Kituo cha maonesho ya michezo ya sanaa, Kituo cha Maonesho ya kimatiafa na Jumba la tafsiri ya kauli mbiu. Jengo la mstari wa kati ni kama lango kuu la kuingia kwenye Maonesho ya kimataifa ya Shanghai, nalo liko kwenye mstari wa kati katika eneo la Maonesho ya kimataifa ya Shanghai na barabara kuu ya mawasiliano, upande wake wa kushoto na wa kulia unapakana na Jumba la maonesho la China, Kituo cha maonesho ya michezo ya sanaa, Kituo cha Maonesho ya kimataifa na Kituo cha tafsiri ya kauli mbiu, umbo la jengo hilo ni mithili ya tanga la meli ambalo linawakaribisha watu. Jumba la maonesho la China ni jekundu, ambapo watu wanaweza kujionea utamaduni wa China na mambo yenye mitindo ya China. Kituo cha maonesho ya michezo ya sanaa ni jengo lililojaa harufu nzito ya usanii, jengo hilo liko kando la Mto Huangpu, wakati wa usiku jengo hilo linameremeta mithili ya magamba ya samaki, wakati wa Maonesho ya kimataifa ya Shanghai, maonesho makubwa ya michezo ya sanaa na shughuli kubwa zitafanyika kwenye kituo hicho.


    1 2 3 4
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako