• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mikopo midogo yawasaidia wanawake kuanzisha shughuli zao

    (GMT+08:00) 2010-03-04 16:02:18

    wafanyakazi wa kampuni ya mikopo midogo wakiwa wanasaidia wanawake kupata mikop

    Katikati ya miaka ya 90 ya karne iliyopita, katika mji wa Tianjin, ambao ni mji wa kasakzini mwa China, viwanda vingi vilianzishwa zamani sana huko, wanawake wengi walipunguzwa viwandani; lakini hivi sasa wanawake wengi wanafanikiwa kuanzisha shughuli zao. Wakati siku ya 100 ya Tarehe 8 Machi ya wanawake inapokaribia, waandishi wetu wa habari walikwenda Tianjin kufanya mahojiano kuhusu maendeleo ya wanawake.

    Duka la bibi He Jianchun liko karibu na kituo cha mabasi kilichopo katika sehemu ya Hedong mjini Tianjin. Duka hilo lenye mita 6 za mraba linauza sigara, pombe na vitu mbalimbali. Bibi He Jianchun anaanza kufanya kazi mapema asubuhi, anauza kifungua kinywa, kadi za kuongeza pesa kwenye simu za mkononi na vitu vingine. Ingawa ana umri wa miaka 47, lakini anaweza kutumia kompyuta. Alisema,

    "Ninaamka saa kumi na moja alfajiri, na kufungua duka saa kumi na moja na nusu. Kwa kuwa duka langu liko karibu na kituo cha mabasi, hivyo saa kumi na mbili na nusu hivi kunakuwa na watu wanaosubiri hapa kwenda ofisini. Asubuhi huwa nauza chakula cha asubuhi, maziwa, mikate na hamburger, hivyo nina pilikapilika nyingi."

    Katikati ya miaka ya 90 ya karne iliyopita, mji wa Tianjin ulianza kufanyia mageuzi mfumo wa kiuchumi, wafanyakazi wengi wa makampuni ya kiserikali, hasa wafanyakazi walipunguzwa. Bibi He Jianchun ambaye ni kiwete pia alipunguzwa.

    Bahati mbaya zaidi, muda si mrefu baada ya bibi He Jianchun kupunguzwa kazini, mumewe pia alipunguzwa kiwandani. Ili maisha yao yaweze kuendelea, bibi He Jianchun alianza kuuza vitu mbalimbali barabarani. Bila kujali ni majira ya baridi au ni majira ya joto, kila siku anaanza biashara yake mapema na kurudi nyumbani usiku. Mwanzoni kila mwezi aliweza kuchuma Yuan kumi kadhaa tu, baadaye kila mwezi alipata zaidi ya Yuan 2,000.

    Miaka mitano iliyopita, binti wa bibi He Jianchun alihitimu kutoka shule ya sekondari na kuanza kusoma katika chuo kikuu, na bibi He Jianchun alikuwa na wasiwasi, kwa kuwa mapato yanayotokana na biashara yanaweza tu kutatua suala la maisha ya kimsingi, hawakuwa na uwezo wa kumlipia karo ya chuo.

    Wakati huo bibi He Jianchun alisoma habari kutoka gazetini kuhusu mikopo midogo ya wanawake, ambayo ilisema kuna aina moja ya mkopo wa elimu inayowasaidia watoto wa mama wazazi maskini, ambao na riba ndogo. Habari hii kweli ilikuwa nzuri kwake! Lakini ni kweli? Bibi He Jianchun alikwenda kwenye ofisi za Shirika la Tianjin la kuhimiza uanzishaji wa shughuli na maendeleo ya wanawake linaloshughulikia kutoa mikopo. Alisema,

    "Wakati wa kulipa karo, nilikwenda kuomba mkopo kutoka kwa shirika hilo. Nilikwenda na gazeti lile na kuuliza kama shirika hilo linaweza kunikopesha, wafanyakazi wa shirika hilo wakajibu kuwa naweza kukopa nikiwa na fedha za uhakikisho za watu wanaostaafu na kitambulisho cha mwanafunzi cha binti yangu. Utaratibu huu haukuwa na matatizo, na siku 15 baadaye nilipata mkopo."

    Sherehe ya kuanzishwa kwa kampuni ya mikopo midogo mjini Tianjin

    Mkopo wa elimu wa mwaka mmoja wa Yuan 6,000 ulitatua tatizo gumu la karo. Sio tu biashara yake haikuathiriwa, bali kulipa Yuan zaidi ya 500 kila mwezi si tatizo kubwa kwa familia hiyo. Miaka minne baadaye, binti yake alihitimu kutoka chuo kikuu, na biashara ya bibi He Jianchun pia inaendelea vizuri, kila mwezi anaweza kupata Yuan zaidi ya 3,000.

    Wakati huo kulikuwa na fursa nzuri ya biashara. Ili kuwasaidia walemavu kuanzisha shughuli na kupata ajira, serikali ya sehemu ya Hedong ya mji wa Tianjin ilimpa bibi He Jianchun kibanda kimoja ambacho kiko karibu na kituo cha mabasi.

    Lakini tatizo lingine gumu linamkabili bibi He Jianchun. Ingawa hapaswi kulipa kodi kwa ajili ya duka lake, lakini alipaswa kuwa na mtaji wa kuanzisha duka hilo. Kwa kuwa ana uzoefu wa kukopa, bibi He Jianchun alikwenda tena kwenye ofisi za shirika la Tianjin la kuhimiza uanzishaji na shughuli za maendeleo ya wanawake. Kwa sababu katika miaka minne iliyopita alikuwa anaaminika, bibi He Jianchun alipata mkopo wa Yuan elfu 20 kwa haraka. Tofauti na safari iliyopita, mkopo huu ni kwa ajili ya kuwasaidia wanawake kuanzisha shughuli zao.

    Kama ilivyo kwa bibi He Jianchun, wanawake wengi mjini Tianjin wananufaika na mikopo midogo ya wanawake. Kwa mujibu wa takwimu, kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2009, kwa ujumla mji wa Tianjin ulitoa mikopo midogo yenye thamani ya Yuan karibu milioni 100, ambayo iliwaunga mkono moja kwa moja wanawake zaidi ya elfu 10 kuanzisha shughuli zao, na kuwasaidia wanawake zaidi ya elfu 50 kupata ajira.

    Ili kupanua njia ya kukusanya fedha, mwezi Agosti mwaka 2009 Shirikisho la wanawake la Tianjin liliunda kampuni ya hisa ya mikopo midogo ya wanawake, ambayo inaweza kutoa mikopo mara 10 zaidi kuliko zamani, na imeongeza aina za mikopo kama vile mkopo wa vifaa vya kilimo.

    Mikopo hiyo imetatua tatizo kubwa la wanawake la kuanzisha shughuli zao. Mwenyekiti wa Shirikisho la wanawake la Tianjin bibi Zhu Liping alisema,

    "Wanawake wanapoanzisha shughuli zao, tatizo kubwa zaidi ni fedha. Hivi sasa wanawake wakitaka kuanzisha shughuli zao, wanaweza kuja hapa, kama wanakidhi matakwa ya kukopa, kama vile wanaaminika, na miradi yao ni mizuri, basi ni rahisi kwao kupata mikopo. Suala la fedha ni suala kubwa, baada ya kuwa na kampuni ya mikopo midogo, tunaongeza nguvu za kuwasaidia wanawake kuanzisha shughuli na kupata ajira."

    Katibu mkuu wa shirikisho la kuhimiza uanzishaji wa shughuli na maendeleo ya wanawake la Tianjin bibi Li Jinfeng alisema, mikopo midogo sio tu inawasaidia wanawake kuondoa umaskini, bali pia inawasaidia kuinua hadhi yao katika familia na jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako