• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matembezi kwenye sehemu ya Huayuankou kando ya mto Manjano

    (GMT+08:00) 2010-03-08 17:03:19

    Mto Manjano unachukuliwa kuwa ni mto mama wa taifa la China. Kuna watu wanaosema mto Manjano umeipa sehemu ya kati ya China kitu chake kilicho kizuri zaidi, lakini wakazi wa mkoa wa Henan ulioko sehemu ya kati ya China, wanasema mto Manjano umebakiza taabu zake kwa sehemu ya kati ya China. Wakazi wa Henan wanatatizwa sana katika hisia zao kuhusu mto Manjano, kwa upande mmoja mto Manjano ni mto mama, lakini kwa upande mwingine ni maji yanayoweza kupoteza maisha yao. Kijiji cha Huanyuankou kiko kwenye kando ya mto Manjano, kijiji hicho kimewahi kufunikwa mara nyingi na maji ya mafuriko ya mto huu. Lakini kila baada ya mafuriko kuondoka, sehemu hiyo inaweza kujengwa upya na kuonekana hali ya ustawi. Inasemekana kuwa katika enzi ya Ming, miaka zaidi ya 500 iliyopita, ofisa Xu aliyekuwa na cheo cha juu, alijenga bustani yenye eneo karibu hekta 40 kwenye kando ya mto Manjano, alipanda miti na maua mbalimbali, ambayo baadhi yake inastawi na kuchanua maua hata katika majira ya baridi, wakazi wa karibu wanaume kwa wanawake na wazee kwa watoto walimiminikia huko kuangalia. Hapo baadaye mto Manjano ulibadilisha njia yake, na mafuriko ya mto yaliharibu kabisa bustani hiyo. Tokea hapo sehemu hiyo ikawa sehemu ya kuvuka kwenye kando ya kusini ya mto Manjano, na wakazi waliita Huayuankou. Hivi sasa Huayuankou iko kwenye kando ya kusini ya mto Manjano, umbali wa kilomita 17 kaskazini mwa mji wa Zhengzhou. Sehemu hii ni kielelezo cha mto Manjano, na pia ni kama dirisha la mto huo. Kuwepo katika sehemu maalum kijografia kumeifanya historia ya sehemu hiyo isiwe ya kawaida. Kwa sasa hakuna anayeweza kuthibitisha kama bustani ya ofisa Xu kwa wakati ule ilikuwa na maua na miti iliyostawi au la. Lakini hivi sasa sehemu ya Huayuankou kweli ina maua na miti mingi, na sehemu ya ukingo uliojengwa mtoni, ambao unaitwa "ukingo wa jemadari" imekuwa moja ya sehemu zenye mandhari nzuri katika sehemu ya Huayuankou. Naibu meneja mkuu wa kampuni ya utalii ya Huanghe Bw Yu Hanqing alisema"Jina la ukingo wa jemadari lilitokana na jemadari mmoja aliyesawazisha mto Manjano, kila mara alipata mafanikio katika kusawazisha mto huu na kupandishwa cheo na mfalme. Mwaka 1754 watu waliofuata walijenga hekalu la jemadari ili kumkumbuka, ukingo ule ulijengwa karibu na hekalu hilo hivyo watu walianza kuuita ukingo wa jemadari." Sanamu za kuabudiwa zilizowekwa ndani ya hekalu la jemadari ni miungu wa maji wa mto Manjano, inasemekana kuna miungu 64. jemadari yule ni mwakilishi wa maofisa waliokabidhiwa jukumu la kusawazisha matatizo ya mto Manjano wa enzi mbalimbali, maofisa hao walitekeleza vizuri sana majukumu yao walipokuwa hai, baada ya maofisa hao kufariki dunia, watu wanawakumbuka sana, kidogo kidogo wakachukuliwa kama miungu mioyoni mwa watu. Baada ya kuelezwa kuhusu sehemu ya Huayuankou iliyoko kando ya mto Manjano, tunataka kuwafahamisha kuhusu "wimbo wa kazini wa mto Manjano", wimbo huu ni kitu muhimu katika utamaduni wa mto Manjano, ambao ulitungwa na wafanyakazi katika kazi za kusawazisha mto Manjano. Wafanyakazi wa kusawazisha mto Manjano waliishi kwenye mashua mtoni kizazi hadi kizazi, wanaufahamu sana mto Manjano.

    Katika maisha yao ya kupambana na mawimbi makubwa na upepo mkali wa mto Manjano, wafanyakazi hao walibuni na kuendeleza wimbo maalumu waliokuwa wanaimba kazini. Pamoja na mabadiliko ya sehemu ya mto, wimbo uliokuwa ukiimbwa na wafanyakazi unabadilika pia kwa kuambatana na kasi ya maji ya mto. Sehemu za mwanzo na katikati za mto Manjano ni uwanda wa juu wa udongo wa rangi ya manjano na sehemu ya milima magharibi mwa mkoa wa Henan, sehemu hiyo maji ya mto ni yenye kina kirefu na yanatiririka kwa kasi, wimbo wa kazi ukiimbwa katika sehemu hiyo unaimbwa kwa nguvu na kwa haraka zaidi. Maji ya mto baada ya kutoka sehemu hiyo na kuingia kwenye sehemu ya tambarare ya kaskazini ya China, maji ya mto yaliyotiririka kwa kasi yanatulia hadi kuingia kwenye bahari ya Bo, wafanyakazi wa mashua wakiendesha mashua zao katika sehemu hii, wanaimba wimbo kwa taratibu na kwa madoido. Hivi sasa wimbo unaoimbwa kazini na wafanyakazi wa mashua umekuwa moja ya maonesho maarufu kwenye sehemu yenye mandhari nzuri ya Huayuankou, kila siku uimbaji wa wimbo huo unaoneshwa kwa watalii. "kiwango cha maisha ya wakazi wanaoishi kwenye kando za mto Manjano kimeinuka, hali kadhalika kwa wavuvi. Mto Manjano kweli ni mto mama, mto huu ni mama yetu." Kwenye kando mbili za mto Manjano kuna rasilimali nyingi ya maji na ardhi oevu, ardhi oevu nyingi zimejengwa kuwa sehemu za ikolojia za kilimo, ambazo zinatembelewa na watalii, eneo la ikolojia la Hujing la Mto Manjano ni moja kati ya maeneo hayo. Eneo la ikolojia la Fujing ya mto Manjano liko kwenye kando mbili kusini na kaskazini za mto Manjano, lina urefu wa kilomita 8 kwa kuambaa karibu na mto huo. Tofauti na maeneo mengine ya ikolojia ni kuwa eneo hilo la ikolojia lilianzishwa na kampuni ya ukoo wa Lian ya kundi la kampuni la Fujing. Wasimamizi wote kutoka wa ngazi ya juu hadi ngazi ya chini wanatoka katika ukoo wa Lian huko Taiwan. Mzee Lian aliyeanzisha eneo la ikolojia anaitwa kirafiki na wakazi wa huko kuwa Lao Lian. Mzee huyu ameleta chakula kitamu na michezo ya burudani ya Taiwan katika eneo hilo. Mtoto wa kaka wa Bw Lian alisema, "Eneo hilo limewekezwa na baba mdogo, kwani sisi watu wa Taiwan tunaona mto Manjano ni mto mama. Tukiwa hapa kando ya mto Manjano, tutatoa mchango wetu kwa watu wanaoishi hapa." Lao Lian ana hisia nyingi kuhusu maskani yake na China, amechimba ziwa moja kubwa lenye ukubwa wa hekta 40, ambalo linaitwa "ziwa Riyue", maana yake katika lugha ya Kichina ni ziwa la jua na mwezi. Ukingo wa ziwa unapindapinda, na ambapo imepandwa kanda mbili za miti, na wamefuga samaki maalumu laki 5 wa aina nyingi wa mto Manjano. Ndani ya eneo hilo kuna sehemu ya kuvua samaki kwa ndoano na sehemu ya kuogelea, ambazo ni mahali pazuri pa mapumziko. Watu wanaofika sehemu ya Huayuankou ya sasa, licha ya kuweza kufahamu historia yake, wanaweza kuona mandhari ya miti iliyojengwa katika zama mpya, kweli ni mahali pazuri pa kufahamu mambo ya zamani na kujiburudisha kwa mandhari nzuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako