• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makala ya pili ya Chenmsha bongo kuhusu Maonesho ya kimataifa ya Shanghai

    (GMT+08:00) 2010-03-09 18:20:54

    Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yatafunguliwa tarehe 1 Mei mwaka huu, maonesho hayo yatafanyika kwa siku 184, marafiki wa sehemu mbalimbali duniani wanakaribishwa kwenda kutembelea maonesho hayo. Leo tunawasomea makala ya pili ya chemsha bongo kuhusu Jumba la maonesho la China.

    Kabla ya kuwasomea makala hii, kwanza tunatoa maswali mawili ili wasikilizaji wetu muweze kufuatilia na kusikiliza vizuri, na baadaye kuyajibu. Maswali hayo ni: 1. Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yatafunguliwa tarehe ngapi? 2. Jumba la maonesho la China ni la rangi gani?

    Jumba la maonesho la China liko katikati ya eneo la Maonesho ya kimataifa ya Shanghai, nalo linaundwa na Jumba la maonesho la taifa la China, Jumba la maonesho ya sehemu mbalimbali za China na majumba ya maonesho ya Hong Kong, Makau na Taiwan. Katika Jumba la maonesho la China, watu wanaweza kujionea na kufahamishwa utamaduni wa China, fikra za wachina na mitizamo ya China juu ya thamani ya mambo.

    Eneo la maonesho ya Jumba la China ni kubwa zaidi kuliko mengine kwenye Maonesho ya kimataifa ya Shanghai, hata ukubwa wa paa lake ni kama ule wa viwanja viwili na nusu vya soka. Jumba la maonesho la China linaonekana na sura halisi ya kichina, umbo la jumba hilo linafuata kitu cha jadi cha "Douguan" cha utamaduni wa ujenzi wa majengo wa China, maana yake ni "taji la mfalme", rangi yake ni "nyekundu iliyotumika katika majumba ya wafalme wa China", jengo hilo linaonesha undani na sifa ya utamaduni wa China.

    Na usanifu wa Jumba la maonesho ya sehemu mbalimbali za China pia unaonesha sura na mtindo wa China, ambao umeiga usanifu mwingi wa ujenzi wa majengo ya zama za kale nchini China. Kwenye kuta za ujia wa nje wa jumba hilo, kuna maneno 34 ya Kichina yanayoonesha enzi mbalimbali katika zama za kale za China, ambayo ni kama alama ya historia ndefu na utamaduni wa taifa la China tangu enzi na dahari. Mikoa yote ya China itashiriki kwenye Maonesho ya kimataifa ya Shanghai, watu watakaotembelea maonesho hayo hakika watapata ujuzi kuhusu hali ya jumla ya sehemu mbalimbali nchini China.

    Na Jumba la maonesho ya Hong Kong linalenga kuonesha umaalum wa Hong Kong, pamoja na hadhi yake maalum ya kijioglafia, ujenzi wa miundo mbinu kamili, na mawasiliano barabara kati yake na dunia na miji ya sehemu mbalimbali nchini China; mfumo kamili wa mawasiliano barabarani na angani yanayoelekea sehemu mbalimbali, na huduma za uchukuzi zenye ufanisi kabisa; maendeleo mazuri ya majengo ya kufanya mawasiliano ya habari na upashanaji wa habari wa kisayansi na kiteknolojia bila kusita; mzunguko huria wa fedha, bidhaa na habari; mambo mbalimbali yanayopatana ya utamaduni wa China na wa nchi za nje, pamoja na maisha ya mjini yenye sifa bora yanayoonesha mambo mbalimbali yaliyovumbuliwa na ya maendeleo endelevu.

    Na umbo la Jumba la maonesho la Makau ni mithili ya "sungura wa jade" anayependeza, kuta za nje zimetengenezwa kwa plastiki ya kioo yenye matabaka mawili, ambayo rangi yake inaweza kubadilikabadilika bila kusita, huku inaweza kuonesha picha mbalimbali tofauti. "Kichwa cha Sungura" na "Mkia wa Sungura" ni maputo mawili ambayo yanaweza kupanda au kushuka kama yanavyopenda. Wakati wa Maonesho ya kimataifa ya Shanghai, kila mtu atakapotembelea Jumba la maonesho la Makau atapata zawadi ya taa moja yenye umbo la sungura.

    Na Jumba la maonesho la Taiwan linaundwa na majengo yenye umbo la mlima, "taa ya mbingu" ambayo ni taa kubwa ya kioo na pazia lenye umbo la mpira wenye taa ya LED. Mhandisi wa ujenzi alifahamisha kuwa, umbo la jumla hilo lilisanifiwa kutokana na umbo la taa ya Kong Ming ya zama za kale nchini China. Kong Ming alikuwa mtaalamu wa kijeshi katika zama za kale za China. Taa ya Kong Ming ni taa ya karatasi yenye umbo la mcheduara, sehemu yake ya chini iko wazi, taa ikiwashwa inaweza kuelea juu. Na kuwasha "taa ya mbingu", kuombea heri na baraka, kutazama filamu zitakazooneshwa kwenye pazia la mpira kuhusu "miji ya kimaumbile", "miji inayotarajiwa", hayo yatakuwa mambo muhimu yatakayooneshwa kwenye Jumba la maonesho la Taiwan.

    Sasa tunatoa tena maswali mawili: 1. Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yatafunguliwa tarehe ngapi? 2. Jumba la maonesho la China ni la rangi gani?


    1 2 3
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako