• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumba la maonesho la China katika Maonesho ya kimataifa ya Shanghai

    (GMT+08:00) 2010-03-15 18:03:28

    Jumba la maonesho la China, ambalo ni la nchi inayoandaa maonesho ya safari hii. Jengo hilo lenye umbo la tao na kimo cha mita 50 lina "rangi nyekundu ya kichina", jengo hilo lilijengwa kwa maboriti 56, jengo linapendeza na ni imara sana, baadhi ya vitu vidogo vya jengo hilo vinafanana na maandiko ya sanaa ya maneno ya kichina. Mkurugenzi msaidizi wa ofisi ya uongozi ya ujenzi wa mradi ya idara ya maonesho ya kimataifa ya Shanghai Bw. Ma Liang alisema,

    "Jumba la maonesho la China la rangi nyekundu linaundwa na maboriti 56 ikiwa ni alama ya mshikamano wa makabila 56, kwenye sehemu ya mwanzo wa kila boriti kuna neno moja la Kichina la maandiko ya Zhuan lenye maana 'mashariki', 'kusini', 'magharibi' na 'kaskazini' kwa kufuata upande linaoelekea boriti hilo."

    Msanifu wa Jumba la maonesho la China alisema jengo hilo ni alama ya nchi ya China, na ni mahali pa kuangalia utamaduni wa China, fikra ya wachina na mtazamo kuhusu thamani ya zama za sasa za China kwa watazamaji. Kumaliza kutembelea Jumba la maonesho la China kunahitaji dakika zaidi ya 40. Je tutaweza kuona vitu gani kwenye jengo hilo? Kwa ujumla watu wanaweza kuona vitu vitano, yaani ukumbi wa sinema, michoro, mazingira ya rangi ya kijani, na uzoefu na ufahamu".

    "Ukumbi wa sinema" ni kimoja cha vitu muhimu vya maonesho vya Jumba la maonesho la China. Ukumbi huo wa sinema si wa kawaida, bali ni ukumbi wa sinema wa kupata uzoefu, ambao unatumia vitu vya sanaa na teknolojia ya multimedia. Watu wataweza kuona sinema moja ya dakika 8 hivi. Filamu hiyo itaoneshwa kwa wakati mmoja kwenye mapazia matatu meupe ya pande tatu za mbele, kushoto na kulia, filamu hizo zitahusu jitihada na mafanikio ya ujenzi wa miji katika miaka 30 iliyopita tangu kuanza kwa mageuzi na sera za ufunguaji mlango, mambo yanatakayooneshwa ni kama kipande cha historia.

    "Mchoro mmoja", ni "Mchoro wa Qingmingshanghe", ambao ni mchoro maarufu wa kale wa China uliochorwa miaka zaidi ya elfu moja iliyopita. Katika Jumba la maonesho la China, mchoro huo umekuzwa kwa mara mia kadhaa, tena watu zaidi ya 600 waliochorwa humo ndani wote ni kama watu hai, tena inawaonesha watu maisha ya mitaani ya enzi ya Song toka asubuhi hadi jioni. Watazamaji watajiona kama wanaishi katika mazingira ya ustawi ya mji wa kale wa China. Mbali na mchoro huo, kuna vitu vingi vya thamani kubwa vinavyooneshwa vikiwa ni kama mfano wa ustaarabu wa miji ya China, vitu hivyo vyote vimepangwa kusafirishwa kwenda mjini Shanghai tarehe 10 Machi.

    Mkuu wa Jumba la maonesho la China wa idara ya Maonesho ya kimataifa ya Shanghai Bw Qian Zhiguang alisema, vitu vinavyooneshwa kwenye Jumba la maonesho la China ni majumuisho ya mambo ya jadi na ya kisasa, vinaonesha maendeleo ya historia. Alisema,

    "Maonesho kwenye Jumba la China yana vitu vingi vya jadi ya China, vikionesha urithi wa akili wa China, vikiwemo vitu vya kale vya utamaduni, lakini hatukusimama katika enzi za kale, umaalumu wetu ni kurithi na kukuza maendeleo ya enzi ya zamani kwa mfululizo."

    Kitu kingine ni "mazingira ya rangi ya kijani", maonesho ya jumba hilo ni masikilizano kati ya watu na watu, mapatano kati ya binadamu na maumbile, na mkakati wa maendeleo ya kuunganisha miji na vijiji katika siku za baadaye. Hivi sasa maandalizi ya maonesho yameingia kipindi cha utengenezaji. Kivutio kikubwa zaidi katika maonesho hayo ni maudhui yanayoitwa "Tuko katika upenu mmoja", ambayo yanaonesha uhusiano mzuri wa majirani katika miji ya baadaye. Vitu vya maudhui hayo sasa viko katika kipindi cha utengenezaji na upigaji wa video.

    "Uzoefu mmoja", katika Jumba la maonesho la China watazamaji wanaweza kupanda kwenye subway inayokwenda juu ya ardhi na kupita kwenye vivutio mbalimbali murua, katika burudani hiyo watu wanaweza kufahamu busara ya ujenzi wa miji ya China.

    "Ufahamu", kwenye sehemu ya chini ya Jumba la maonesho la China yenye kauli mbiu ya "Siku za baadaye za kiwango cha chini cha carbon" inafahamisha watu kuhusu mpango wa maendeleo uliotolewa na serikali ya China kuhusu kubana matumizi ya nishati, kupunguza utoaji wa uchafuzi na kiwango cha chini cha hewa ya carbon, na kuwaeleza watu mustakabali wa maendeleo ya aina mpya za nishati. Kwenye sehemu ya mwisho ya eneo hilo la maonesho kuna "chemchemi ya ufahamu" inayoeleza ipasavyo kuhusu maji. Kwa jumla, jengo la maonesho la China likitumia mtindo mpya kuwapa ufahamu kamili watazamaji kuhusu "busara za China katika maendeleo ya miji" kabla hawajaondoka katika jumba hilo.

    Mkuu wa Jumba la maonesho la China Bw Qian Zhiguang alisema, sehemu hiyo ya maonesho inatarajia kuonesha ufuatiliaji wa sasa na wazo la binadamu la kuchukua na kutumia ipasavyo maliasili za maumbile kwa teknolojia ya kisasa. Alisema,

    "Kiwango cha chini cha carbon kinaoneshwa kwenye Jumba la maonesho la China kama ifuatavyo: watazamaji mara tu baada ya kuingia ndani wanaona onyo linalosema, masuala yanayotukabili hivi sasa, hususan baada ya utandawazi wa viwanda yanazingatiwa na watu. Baada ya hapo kuna sehemu kadhaa, ambazo ya kwanza ni kuhusu kuchukua maliasili kwa njia mwafaka, licha ya kutumia mafuta ya asili ya petroli, tunapaswa kutumia zaidi nishati endelevu, zikiwa ni pamoja na upepo, mwangaza wa jua na ya viumbe. Ya pili ni kuhusu kubana matumizi ya nishati na kupunguza utoaji wa uchafuzi, tuwe na wazo la kupunguza utoaji wa uchafuzi katika maisha yetu ya kila siku. Sehemu ya tatu ni kiwango cha chini cha carbon, tunatakiwa kubadilisha hewa ya carbon dioxide inayotolewa kuwa yabisi."

    Katika sehemu mbalimbali za Jumba la China, watu wanaweza kuona "maji yanayotiririka", ambayo baadhi yake ni maji ya kweli, na nyingine ni maji ya bandia yanayoonekana kwa teknolojia ya kisasa, kitu kingine cha kushangaza ni "mtindo wa maji mapya". Mambo yote yaliyoko katika Jumba la maonesho la China yanaambatana na maji, ambayo ni mfano wa akili ya mashariki, vilevile ni matokeo kuhusu suala la upungufu wa rasilimali ya maji duniani, hususan yanaonesha hali ya kupatana kati ya watu na watu, kati ya watu na mazingira, kati ya miji, maendeleo na maumbile.

    Watazamaji wakifika katika Jumba la maonesho la China, ni muhimu sana wasisahau kupanda kwenye sehemu ya juu kuona ujia uliotundikwa huko, ambapo watu wanaweza kuona eneo lote la Maonesho ya kimataifa ya Shanghai na mandhari nzuri zilizoko kwenye kando mbili za mto Huangpu kwa kupitia vioo vilivyoko chini.

    Inakadiriwa kuwa Jumba la maonesho la China litakuwa moja kati ya majumba yatakayotembelewa na watu wengi katika kipindi cha maonesho, idadi ya watazamaji huenda itafikia laki 4 au 5 hivi, lakini uwezo wa jumba hilo la kupokea watazamaji ni elfu 50 tu, hivyo watazamaji wengi watashindwa kuingia ndani. Mkuu wa idara ya Maonesho ya kimataifa ya Shanghai Bw Hong Hao alisema,

    "Tutafuata utaratibu wa kujiandikisha kabla kwa kutimia mashine 180 zilizowekwa katika sehemu 23 ndani ya eneo la maonesho ya kimataifa ili kupunguza msongamano wa watu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako