• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wajumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa watoa mapendekezo kuhusu maendeleo ya uchumi katika sehemu za makabila madogo madogo yenye watu wachache

    (GMT+08:00) 2010-03-18 19:09:53

    Mkutano wa baraza la mashauriano ya kisiasa umefungwa hivi karibuni nchini China. Kwenye mkutano huo wajumbe kutoka sehemu za makabila madogo madogo yenye watu wachache walitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu maendeleo ya uchumi katika sehemu hizo. Nchini China kati ya makabila 55 madogo madogo, kuna makabila 22 yenye watu wasiofikia laki moja, na makabila hayo yanajulikana kuwa makabila madogo madogo yenye watu wachache.

    Kabila la Waheze lililoko katika sehemu ya kaskazini mashariki mwa China ni kabila dogo lenye historia ndefu. Takwimu za idadi ya watu zilizofanyika mwaka 2000 nchini China zinaonesha kuwa, idadi ya watu wa kabila hilo ilikuwa 4,640. Zamani waheze waliendesha maisha kwa kuvuvi samaki. Mjumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa kutoka kabila la Waheze Bw. Fu Gang, ambaye pia ni naibu mkuu wa wilaya ya Raohe mkoani Heilongjiang alisema, kutokana na mpango wa kustawisha sehemu za mbali na sera nyingine za kuwasaidia watu wa makabila madogo madogo zinazotekelezwa na serikali kuu, hali ya miundo mbinu katika sehemu ya waheze imeboreshwa, lakini waheze bado wanahitaji msaada wa kuwaongezea uwezo wa kutajirika.

    Bw. Fu Gang alisema, "Serikali inapaswa kuongeza nguvu ya kuzisaidia sehemu za makabila madogo madogo kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi, na kuandaa mafunzo mengi zaidi kwa watu wa makabila hayo. Kwa kuwa kitu muhimu zaidi katika kuendeleza uchumi ni watu wenye ujuzi. Sera za serikali kuu za kuzisaidia sehemu za makabila madogo madogo zinaweza kuboresha miundo mbinu tu, njia muhimu zaidi ya kubadilisha kabisa hali ya sehemu hizo kuwa nyuma kimaendeleo ni kuwaelimisha watu."

    Bw. Fu Gang alisema sehemu ya kabila la Waheze yenye mazingira mazuri ya asili inafaa kuendeleza utalii, na utalii si kama tu unaweza kuwasaidia waheze kuongeza mapato, bali pia unaweza kueneza utamaduni wa jadi wa kabila hilo. Alisema

    "Katika miaka kadhaa iliyopita, tumefanya majadiliano na majaribio kadhaa. Kama vile tulipanga wakulima wakubwa kulima mashamba mengi, na wakulima wengine kujishughulisha na shughuli za utalii. Kwani kabila la Waheze ni kabila ndogo sana, watalii wengi wanapenda kuja kuangalia maisha yetu. Shughuli za utalii zimewasaidia waheze kuongeza mapato, pia zimewahimiza kupanua upeo wa macho. Kwa kupitia shughuli hizo, waheze wamejua zaidi dunia ya nje, na uwezo wao wa kujiendeleza pia umeongezeka."

    Kabila la Wanu ambalo watu wake wanaishi hasa katika sehemu ya Mto Nujiang mkoani Yunnan lina idadi ya watu karibu elfu 30. Sehemu hiyo pia ina maliasili kubwa ya utalii. Lakini hadi sasa wanu wanajishughulisha na kazi ya jadi ya kilimo, na kiwango cha maisha yao bado ni chini. Mjumbe kutoka wilaya ya Nujiang Bw. Peng Zhaoqing alisema, hali hii hasa inatokana na hali duni ya mawasiliano ya barabara, kwani sehemu hiyo iko katika milima mirefu. Alisema, "Tuna matumaini kubwa serikali kuu itaongeza uwekezaji kwa ujenzi wa miundo mbinu katika sehemu ya Mto Nujiang. Nataka wilaya ya Nujiang itakuwa sehemu muhimu itakayopata msaada wa kupunguza umaskini kutoka serikali kuu. Nilipendekeza kuwa wilaya ya Nujiang itakuwa sehemu ya kufanyiwa jaribio la kutekeleza mpango wa kupunguza umaskini kote wilayani, ili kuhimiza ujenzi wa wilaya yetu katika sekta mbalimbali."

    Kabila la Wasara ambalo watu wake wanaishi hasa katika wilaya inayojiendesha ya kabila la Wasara ya Xunhua mkoani Qinghai lina idadi ya watu wasiofikia laki moja. Mjumbe kutoka kabila hilo Bw. Han Xingwang, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa Shirikisho la Viwanda na Biashara la Qinghai, alisema kabila la Wasara limepata misaada mingi kutoka serikali kuu, na maisha ya wasara yameboreshwa sana. Bw. Han Xingwang anamiliki shirika binafsi kubwa. Alisema kutokana na msaada wa serikali, kuendeleza mashirika binafsi kumekuwa njia nzuri ya kuendeleza kwa kasi makabila madogo madogo yenye watu wachache. Alisema, "Baada ya kupata msaada kutoka serikali, baadhi ya wasara wameanzisha mashirika binafsi au kujishughulisha na biashara. Sisi wasara wanafanya kazi kwa bidii, na naamini kuwa muda mfupi baadaye, tutaondoa umaskini, na wilaya yetu itakuwa moja kati ya wilaya iliyoendelea."

    Kati ya makabila 22 madogo madogo yenye watu wachache, makabila mengi yako katika sehemu za mipakani. Hivyo kuendeleza biashara za mipakani ni mkakati muhimu ya makabila hayo katika kuendeleza uchumi. Katika wilaya inayojiendesha ya kabila la Wakazkh ya Yili iliyoko kaskazini mashariki mwa mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, kuna makabila kdhaa madogo madogo yenye watu wasiofikia elfu 20 yakiwemo makabila ya Warussia, Watatar na Wauzbeki. Mababu ya watu wengi wa makabila hayo walitoka nchini Russia na nchi nyingine za Asia ya kati, hivyo lugha, utamaduni, mila na desturi za watu hao zinafanana na watu wa nchi za Asia ya kati. Kutokana na hali hiyo, katika miaka ya hivi karibuni njia ya kuendeleza uchumi ya wilaya ya Yili imerekebishwa. Hivi sasa wilaya hiyo imeanzisha kimsingi muundo maalumu wa shughuli za kiuchumi ambao nguzo yake ni kutengeneza na kuuza bidhaa kwa nchi za nje. Mwaka 2008, thamani ya mauzo ya bidhaa ya wilaya hiyo kwa nchi za nje ilifikia dola za kimarekani milioni 130, ambalo ni ongezeko la asilimia 83.4 kuliko mwaka 2007.

    Mjumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa kutoka mji wa Yining Bw. Luniov Ivanovic ni mkuu wa shule ya kabila la Warussia. Alisema shule yake inawafundisha wanafunzi kwa lugha za Kirussia na Kichina, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya uchumi mjini Yining. Alisema "Maendeleo ya sehemu yetu iliyoko mpakani yanategemea biashara za mipakani na sera nzuri ya serikali kuu, kama vile kuanzisha maeneo ya kuhimiza maendeleo, na kuchukua hatua za kutusaidia kuvutia uwekezaji kutoka nchi za nje."

    Bw. Ivanovic alisema serikali pia inawaalika watu wanaoshughulikia utamaduni na usanii kutoka nchi za Asia ya kati kutembelea mjini Yili mara kwa mara, ili kuhimiza mawasiliano kati ya pande hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako