• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanawake watimiza ndoto za kuanzisha shughuli zao

    (GMT+08:00) 2010-03-18 19:09:18

    Mikopo midogo inatatua suala la fedha kwa wanawake wanaoanzisha shughuli zao, lakini mwanzoni wakati wanaanzisha shughuli zao, huwa wanakabiliwa na changamoto nyingine mbalimbali. Ili kuwasaidia wanawake hao kukabiliana na changamoto hizo, "kituo cha kusaidia biashara" kilianzishwa, ambacho lengo lake ni kuyasaidia makampuni ambayo yako katika hatua ya mwanzo, ili ndoto ya wanawake kuhusu kuanzisha shughuli zao itimizwe.

    Kituo cha utoaji huduma kwa wanawake kuanzisha shughuli zao katika Shirikisho la wanawake la Tianjin kilianzishwa miaka 10 iliyopita kwa lengo la kuwaunga mkono wanawake wanaoanzisha shughuli zao. Katika miaka 10 iliyopita, makampuni zaidi ya 200 yaliyoanzishwa na wanawake yameendelezwa baada ya kusaidiwa na kituo hicho, na makampuni hayo yametoa moja kwa moja nafasi zaidi ya 65,000 za ajira kwa wanawake.

    Hivi sasa kuna makampuni 62 yaliyopiga kambi katika kituo hicho. Kampuni ya utoaji huduma kwa watoto cha Sunshower ni moja ya makampuni yanayopiga kambi mapema katika kituo hicho. Kutokana na kusaidiwa na kituo hicho, kampuni ya Sunshower imeendelezwa na kuwa kampuni yenye eneo la mita 200 za mraba na wafanyakazi kumi kadhaa inayoshughulikia mambo mbalimbali ya watoto kutoka duka la kinyozi wa watoto lenye wafanyakazi wawili au watatu tu. Meneja msaidizi wa kampuni ya Sunshower bibi Liu Ziyang alifahamisha kuwa, kampuni ya Sunshower imepata maendeleo ya kasi katika miaka mitano iliyopita, hii inatokana na uungaji mkono mkubwa wa kituo cha utoaji huduma kwa wanawake katika fedha na utoaji wa mafunzo. Alisema,

    "Hii inatokana na uungaji mkono wa kituo cha utoaji huduma kwa wanawake kuanzisha shughuli zao. Kituo hicho kinatoa bure mafunzo na maelekezo ya kuanzisha shughuli; katika upande wa fedha, kinatupatia mikopo isiyo na riba; pia kinafanya uenezi kwa ajili ya kampuni yetu kwenye mtandao wa internet, ambao unasaidia sana kuboresha sura ya kampuni yetu."

    Bibi Liu Ziyang alisema, wataalam wa kituo hicho sio tu wanaisaidia kampuni ya Sunshower kujenga tovuti yake, pia wanatoa mafunzo bure kuhusu elimu za kompyuta na mambo ya fedha, na usimamizi wa kampuni. Katika miaka 10 iliyopita kituo hicho kimetoa mafunzo kwa watu zaidi ya 60,000. Naibu mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Zhang Yufa alifahamisha kuwa, wanawake wanapoanzisha shughuli zao, wanakabiliwa na changamoto nyingi, hivyo lengo la kutoa mafunzo ni kuwasaidia wanawake wanaoanzisha shughuli zao kutatua masuala mbalimbali. Alisema,

    "Wanawake wanapaswa kubadili mtizamo wao, ambao zamani ulikuwa ni kupatiwa ajira, sasa uwe ni kuanzisha shughuli zao, na kuongeza nafasi za ajira kupitia kuanzisha shughuli zao, kubadili mtizamo huo ni muhimu. Wanawake wanaoanzisha shughuli zao pia wanakutana na masuala ya miradi, ushindani wa soko na fedha, hivyo kituo chetu kinalenga masuala hayo na kutoa mafunzo kadhaa, ili kuwasaidia wanawake kutatua masuala yao."

    Kituo hicho pia kilianzisha tovuti ya "Uwanja wa wanawake wa kaskazini wa kuanzisha shughuli kwenye mtandao wa internet", ambayo inatoa jukwaa la kuonesha bidhaa, kutoa habari na kufanya mawasiliano kwa makampuni, na kutoa huduma kwa pande zote kwa wanawake wanaoanzisha shughuli zao. Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanawake la Tianjin bibi Zhu Liping alisema,

    "Miradi mbalimbali ya biashara inapatikana kwenye tovuti hiyo, waanzishaji wa shughuli wanaweza kufuata hali yao ya fedha kutafuta miradi karibu 1,000 inayochaguliwa na wataalam, ambayo inahitaji fedha chache na hatari yake pia ni ndogo, hivyo inaweza kuwasaidia wanawake wawe kwenye 'hali ya juu' katika hatua ya mwanzo ya kuanzisha shughuli zao."

    Duka la kushona nguo iliyoanzishwa na mzee Xue Guiying, ambaye ana umri wa miaka 70, ilihamia kwenye kituo hicho mwezi Machi mwaka 2009. Hivi karibuni, alifanikiwa kufanya biashara yake ya kwanza kupitia tovuti ya "uwanja", na alifurahi sana. Alisema,

    "Mwanzoni wateja kutoka Beijing walitutumia vya nguo wanazotaka vipimo kupitia mtandao wa internet, nilikuwa na wasiwasi, kwa sababu hawakueleza kikamilifu vipimo vya nguo zao, lakini baada ya kumaliza utengenezaji wa nguo, walikuja kujaribu na nguo ziliwatosha, nilifurahi sana, kwani hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kupokea oda kupitia mtandao wa internet, nilijisikia vizuri, kwa kuwa watu kama sisi wenye umri mkubwa hatufahamu vizuri matumizi ya internet, hivyo niliona inafurahisha, na matokeo yake pia ni mazuri."

    Kwa kuwa kituo cha utoaji huduma kwa wanawake kuanzisha shughuli zao kinatoa misaada mbalimbali ikiwemo kodi ndogo na uenezi, duka la kushona nguo la mzee Xue linapata faida baada ya kuhamia kwenye kituo hicho. Bw. Zhang Yufa alisema aliona mwenyewe baadhi ya wanawake walipoanza kuanzisha shughuli zao, walipanda baiskeli na kuvaa nguo za kawaida, lakini baada ya miaka kadhaa, wamekuwa na magari na wanavaa nguo zenye chapa maarufu. Alisema kuboreshwa kwa maisha kumewawezesha waoneshe sura yao nzuri, jambo muhimu zaidi ni kwamba, wanawake wanapojiendeleza, hadhi yao kiuchumi pia inainuka, na hadhi yao katika familia na jamii pia inainuka. Bw. Zhang alisema,

    "Madhumuni ya kuanzisha kituo hicho ni kulinda haki za wanawake, na ulinzi huu wa haki unapaswa kuoneshwa katika kutatua hadhi ya wanawake. Kwa kuwa wanawake wakipunguzwa kazini, huwa wanapuuzwa, hivyo kama unawapa fursa ya kuanzisha shughuli na kupata ajira, hawatapuuzwa tena."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako