• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutalii kwenye jumba la maonesho la Australia

    (GMT+08:00) 2010-03-22 11:23:36

    Ikitajwa nchi ya Australia, pengine mnakumbuka jengo moja ambalo ni kama alama ya nchi hiyo, jengo hilo ndiyo jumba la maonesho ya michezo ya opera la Sydney; mnaweza kukumbuka ufukwe mzuri mrefu sana wa Bondi; mnaweza kufikiri kuogelea chini ya maji ya bahari na kutazama mandhari ya matumbawe; au kuwa karibu na ardhi ya rangi nyekundu pamoja na kundi kubwa la Kangaroo ... vitu hivyo maalumu vya Australia vitaoneshwa kwenye jumba la maonesho la nchi hiyo.

    Umbo la jumba la maonesho la Australia ni la muundo wa samaki, ukuta wa sehemu ya nje ina rangi ya udongo mwekundu. Kitu kinachostahili kuelezwa zaidi ni sehemu ya nje ya ukuta wa jengo hilo, ambayo imefunikwa kwa chuma cha pua maalumu kisichoingia kutu. Mwanzoni sehemu hiyo ya nje ya ukuta haikuwa ya rangi ya udongo mwekundu, bali ilikuwa nyeupe kama fedha. Baada ya kupigwa na mwangaza wa jua na maji ya mvua kwa muda mrefu, sehemu hiyo ya nje ikabadilika na kuwa ya rangi ya udongo mwekundu. Pengine wasikilizaji mtauliza, mbona watu wa Australia walikuwa na wazo hilo la uvumbuzi wa matumizi ya teknolojia na sayansi kama haya, na kuchagua rangi hii na umbo hili kwa jengo la maonesho la nchi yao? Msimamizi mkuu wa jumba la Australia Bw Peter Sams alisema,

    "Rangi ya nje ya jumba la maonesho ni rangi ya udongo mwekundu wa sehemu ya ndani ya Australia katika majira ya joto, na umbo la jengo hilo linafanana na mwambao wa Australia."

    Jumba la Australia katika maonesho ya kimataifa ya Shanghai linagawanyika katika sehemu 3 za kutalii, ugunduzi na wazo. Sehemu ya kwanza inaitwa "jiwe la msingi", ikitumia mbinu ya kueleza mambo halisi na ya kubuni inaonesha mabadiliko ya sura ya historia ya jamii ya Australia kutoka kipindi cha wakazi wenyeji wa asili hadi sasa. Watu wakipita kwenye eneo hilo wanasikia kama wanapita kipindi cha kale hadi cha hivi sasa hata cha siku za baadaye cha historia ya nchi hiyo, mabadiliko na maendeleo ya ustaarabu yanavutia watazamaji. Wasanii wakazi wa asili kutoka sehemu ya kaskazini ya Australia walioko katika maonesho wakichonga vitu vya sanaa kwa kutumia mawe na mbao, na kuonesha utamaduni wa kale wa nchi hii kwa kutumia sanaa ya kale. Bw Peter Sams alisema, kila mchoro ulioko katika vitu hivyo vya sanaa ina maana maalumu na ni alama ya utamaduni wa Australia, lakini Bw Sams hakueleza siri yake,

    "Hii ni michoro halisi ya ukutani ya wakazi wa asili wa Australia, michoro hiyo ni yenye maana muhimu sana ni yenye hadithi na visa mbalimbali, tutawaeleza watazamaji baada ya maonesho kuanza rasmi."

    Mbali na hayo, mambo muhimu zaidi ya 20 katika historia ya nchi hiyo, yakiwemo maonesho ya Brisbane ya mwaka 1998 na michezo ya Olimpiki ya Sydney ya mwaka 2000, yote yanaoneshwa kwenye eneo hilo kwa watazamaji.

    Bahari ni kitu kinachohusiana sana na Australia. Kwenye eneo linaloitwa "Jiwe la Msingi", wasanii walibuni vitu vinavyohusiana na bahari vikiwemo picha ya mawe yaliyochongwa na michoro ya rangi ya ukutani; watazamaji wanaweza kuona mawimbi makubwa, anga ya buluu na ufukwe mrefu, tena wanaweza kuhisi maisha ya furaha ya wakazi wa sehemu ya pwani.

    Jumba la Australia lililoko kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai ni kubwa zaidi limegharimu fedha nyingi zaidi tangu nchi hiyo ianze kushiriki kwenye maonesho ya kimataifa. Jumba la Australia liko karibu na jumba la maonesho la China kwa upande wa kusini mashariki, watu wanaweza kuona jumba la China kupitia madirisha ya jumba la maonesho. Bw Peter Sams alisema, Australia inatarajia sana kuimarisha uhusiano wa kirafiki na China, nchi inayoandaa maonesho ya kimataifa, kwa hiyo wakati wa kupanga vitu vya maonesho, walizingatia kujihusisha na China katika mambo ya maonesho. Kwa mfano, kwenye sehemu ya kwanza ya maonesho itaoneshwa filamu inayoitwa "kina dada".

    "Sehemu hii itaoneshwa sinema moja fupi ya dakika mbili hivi inayoitwa 'kina dada', ambayo inawafahamisha watazamaji wanawake hodari 25 wa Australia na wa China walioko nchini Australia pamoja na mafanikio yao. Kipande kimoja katika filamu hiyo ni kuhusu mwanamke mmoja wa Australia aliyewaokoa wanyama wakati yalipotokea maafa ya moto msituni, kipande hiki cha filamu kinafanana na kisa cha mwanamke mmoja aliyewaokoa Panda wakati lilipotokea tetemeko la ardhi mkoani Sichuan."

    Kwenye sehemu ya pili ya maonesho kuna ukumbi wa michezo unaoweza kuchukua watu 1,000, ambapo skrini yake kubwa inaweza kuzunguka na kusogezwa juu na chini. Ni tofauti na hali ya kihistoria inayooneshwa kwenye sehemu ya maonesho ya "Jiwe la Msingi", sehemu hiyo ya maonesho ya jumba la mviringo itaonesha wazo la watu wa Australia kuhusu maendeleo ya miji katika siku za mbele kwa kupitia skrini hiyo kubwa, watazamaji wataona uvumbuzi na vivutio vya teknolojia na sayansi, licha ya kuona maajabu mengi, watu watakuwa na matarajio kuhusu siku za baadaye. Bw Sams alisema, kuonesha sanaa ya video na sauti kwa skrini kama hili ni nadra sana hata nchini Australia, Hii ni mara ya kwanza kwa Australia kutumia wazo na teknolojia ya uvumbuzi kwenye maonesho ya kimataifa. Alisema,

    "Pazia hilo ni kubwa sana, ambalo lilijengwa kwa kutumia tani 36 za nondo, linaweza kuzunguka mzunguko mmoja kwa dakika moja. Kauli mbiu inayooneshwa ni kuhusu matarajio ya watu wa Australia kuhusu maisha ya baadaye, wanatarajia kuwa miji yao katika siku za baadaye itakuwa mizuri zaidi. Hii ni mara yetu ya kwanza kuwaonesha watazamaji teknolojia hii ya utengenezaji na mradi huo."

    Baada ya kutoka kwenye eneo hilo lenye maajabu mengi na sayansi na teknolojia ya kiwango cha juu, watu wanaingia kwenye sehemu ya tatu ya maonesho, ambapo watu wataburudishwa kwa vitu vya sanaa na burudani. Sehemu hiyo ina vinyago vikubwa 7 vyenye kimo cha mita 10, vikiwa ni maua ya alama za majimbo 7 ya Australia. Katika kipindi cha maonesho ya kimataifa, wasanii hodari wa Australia watawaonesha watazamaji muziki wa Hip-Hop, muziki wa Jazz, michezo ya ngonjera na kuimba, pamoja na nyimbo na ngoma za asili za huko. Kwa watu wanaopenda utamaduni na mandhari ya pwani au wanaopenda chakula maalumu cha Australia, wanaweza kupata bia halisi ya Australia na nyama ya Kangaroo kwenye jumba la Australia. Bw Peter Sams alisema,

    "Tutawapatia watu vyakula mbalimbali vitamu, kwa mfano, huenda tutawapa nyama ya Kangaroo, licha ya hayo tutawapa bia na pombe ya Australia. Chakula ni safi tena ni cha kiwango cha juu, lakini chakula kitakachotolewa ni chepesi kutokana na idadi kubwa ya watazamaji."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako