Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Zhong Shan ambaye yuko ziarani mjini Washington tarehe 24 na 25 alikutana na maofisa wa nagazi ya juu wa serikali ya Marekani, na kufanya mazungumzo nao kuhusu uwiano wa biashara kati ya China na Marekani, mikwaruzano ya biashara na masuala mengine yanayohusu mambo ya biashara.
Katika ziara hiyo, Bw. Zhong alikutana na maofisa wengi wa serikali, wakiwemo naibu waziri mteule wa biashara wa Marekani Bw. Francisco Sanchez, naibu mjumbe wa biashara Bw. Demetrios Marantis na nabibu waziri wa mambo ya nje Bw. Robert D. Hormats.
Bw. Zhong alipokutana na maofisa hao alisema, uzoefu umethibitisha kuwa uhusiano mzuri wenye utulivu kati ya China na Marekani unalingana na maslahi makuu ya nchi hizi mbili. Anataka pande hizi mbili zitupie macho siku za mbele wakati wa kushughulikia uhusiano wa kibiashara kwa njia ya kimkakati, na kufanya juhudi za kutafuta na kuzidisha maslahi ya pamoja, ili kusukuma mbele uhusiano wa kibiashara kati ya pande hizi mbili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |