• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mikopo iliyotolewa na benki yawasaida wanawake kufanya biashara ndogondogo

    (GMT+08:00) 2010-03-29 15:03:45

    Msemo mmoja wa kiafrika unasema kuwa mwanamke ni mizizi ya familia. Ama kwa hakika mti ukinyunyiziwa maji ya kutosha, mizizi zinaota arthini ili kupata virutubisho ambazo zinaukuza na kufanya shina, matawi, majani na matunda kunawiri. Msemo huu unamithilisha mwanamke kuwa ni mizizi, na shina kuwa ni mumewe. Matawi, majani na matunda ni watoto na maendeleo katika familia na jamii anayoishi mama huyo.

    Lakini, pia tunajua kuwa mila na utamaduni wa Afrika haimthamini mwanamke kuwa msaidizi nyumbani na pia kumsaidia mumewe kutafuta mahitaji ya maisha. Lakini, mambo haya bado yanafuatiliwa katika karne hii? Ripota wetu Lucy Morangi alichunguza jambo hili na ameleta ripoti hii

    Kwa miaka nyingi sasa jamii ya kiafrika imekuwa ikizingatia mwanamke kama msaidizi nyumbani. Tangu utotoni, mtoto msichana anafunzwa jinsi ya kutunza familia yake katika hali ya kupika, usafi na kulea watoto. Yeye anahitajika tu kumtunza mumewe anaporudi nyumbani baada ya mchana kutwa kutafuta pesa za kukimu mahitaji ya nyumbani. Lakini gharama za maisha zimeongezeka na mengi yanahitajika. Kama mwanamke ndiye mizizi ya familia, basi anahitajika kufanya mengi zaidi na kukaa nyumbani?

    Nilitembelea eneo moja lililo umbali wa kilomita 20 kutoka mjini Nairobi. Nilimpata rafiki yangu mmoja aliye pia mkazi wa eneo hilo. James Kinuthia ni mlinzi katika mtaa mmoja wa mabwenyeye ya spring valley ambayo ni kama kilomita tano kutoka wangige. Nilimuuliza anielekeze kwa mfanya biashara mwanamke anayenawiri katika eneo hilo, naye hakusita kuniambia juu ya Margaret Mwikali

    Tuliandamana hadi kibanda cha Margaret na tukampata yuko katika pilikapilika za kuwahudumia wateja waliozingira mahala pake pa biashara. Kibanda chenyewe sio kikubwa. Ni muundo wa meza takribani futi sita kwa futi nne. Yeye anauza mboga na matunda na kando pia niliona mtugi na chupa. Ni wazi kuwa vilikuwa vipimo vya kuuzia mafuta ya taa ambayo ni maarufu ya kutumia kupikia. Margaret ana umri wa miaka 46 na ni mchangamfu sana. Ni nini kilimfanya kuanzisha biashara hii?

    Kufuatia kupata mkopo huo na kupanua bisahara yake, sasa kiwango cha maisha cha familia yake kimeimarika. Anasema:

    Kutoka hapo nilielekea kwenye benki ambayo Margaret na wenzake waliweza kupata mkopo wao. Nilikutana naye Bw. Titus Chweya aliye afisa anayehusika na utoaji mikopo kwa vikundi vya kina mama kuanzisha biashara ndogondogo. Nilimwuliza kwa nini benki hiyo imewaangazia kina mama na vijana zaidi. .

    Titus anasema kuwa asilimia 99 ya vikundi hivi vinalipa kikamilifu mikopo wanayopokea kutoka kwenye benki. Aliongeza kuwa kama vile mti unanawiri na kuzaa matunda mengi kama unapata maji na rotuba nzuri ya ardhi, jamii na bara nzima la Afrika inanufaika kutoka kwa biashara hizi ndogo wanazoziendesha kina mama.

    Afisa wa nyanjani Martha Kanyingi kuto wa benki hii anayeshughulika na kusimamia vikundi hivi hasa ya Margaret, anasema kuwa kuna tofauti kubwa inayoonekana wakati kikundi kinapoanza kupata mkopo na wakati wanaanza kurudisha pesa hizo

    Benki kuu ya Kenya inasema kwenye ripoti yake kuwa biashara ndogo zinachangia asilimia 75 pato la jumla la kitaifa. Katika washa iliyowaleta pamoja wakurugenzi wa benki kuu barani Afrika iliyofanyika hapa Nairobi mwaka uliopita, wakurugenzi hawa walisema kuwa biashara hizi ndogo ndizo zitaendeleza uchumi wa Afrika hasa wakati ulimwengu unapokabiliana na hali mbaya ya kiuchumi. Basi msemo huo wa Afrika unaosema kuwa mwanamke ni mzizi wa familia, unaashiria kuwa, familia sio tu baba na watoto bali pia jamii, taifa na bara lote kwa jumla hunufaika na na bidii na wajibu wa wanawake. Nikiripotia CRI Nairobi, mimi ni Lucy Morangi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako