• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Austria

    (GMT+08:00) 2010-03-29 18:12:16

    Wakati mnaposikia muziki unaoitwa "Mto Bluu Danube", pengine mnaweza kufikiri kuhusu nchi ya muziki Austria.

    Austria iliandaa maoneshoya kimataifa ya Vienna mwaka 1873. Watu wa Austria licha ya kuleta muziki wa dansi ya Waltz, ambao ulivuma sana kwenye maonesho ya kimataifa ya karne ya 19, kwenye maoneshoya kimataifa ya Shanghai ya mwaka 2010, watawaonesha watazamaji kuhusu mawazo yao yasiyo ya kawaida kuhusu nchi hiyo ya muziki. Kwenye jumba la maonesho la Austria kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai, watu wa Austria wenye mambo mengi ya kuvutia na mawazo yasiyo ya kawaida, watawaletea watazamaji furaha na uzoefu wa theluji na barafu. Naibu mwakilishi mkuu wa jumba la maonesho la Austria Bi Birgit Murr alisema, ujoto wa ukumbi wa kwanza wa maonesho ya Austria utakuwa chini ya nyuzi 15 sentigredi ili kuwafanya watazamaji wahisi mazingira ya theluji na barafu. Alisema,

    "Kwenye sehemu ya chini ya jumba la Maonesho, watazamaji mara tu baada ya kuingia kwenye ukumbi wa kwanza, wataona kama wako mlimani, kwa sababu kuna baridi. Kuna eneo moja ardhi lenye theluji na barafu ya kweli. Watazamaji wataweza kuchezea theluji na kutengengeza mabonge ya theluji. Vilevile wanaweza kutupa mabonge ya theluji kwenye ukuta, ambapo zitajitokeza picha ya vitu."

    Mafundi walisema ukuta ule unaweza kutambua kasi ya mabonge yaliyotupwa na watu, na kujitokeza picha tofauti, pengine bonge la theluji linalorushwa linaweza kusababisha maporomoko ya theluji kwenye mlima. Lakini inawezekana vipi kutengeneza mazingira ya theluji na barafu katika majira ya joto? Mafundi walisema, wanatumia teknolojia ya kuleta baridi kwa dawa ya maji ya baridi sana, ili kudumisha hewa ya ukumbini iwe kwenye nyuzi 15 hivi. Kwenye jumba la Austria, waandaaji wataleta wasanii wa video na sauti, wataonesha maisha ya miji na vijiji vya Austria kwa teknolojia ya 3D.

    Baada ya kutelemka kwenye mlima Alps wenye theluji na barafu, watu wanaweza kufika kwenye misitu ya nchi hiyo. Karibu nusu ya eneo la nchi hiyo inafunikwa na misitu, hali hii itaoneshwa kwenye jumba la maoneshola Austria kwenye maoneshoya kimataifa ya Shanghai. Kwenye sehemu ya maonesho, watu wataweza kujionea hewa safi ya msituni, miti ya aina mbalimbali pamoja na harufu nzuri ya uyoga. Sauti za majani ya miti kukwaruzana, milio ya ndege pamoja na mluzi unaosikika mara kwa mara. Msituni licha ya mabadiliko ya mwanga, pia kuna sauti inayoambatana na mwanga huo. Bi Birgit Murr alisema,

    "Baada ya kutoka mlimani, watu wanaingia msituni, ambapo kuna sauti mbalimbali, milio ya ndege na mbwa, tena kuna mtu anayepiga mluzi. Kwenye eneo la msitu, watazamaji wataweza kuona mabadiliko ya majira manne, watu wataona tofauti ya mazingira. Kuta za mle ndani zikiguswa na watazamaji picha mbalimbali tofauti zitajitokeza."

    Mbali na mazingira ya sehemu ya vijijini, watu wataweza kuona mazingira ya miji mikubwa ya Austria, Ambapo watu wataweza kuona bendi zinazopiga muziki wa Austria wa Mozart na Strauss. Aidha, zitaoneshwa hali ya mawasiliano ya mijini, teknolojia ya hifadhi ya mazingira ya maumbile, aina mpya za nishati na uzalishaji mali kwa kutumia teknolojia mpya.

    Kwenye jumba la Austria, watu licha ya kuweza kupata uzoefu katika kutazama, kusikia, kugusa na kwa harufu, watu pia watapata uzoefu wa kuonja chakula. Kwenye ghorofa la jumba la maoneshowapishi kutoka Austria wataonesha ustadi wao wa kupika chakula cha jadi cha nchi hiyo. Bi Birgit Murr alisema,

    "Kwenye ukumbi wa chakula ulioko kwenye ghorofa, watu wataweza kupata chakula, vinywaji na bia za Austria. Wapishi wote ni watu kutoka Austria, watazamaji watapata uzoefu wa Austria."

    Kuhusu kununua vitu, wanawake wanaopenda fuwele inabidi wawe macho, kwani kuna duka moja la zawadi kwenye jumba la maoneshola Austria, watu wataweza kununua vitu vya fuwele ambavyo ni maarufu sana duniani. Kwenye chemchemi na ngazi za umeme ukumbini, watu wataweza kuona mapambo yaliyotengenezwa kwa fuwele, watu wanapoingia katika jumba la maonesho la Austria, licha ya kuweza kuona mandhari ya kimaumbile, pia wataweza kuona mapambo ya fuwele. Watu wa Austria pia wanazingatia sana maingiliano ya kiutamaduni na China, kwa kuwa maoneshohayo ya kimataifa yanaandaliwa na China, kwa hiyo yanapaswa kuonesha umaalumu wa China, hivyo wasanifu wataweka vitu vya kauri vinavyowakilisha utamaduni wa nchi mbili kwenye sehemu ya nje ya ukuta wa jumba la maoensho. Ili kuonesha wazo la wachina la "Salama kila mwaka", vipande vidogo vya vyombo vya kauri vilivyovunjika vya rangi nyekundu na nyeupe zaidi ya milioni 10 vitabandikwa ukutani. Bw Matia del Campo, ambaye ni mmoja kati ya wasanifu wa jengo hilo, alisema,

    "Austria ni nchi iliyoanza mapema zaidi shughuli za kutengeneza vyombo vya udongo wa mfinyanzi na kauri katika zamani za kale barani Ulaya, Austria inatia maanani sana vyombo vya kauri, kwa hiyo tunataka kuonesha kitu cha namna moja katika utamaduni wa nchi zetu mbili. Tumesikia kuwa vipande vidogo vya vyombo vya kauri vilivyovunjika ni vitu vya baraka, kwa hiyo tumetumia vipande vidogo vya kauri milioni 10 hapa."

    Aidha Austria imetumia neno la Kichina "人"(ren)maana yake ni mtu, na herufi ya Kingereza ya "A" kama alama ya jengo la maonesho ili kuonesha maingiliano ya utamaduni wa China na Austria.

    Austria inaitwa nchi ya muziki, katika siku ya jumba la maonesho la Austria, bendi maarufu ya duniani "Vienna Philharmonic Orchestra" na bendi ya "China National Symphony Orchestra" zitafanya maonesho ya muziki kwa ushirikiano. Mbali na wanamuziki maarufu kufanya maoensho, Austria pia itaandaa mashindano ya piano nchini China kwa kutumia nafasi ya kushiriki maoneshoya kimataifa, na itawashirikisha wanafunzi wenye umri wa miaka 14 hadi 18 wa shule za muziki zilizoko katika sehemu mbalimbali za China. Mwandaaji wa mashindano hayo, Bi Bai Lin, ambaye ni balozi wa heshima wa jumba la Austria kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai, alisema:

    "Tumeamua kuandaa mashindano ya piano, ili kuwahimiza wanafunzi wa chuo kikuu cha muziki cha China, tunataka chuo kikuu cha muziki cha Austria na wanafunzi wake watunge muziki, muziki huo utapigwa na wanafunzi wa chuo kikuu cha muziki cha China, siyo njia ile ya kawaida, bali ni kupiga muziki kwenye piano yenye miguu minne, inaitwa pedali ya mapatano, huu ni uvumbuzi mpya, pedali hiyo ya nne itafikia kiwango kipya cha teknolojia na sauti ya piano."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako