• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua 0330

    (GMT+08:00) 2010-03-30 17:05:11

    Barua ya kwanza inatoka kwa msikilizaji wetu Mwanahawa Akoth wa S.L,P 34-40602 Ndori Kenya, anasema ni matumaini yangu kuwa hamjambo na mmeuanza mwaka huu kwa bashasha, mbwembwe na matumaini makubwa, pokeeni zangu salamu na matumaini ya mwaka mpya wa 2010.

    Lengo la kuandika barua hii ni kuwashukuru kwa kile mlichonitumia ikiwa ni bahasha iliyolipwa na kadi mbili za salamu, ahsante. Naomba kutumiwa kalenda ya mwaka huu wa 2010 pamoja na majarida mbalimbali yanayochapishwa huko kama vile China today na China pictorial.

    Kwa kumalizia natoa shukrani zangu na pongezi nyingi kwa namna mnavyotuhudumia sisi wasikilizaji, ningewahimiza kuwa kazi hiyo nzuri muiendeleze, na kwa upande wetu sisi wasikilizaji tunapaswa kuzidisha kutumiana salamu na kusikiliza Idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa, mwisho nawapa pole wananchi wote wa China waliokumbwa na balaa mwaka uliopita, Mungu atawaepusha balaa nyingine kama hizo kwa siku za usoni.

    Shukran nyingi sana Bibi Mwanahawa Akoth kwa barua yako, ambayo umetujuulisha kuwa umepokea bahasha pamoja na kadi, kuhusu kalenda ya mwaka 2010 tayari tumeshatuma kwa wasikilizaji wetu labda imechelewa kukufikia hivyo vuta subira.

    Barua nyingine inatoka kwa msikilizaji wetu Halima Ijeiza wa S.L.P 14-40602 ndori Kenya, anasema namshukuru Maulana kwa kupata fursa hii ya kuwasabahi na kuwatakieni habari njema ya mwaka mpya, ni matumaini yangu kuwa mnaendelea kuchapa kazi kama kawaida yenu, nawapongeza sana kwa kazi yenu ya kutupasha habari mbalimbali, salamu na burudani ya muziki. Aidha nashukuru kwa kadi za salamu, bahasha iliyolipwa na kalenda nzuri ya mwaka 2010, nafurahia sana zawadi zote mnazonitumia mara kwa mara hususan zawadi zinazotokana na ushindi wa Chemsha bongo, je mtatuleta tena lini mashindano hayo?

    Sasa nachukua fursa hii kuipongeza serikali ya China kwa kuwa mstari wa mbele kuisaidia serikali na watu wa Haiti walipokumbwa na balaa la tetemeko la ardhi. Na si hayo tu bali misaada mingi kwa nchi za Afrika na hasa nchi yangu ya Kenya Mungu ibariki serikali ya China, Mungu ibariki Afrika.

    Kwanza tunakushukuru sana Bibi Halima Ijeiza kwa kututakia heri ya mwaka mpya, na tunapenda kukutaarifu kuwa chemsha bongo nyengine imeanza kuhusu maonesho ya kimataifa ya Shanghai, tafadhali ifuatilie. Aidha kuhusu China inavyojitahidi katika kusaidia nchi zinazokumbwa na majanga, hili ni jambo jema kwa rafiki yeyote kumsaidia mwenziwe pale anapokumbwa na tatizo lolote na ndio maana China inasaidia nchi yoyote inayofikwa na maafa bila kubagua.

    Barua nyingine inatoka kwa Mahimana Theophile wa kambi ya wakimbizi Maratane S.L.P 173, Nampula Msumbiji. Anaanza kwa kusema kwanza ninashukuru kwa barua mliyonitumia tarehe 12 mwezi wa 6 mwaka 2009. ningependa kuwafahamisha kwamba barua hii imechelewa sana kunifikia, kwa hiyo ni bora zaidi kunitumia barua zenu kupitia mtandao wa intanet ili niweze kupima bahati yangu kwa maana sisi ambao tunaishi katika bara la Afrika barua huwa zinatufikia kwa tabu. Tena nashukuru kwa jinsi mnavyofanya jitihida zote ili kuwepo mawasiliano.


    1 2
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako