• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mzee mwenye umri wa miaka 70 aanzisha duka la kushona nguo

    (GMT+08:00) 2010-04-01 15:33:59

    Kutokana na misaada ya "mikopo midogo" na "kituo cha kusaidia biashara" inayotolewa na Shirikisho la wanawake la Tianjin, wanawake wengi mjini Tianjin wamepata ajira na hata wameanzisha shughuli zao kwa mafanikio. Mzee Xue Guiying, ambaye ametimiza umri wa miaka 70 ni mmoja wao.

    Mwezi Machi mwaka 2009, mzee Xue Guiying alianzisha duka la kushona nguo, ambalo linasanifu nguo zinazofaa wanawake wanaofanya kazi ofisini au ni waalimu. Hivi sasa duka hilo linajulikana sana mjini Tianjin.

    Kabla ya kustaafu, mzee Xue Guiying alikuwa mwalimu wa shule ya sekondari, hivyo watu humwita mwalimu Xue. Alisema kazi yake mpya ya sasa ni tofauti sana na kazi yake ya zamani. Lakini siku zote anapenda usanifu wa nguo, na kuwa msanifu wa nguo kulikuwa ni ndoto yake, hivyo alipokuwa kijana alisoma vitabu vya usanifu wa nguo, na kwenda kujifunza ushonaji wa nguo. Lakini kutokana na sababu mbalimbali, ndoto ya mwalimu Xue haikutimizwa.

    Lakini siku moja kulikuwa na fursa moja. Rafiki wa mwalimu Xue alimshauri apige kambi kwenye kituo cha utoaji huduma kwa wanawake kuanzisha shughuli zao, na kuanzisha duka la kushona nguo, ili kutimiza ndoto yake. Mwalimu Xue alisema,

    "Rafiki yangu aliniambia niende kwenye kituo cha utoaji huduma kwa wanawake, alisema pale kuna wanawake wengi wanaoanzisha shughuli zao, pia kuna wateja wengi, vilevile watu wengi wanakwenda pale kujifunza, ambapo kuna fursa nyingi kuliko sehemu nyingine, hivyo niliamua kujaribu, nilifikiri kuwa naweza kujifunza mambo mengi pale."

    Kituo cha utoaji huduma kwa wanawake kuanzisha shughuli zao mjini Tianjin ni "kituo cha kusaidia biashara" kinachowaunga mkono wanawake wanaoanzisha shughuli zao. "Kituo cha kusaidia biashara" kinatoa uungaji mkono mbalimbali kwa makampuni ambayo yako katika hatua ya mwanzo, ili makampuni hayo yaweze kuendelezwa.

    Baada ya kupiga kambi kwa mafanikio kwenye kituo hicho, mwalimu Xue alipewa mafunzo mbalimbali bure, ambayo ni pamoja na ujuzi wa kompyuta, mambo ya fedha, usimamizi wa makampuni na ufundi mbalimbali. Baadaye "duka la kushona nguo kwa wanawake wasomi" lilianzishwa katika ofisi ya ghorofa ya pili ya kituo hicho.

    Kuna usemi usemao "mwanzo ni mgumu". Katika kipindi cha mwanzo duka hilo lilipoanzishwa, kwa kuwa halikujulikana kwa watu wengi, na biashara ya nguo ilikuwa ngumu, hivyo biashara ya duka hilo haikuwa nzuri, hata hakuweza kulipa kodi. Mwalimu Xue alisema,

    "Mwanzoni mapato yalikuwa madogo hata hayakutosha kulipa kodi, lakini sasa hali inaelekea kuwa nzuri, baada ya kulipa kodi, tutabaki faida kidogo, kwa uchache sasa hatupati hasara. Mwanzoni tulikuwa tunapata hasara, ilikuwa vigumu, lakini niliamini kuwa tutaelekea katika hali nzuri hatua baada ya hatua, hivyo nimeshikilia hadi sasa."

    Kutokana na misaada ya kituo cha utoaji huduma kwa wanawake kuanzisha shughuli zao, biashara ya mwalimu Xue imekuwa nzuri siku hadi siku, na anaweza kupata faida.

    Tarehe 15 Januari mwaka huu, kituo cha utoaji huduma kwa wanawake kuanzisha shughuli zao kilianzisha tovuti yake, ambayo inatoa jukwaa kwa makampuni kuonesha bidhaa zao, kutoa habari, na kufanya mawasiliano na kusaidiana, pia inawaalika wataalam kutoa mafunzo kwenye mtandao wa internet, ili kutoa huduma kwa pande zote kwa watu wanaoanzisha shughuli zao.

    Baada ya tovuti hiyo kuanzishwa, mwalimu Xue alianza kufanya biashara yake kwenye mtandao wa internet. Ikilinganishwa na njia ya jadi ya wateja kuja wenyewe kununua nguo, njia hiyo ya ununuzi kwenye mtandao wa internet inamsaidia kwa kiasi kikubwa mwalimu Xue kufanya biashara. Alipozungumzia biashara yake ya kwanza kwenye mtandao wa internet, mwalimu Xue alifurahi sana. Alisema,

    "Mwanzoni wateja kutoka Beijing walitutumia vipimo vya nguo wanazotaka kupitia mtandao wa internet, nilikuwa na wasiwasi, kwa sababu hawakueleza kikamilifu vipimo vya nguo zao, lakini baada ya kumaliza utengenezaji wa nguo, walikuja kujaribu na nguo ziliwatosha, nilifurahi sana, kwani hii ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kupokea oda kupitia mtandao wa internet, nilijisikia vizuri, kwa kuwa watu kama sisi wenye umri mkubwa hatufahamu vizuri matumizi ya internet, hivyo niliona inafurahisha, na matokeo yake pia ni mazuri."

    Hivi sasa duka hilo la mwalimu Xue limekuwa kampuni ya "nyota maarufu" katika kituo cha utoaji huduma kwa wanawake kuanzisha shughuli zao mjini Tianjin, na mwalimu Xue pia anapanga kuendelea kupiga kambi katika kituo hicho, na kujiendeleza pamoja na kituo hicho. Alipozungumzia misaada aliyopata kutoka kwenye kituo hicho, alisema,

    "Wateja wangu wanaongezeka siku hadi siku, na duka langu linazidi kujulikana. Wao wananisaidia sana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako