• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaa wa Jinli wenye utamaduni wa jadi, mkoani Sichuan

    (GMT+08:00) 2010-04-12 17:07:19

    Mtaa wa Jinli wa mji wa Chengdu, mji mkuu wa mkoa wa Sichuan ni mtaa wenye umaalumu wa utamaduni wa jadi wa wenyeji wa huko. Mtaa huu unaonesha desturi na maisha ya wakazi wenyeji yenye umaalumu wa Sichuan.

    Jinli iko kwenye sehemu ya kusini ya mji wa Chengdu, mtaa huu wenye urefu wa mita zaidi ya 350 ni mtaa wa kupumzika wenye mtindo wa tarafa ya kale. Baada ya kupita kwenye lango kubwa lililotundikwa taa mbili kubwa za sanaa ya jadi za rangi nyekundu, kuna barabara ya kale iliyotandikwa vipande vyembamba vya mawe ya rangi ya kijivu kizito, majengo yaliyoko kwenye kando mbili za barabara yote ni ya mtindo wa kale, maduka na mikahawa iliyoko huko yana ghorofa moja au mbili tu, kuta za matofali ya rangi ya kijivu nzito na nguzo za rangi nyekundu iliyokolea ni za kale. Maduka yaliyoko kwenye mtaa huu mengi zaidi yanauza vyombo na vitu vya sanaa vya kale vikiwa ni pamoja na vyombo vya kauri na vitu vya sanaa vya kazi za mikono. Mtalii kutoka Taiwan Bw Yang Ming alisema

    "Nimefika Jinli leo, nimefurahi, mambo mengi ya kale. Kuna vitu vingi vya sanaa za kazi za mikono vinauzwa, vilevile kuna vyakula vingi, vyakula vya Chengdu ni vitamu."

    Mtaa wa kale wa Jinli ulijengwa kwa kufuata hekalu la Wuhou, ambalo ni kivutio maarufu katika mji wa Chengdu, na ni mtaa maarufu wa shughuli za biashara, ambao ni kwa ajili ya watembea kwa miguu tu. Majengo ya huko yalijengwa kwa kufuata mtindo wa majengo yaliyokuwepo mwishoni mwa enzi ya Qing, majengo hayo yalijengwa kwa kufuata utaratibu mzuri, mtaa huu unasifiwa kama ni mchoro maarufu wa sanaa wa mandhari unaoitwa "mchoro wa Qingmingshanghe". Ofisa wa kituo cha huduma ya utalii cha Jinli dada Gong Xuan alisema,

    "Umaalumu wa mtaa huu wa Jinli ni mtaa wa utamaduni wa jadi, hasa unaonesha utamaduni wa jadi wa sehemu ya magharibi ya mkoa wa Sichuan, na kuwaonesha watalii waliotoka sehemu mbalimbali za dunia hali ya maisha, tabia na utamaduni wa wenyeji wa hapa. Kitu kingine ni kwamba tumeuunganisha na utamaduni wa kipindi cha historia cha "madola matatu". Hivyo tunasema kuna umaalumu wa aina mbili, kwanza ni umaalumu wa kihistoria yaani msingi wa historia ya "madola matatu", pili ni umaalumu wa utamaduni wa jadi, yaani umaalumu wa jadi wa sehemu ya hapa."

    Mji wa Chengdu unajulikana sana kwa vyakula vyake vitamu, baada ya kufika Chengdu watu wanavutiwa sana na vyakula mbalimbali vyepesi vya Sichuan. Kwenye mtaa mdogo wa Jinli watu wanaweza kupata kila aina ya chakula cha Sichuan, ikiwa ni pamoja na "nyama ya ng'ombe ya Zheng Fei", jemadari maarufu katika historia; keki ya "zhengzheng" inayotengenezwa kwa unga wa mahindi na yenye sukari; "Lai Tangyuan", donge lililotengenezwa kwa unga wa mchele unaonata na wenye chakula kingine katikati; "Zhong shuijiao", aina ya chakula kama sambusa zinazochemshwa katika maji; na "Long chaoshou", ambacho ni chakula kinachofanana na sambusa ndogo zinazochemshwa katika maji. Watu wanaweza kula huku wakitembea mtaani humo. Bi Gong alielezea vyakula maalumu vya huko kwa furaha, akisema:

    "Kilicho maalumu zaidi kati ya hivyo ni kile kinachoitwa "sandapao", ambacho utengenezaji wake ni tofauti sana. Hata kabla ya sisi kufika kwenye mkahawa ule, tulisikia sauti kubwa tatu, jina la "sandapo", ambalo maana yake ni mzinga kupigwa mara tatu, lilitokana na sauti hizo, chakula hiki ni kitamu sana."

    Mbali na mkahawa wa chai na jukwaa la maonesho ya michezo ya sanaa ya jadi, sehemu ya Jinli pia ina mikahawa kwa ajili ya kahawa. Baa zilizopo kwenye mtaa wa Jinli ni tofauti na za sehemu nyingine, ingawa ni za kisasa, lakini vilevile ni za mtindo wa kale wa Jinli, na zinachukuana vizuri na mandhari ya mtaa huo wenye mtindo wa kale.

    Kuna kiwanja kwenye sehemu ya kati ya mtaa wa Jinli, ambapo kuna jukwaa moja lenye mtindo wa kale. Michezo ya opera ya Sichuan inaoneshwa kwenye jukwaa hilo kila baada ya muda maalumu. Ikilinganishwa na michezo ya opera ya jadi ya Sichuan, watalii wanapenda zaidi kuangalia mchezo wa vivuli, mchezo wa vivuli ni sanaa ya jadi ya China, ambayo ilikuweko miaka zaidi ya elfu moja iliyopita. Vivuli vya rangi rangi vinatokana na wahusika waliotengenezwa kwa ngozi ya Punda na kuchezeshwa mbele ya taa, vinawaonesha watu hadithi za historia. Maonesho ya mchezo wa vivuli unavutia watalii wengi kila siku, hususan baadhi ya watalii kutoka nchi za nje. Watalii wawili kutoka Australia Bi Catherine Jones na Bi Roy Jackson walisema,

    "Sisi tunatoka Australia, tulifika kwenye mtaa huu dakika kumi zilizopita, lakini tunapenda sana hali ya hapa. Tunavutiwa sana na taa nyingi kubwa za rangi nyekundu za jadi za China zilizoko kwenye mtaa huo, tunafurahi sana, hususan tunapenda maonesho ya mchezo wa vivuli, kweli yanapendeza sana."

    Baada ya kuona maonesho ya mchezo wa vivuli yanawavutia sana watu, mchezaji mkubwa anayefanya maonesho ya mchezo wa vivuli kwenye mtaa wa Jinli Bw Zhou Yinong, alifurahi sana na kusema,

    "Nina marafiki wengi hapa nchini na katika nchi za nje. Televisheni ya Italia ilipiga picha za video, mimi ninawafundisha namna ya kutengeneza wahusika wa mchezo kwa ngozi, na namna ya kucheza mchezo wa vivuli. Walionesha video hiyo na kufundisha watu wa nchi yao, wanaweza kufahamu kidogo utamaduni wa China, lengo hasa ni kuwafahamisha watu wa nchi za nje utamaduni wa China."

    Wakati sikukuu ya Spring ilipokuwa inawadia, tamasha kubwa Chengdu, ambalo linafanyika kila mwaka, lilitoa fursa kubwa ya kuonesha umaalumu na utamaduni wa jadi wa sehemu ya Jinli. Tamasha la Chengdu la mwaka huu lililofanyika kuanzia tarehe 11 Februari hadi tarehe 3 Machi katika jumba la makumbusho ya hekalu la Wuhou mjini Chengdu, Jinli ilikuwa moja ya sehemu muhimu za maonesho. Mwelezaji wa sehemu ya Jinli Bibi Gong Xuan alisema,

    "Vitu vya sanaa za kazi za mikono,vibanda vidogo vya kuuzia vitu viko hasa katika sehemu ya maonesho ya Jinli. Kwa hiyo watu wanaweza kuona vitu vingi vya kuvutia katika sehemu ya Jinli, baadhi ya vitu vya sanaa vya kazi za mikono vinatengenezwa na mafundi hapa hapa wa kwenye maonesho, watalii wanaweza kuona namna ya vitu hivyo vinavyotengenezwa. Katika muda wa tamasha michezo mingi ya jadi ya wenyeji ilioneshwa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako