• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanzo mpya wa mtangazaji wa Uingereza nchini China

    (GMT+08:00) 2010-04-16 14:47:34

    Bibi Susan Osman

    Bibi Susan Osman alikuwa mtangazaji mwanamke maarufu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, hivi sasa anafanya kazi katika Radio China Kimataifa, na kuwa mtangazaji wa kipindi kipya cha habari Beijing Hour.

    Bibi Susan mwenye umri wa miaka zaidi ya 50 ana uzoefu wa kazi wa zaidi ya miaka 30. Aliwahi kuwa mwalimu wa Kiingereza, baadaye alifanya kazi katika Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, akawa mtangazaji mwanamke wa taarifa ya habari. Pia aliwahi kufanya kazi nchini Marekani na Japan, hivyo sio tu ana uzoefu mkubwa katika utangazaji wa habari, bali pia ana mtazamo wa kimataifa. Bibi Susan anapenda sana kazi yake, lakini kadiri umri wake unavyoongezeka, ndivyo ufuatiliaji wa wasikilizaji kwake ulivyokuwa ukipungua, na BBC haikutaka kuendelea kuwa naye. Bibi Susan alisema,

    "Ninapenda sana kazi yangu ya kutangaza habari na matukio. Lakini ukiwa na umri mkubwa, huna fursa nyingi kama vijana, na ni vigumu kwako kuthibitisha uwezo wako. Kwa kuwa nina kampuni yangu, na nilisaini mkataba wa kazi tu na BBC, hivyo wakati niliposhindwa kuwavutia wasikilizaji, walisimamisha mkataba nami."

    Bibi Susan alisema, nchini Uingereza watu wenye uzoefu mkubwa wanaweza kupata mshahara mkubwa, kwani uzoefu na umaarufu ni vitu vyenye thamani. Hivyo baada ya kufanya kazi kwa miaka 30 katika shirika la BBC, mshahara wa bibi Susan ulikuwa mkubwa. Kwa hiyo vyombo maarufu vya habari kama BBC huwa vinawajiri vijana kufanya kazi hiyo, lakini mishahara yao ni theluthi moja tu. Hivyo nchini Uingereza, ni vigumu kwa wanawake wenye umri mkubwa kupata maendeleo makubwa zaidi katika kazi zao, moja ni kwa sababu ya umri, nyingine ni jinsia. Bibi Susan alisema,

    "Katika miaka 30 iliyopita, hadhi ya wanawake katika vyombo vya habari iliboreshwa sana, lakini kwa wanawake hasa wanawake wenye umri mkubwa, bado kuna ubaguzi."

    Bibi Susan pia alikuwa hajui hatma ya shughuli zake nchini Uingereza, lakini ushauri wa mtoto wake ulimfunua macho. Alisema,

    "Mtoto wangu alisoma katika chuo kikuu, mwaka jana alikuwa mjini Shanghai, China. Alinishauri kuwa kwa nini usije China kujaribu?"

    Mwezi Oktoba mwaka jana, kwa kupitia habari zilizotangazwa kwenye tovuti, bibi Susan aliwasiliana na Radio China Kimataifa. Baadaye alituma maelezo yake kwa ufupi, picha na data nyingine za sauti, na kuanza mawasiliano rasmi na CRI. Alisema,

    "Kwenye barua pepe, tulizungumza kwa furaha. Baadaye waliniuliza nina umri wa miaka mingapi. Nikatuma barua pepe nikisema, nina uzoefu mkubwa, nchini Uingereza kama nitakuambia umri wangu, utaacha kuzungumza nami na kutowasiliana nami tena."

    Mwanzoni bibi Susan alidhani kuwa, vyombo vya habari vya China pia vinabagua wanawake wenye umri mkubwa, lakini maneno ya aliyemhoji yalimtoa wasiwasi. Alisema,

    "Aliyenihoji alisema nchini China tunawaheshimu watu wenye uzoefu mkubwa, pia tunawaheshimu watu wanaoweza kuwaletea uzoefu. Kwa hiyo tunaona kuwa umri sio tatizo."

    Kwenye mazungumzo hayo, aliyemhoji pia alizungumza na bibi Susan kuhusu utengenezaji wa vipindi, kazi ya bibi Susan na namna ya kuwasaidia vijana, ambayo pande hizo mbili ziliridhika. Kwa hiyo walisaini makubaliano ya kazi bila matatizo, na bibi Susan akaanza kufanya kazi nchini China. Radio China Kimataifa pia ilianzisha kipindi kipya kwa ajili yake kiitwacho Beijing Hour. Kwa bibi Susan anayependa sana kazi ya utangazaji wa habari, hii ilikuwa habari ya kumfurahisha. Alisema,

    "Ninapenda sana kipindi hiki, ingawa sipendi kuamka mapema alfajiri. Kila siku ninaamka saa nane na nusu usiku, na kujiandaa kwa ajili ya kazi saa kumi. Nataka kufanya vizuri zaidi kipindi, kwa kuwa kipindi hiki cha Beijing Hour kinamfanya mtu awe na hamu ya kazi. Nafurahi kutengeneza kipindi hiki, kwani ni uaminifu mkubwa kwangu, kwa hiyo nafuatilia zaidi kufanya vizuri kipindi hiki, ili kuwavutia wasikilizaji wengi zaidi, vilevile napenda kushirikiana na wenzangu."

    Bibi Susan alisema kufanya kazi nchini China ni fursa nzuri kwake, kwa sababu anaweza kujionea maendeleo na mabadiliko ya soko hili linalostawi siku hadi siku. Pia atajaribu kuchukua mtazamo wa Wachina kuangalia dunia, sura na mwelekeo wa China. Kwa hiyo bibi Susan alisema, atajifunza kutoka wenzake wa China katika pande hizo. Alisema,

    "Mtu yeyote hawezi kusita kujifunza. Hivyo bila kujali nina uzoefu mkubwa namna gani, nataka kujifunza kutoka kwa wenzangu. Hapa kuna watu wengi wenye busara, huenda hawana uzoefu mkubwa katika utangazaji wa habari wa moja kwa moja, lakini katika mambo mengine kuhusu njia ya maisha ya Wachina na utamaduni, wanajua mambo mengi zaidi kuliko mimi. Hii inaniwezesha nifahamu vizuri zaidi mtazamo wa Wachina kwa dunia, na kufanya vizuri zaidi kipindi chetu. Naona hii ni sehemu inayonifurahisha zaidi katika kazi yangu."

    Bibi Susan anapenda kusoma, kuandika na kufanya mazoezi, alisema kujilinda vizuri na kuwa na afya nzuri ni msingi wa kufanya kazi kwa bidii. Hivi sasa, bibi Susan pia anajifunza lugha ya Kichina baada ya kazi, ili kuifahamu vizuri zaidi China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako