• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wanaojitolea kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai wako tayari

    (GMT+08:00) 2010-04-19 20:30:24

    Watu wanaojitolea kutoa huduma wakati wa Maonesho ya Kiamtaifa y Shanghai sasa wako tayari. Tarehe 17 ambapo zilibaki tu siku 14 tu kabla ya kufunguliwa kwa maonesho hayo, watu hao walikula kiapo, hii inamaanisha kwamba kazi ya watu wanaojitolea kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai iko tayari. Watu hao walipokula kiapo walisema kwa sauti moja kuwa:

    "Napenda kuwa mtu wa kujitolea kwenye maonesho ya kimataifa. Nitaenzi moyo wa kupendana na kusaidiana, kutimiza matarajio ya pamoja ya kuyafanya Maonesha ya Kimataifa ya Shanghai yawe mazuri kuwa na mafanikio na yasiyosahaulika. Nitashirikiana na wenzangu kwa moyo mmoja, kufanya juhudi kadiri niwezavyo na kutoa mchango kwa hiari kwenye maonesho ya kimataifa. Dunia iko mbele yako, na sisi tuko pamoja na wewe."

    "Dunia iko mbele yako, na sisi tuko pamoja na wewe" huu ni mwito wa watu wanaojitolea kutoa huduma kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai. Kwenye hafla ya kula kiapo, watu hao wanaojitolea walitoa ahadi ya kutoa huduma bora kwa watalii kutoka nchini na nchi za nje.

    Bi. Tang Xiaoting ambaye anafanya kazi kwenye chuo cha elimu ya sheria katika Chuo Kikuu cha Mambo ya Bahari cha Shanghai, ni mmoja kati ya watu wanaojitolea kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai. Alikuwa mtu wa kujitolea wakati wa Michezo ya Olympiki ya Beijing ya Mwaka 2008, anasema anapenda kutumia uzoefu aliopata kwenye Michezo ya Olympiki pamoja na wenzake kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai. Anatumia Kiingereza kuwakaribisha wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani, akisema

    "Karibuni katika Maonesho ya Kimataifa ya Shanghai, hii ni mara ya kwanza kwa maonesho hayo kufanyika mjini Shanghai. Wakazi wote wa Shanghai wanakukaribisha. Sisi tuko tayari, na wewe je?"

    Bw. Ma Chunlei, ambaye ni ofisa anayeshughulikia kazi ya watu wanaojitolea kwenye maonesho ya kimataifa, amefahamisha kuhusu maandalizi ya kazi hiyo, akisema:

    "Kazi mbalimbali zinazohusu watu wanaojitolea kwenye maonesho ya kimataifa zote ziko tayari. Kazi ya kuwachagua watu wanaojitolea imekamilika, ambapo zaidi ya watu laki 6.1 waliomba nafasi ya kuwa watu wanaojitolea, na baada ya kufanya mahojiano zaidi ya elfu 30 ya uso kwa uso, tumechagua watu laki 1.72, wakiwa ni pamoja na watu elfu 72 watakaofanya kazi kwenye sehemu inayofanyika maonesho, na wengine laki 1 watakaotoa huduma kwenye vituo mbalimbali vya huduma kote mjini Shanghai. Kila mtu anayejitolea atapewa mafunzo ya aina tatu, ambayo ni mafunzo ya maadili ya kazi, mafunzo ya ujuzi na ufundi unaohitajika, na mafunzo ya mbinu za kufanya mawasiliano na watu kutoka nchi zenye utamaduni mbalimbali. Watu wanaojitolea watakaofanya kazi kuanzia mwishoni mwa mwezi Aprili ambacho ni kipindi cha uendeshaji wa majaribio wa maonesho ya kimataifa, na mwezi Mei ambapo maonesho hayo yatakapofunguliwa rasmi, wamepitia mafunzo yote wakiwa ndani ya sehemu ya kufanyia maonesho ya kimataifa."

    Kwa mujibu wa ofisa huyu, katika kipindi cha uendeshaji wa majaribio wa maonesho ya kimataifa kitakachoanzia tarehe 20, watu wanaojitolea elfu 15 wataanza kufanya kazi wakiwa kikundi cha kwanza.

    Ofisa wa mji wa Shanghai Bw. Yin Yicui amesema, watu wanaojitolea ni nguvu muhimu ya maonesho ya kimataifa. Watu hao watatumia tabasamu zao na maneno yao kuenzi moyo wa maonesho hayo, na kuhimiza mawasiliano na maingiliano kati ya utamaduni mbalimbali duniani kwa vitendo vyao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako