• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umaalumu wa hifadhi ya mazingira wa "Familia ya Hamburg"

    (GMT+08:00) 2010-04-27 15:52:59

    Hamburg ni mji mzuri wa bandari ulioko sehemu ya kaskazini ya Ujerumani, ambao wengi wanauita mji wa "Mlango wa Ujerumani wa kwenda nchi za nje". Mapema mwaka 1986, Hamburg na Shanghai zilianzisha uhusiano wa miji rafiki. Ili kufanikisha zaidi maonesho ya kimataifa ya Shanghai, mji wa Hamburg umejiandaa kwa juhudi na kuyaletea "zawadi kubwa" maonesho hayo inayoitwa "Familia ya Hamburg". Kutokana na kutumia teknolojia nyingi za hifadhi ya mazingira, jengo hilo ambalo linatumia kiwango kidogo cha nishati, linawavutia na kuwashangaza watu.

    "Familia ya Hamburg" iko kwenye sehemu ya miji yenye uzoefu mzuri kabisa kwenye maoensho ya kimataifa ya Shanghai, jengo hilo lililojengwa kwa matofali ya rangi nyekundu lina sehemu ya chini pamoja na ghorofa tatu. Umbo la jengo hilo ni kama kabati lenye droo, ambazo haziko kwenye mstari mmoja na baadhi yake zimevutwa nje kidogo. Lakini kwa nini walichagua umbo hilo kwa jumba la maoensho lao? Msaidizi wa mkurugenzi wa ofisi ya mawasiliano ya Hamburg iliyoko mjini Shanghai, anayeshughulikia uenezi na masoko Bi Wang Lai alisema,

    "Droo kadhaa za kabati zimevutwa nje, ambapo droo nyingine zimefungwa. Tulifanya marekebisho kuhusu usanifu wa jadi kwa mujibu wa hali ya hewa na mwangaza wa jua wa mji wa Shanghai. Hatimaye jengo hilo linafanana sana na droo za kabati."

    Kumbe sehemu kama droo zilizovutwa nje zinafanya kazi ya kuzuia mwangaza wa jua, na sehemu kama droo zilizofungwa ndani zinarahisisha mwangaza jua kuingia ndani. Umbo hilo la jengo licha ya kuweza kuwa la kipekee, pia linaonesha hali ya kisayansi ya usanifu. Madirisha yaliyoko kwenye upande unaopata mwanga wa jua ni madogo yakilinganishwa na madirisha yaliyoko kwenye upande wa kivulini, ambayo ni tofauti sana na nyumba za jadi za China, ambazo milango yake inaelekea upande wa kusini, na madirisha ya upande wa kusini ni makubwa. Lengo la usanifu huo ni kupunguza mwanga wa jua unaoingia ndani ya nyumba wakati wa majira ya joto.

    Sababu ya kuitwa "Familia ya Hamburg" ni kuwa jengo la hifadhi ya mazingira ni la kiwango cha juu, siyo tu ni kuwa umbo la jengo hilo lililobuniwa kwa akili, limetumia vizuri teknolojia za kubana matumizi ya nishati na hifadhi ya mazingira ya maumbile, bali pia ni "nyumba inayotendewa" ya kwanza nchini China. Mwakilishi wa mkuu wa ofisi ya mawasiliano ya Hamburg iliyoko mjini Shanghai Bw Lars Anke alieleza kuhusu maana ya "nyumba inayotendewa": Alisema:

    "'Nyumba inayotendewa' ni kigezo maalumu cha majengo nchini Ujerumani, majengo hayo yanatumia teknolojia ya kubana sana matumizi ya nishati. Mikazo inayotiliwa katika ujenzi wa majengo hayo ni, kwanza kutumia nishati mpya, kwa mfano nishati ya mwanga wa jua na joto za ardhini; Pili, kuta za nyumba hiyo zisiwe zinaingiza hewa, kwa kuwa ujoto wa ndani ya nyumba unatakiwa kudhibitiwa vizuri, kwa hiyo ni lazima iwe hivyo. Katika hali ya kawaida, viyoyozi havitakiwi kutumiwa ndani."

    Bw Lars Anke alisema, jengo la kutoingia hewa la "Familia ya Hamburg" lina uwezo wa kuzuia joto la nje kuingia ndani na kuzuia joto ya ndani isitoke nje, kwa kutumia rasilimali za kimaumbile ikiwa ni pamoja na joto la ardhini, "Familia ya Hamburg" wakati fulani hata inaweza kujitegemea kwa matumizi ya nishati. Wakati fulani kila mita za mraba ya jengo hilo inatumia umeme chini ya kilowati 50 kwa mwaka, matumizi yake ya umeme yanafikia robo ya matumizi ya umeme ya ofisi za kawaida.

    Umaalumu wa kubana matumizi ya nishati wa "Familia ya Hamburg" unaonekana pia katika uwezo wake, ambao licha ya kutumiwa kama ofisi, inaweza kutumiwa kama nyumba ya makazi ili kupunguza nishati zinazotumika katika usafiri. Watu wanaona raha na usalama kutokana na mtindo wa maisha wa kufanya kazi, kuishi, kupumzika na kushiriki katika shughuli za burudani katika jengo hilo moja. Hali halisi ni kuwa mbinu hiyo siyo uvumbuzi wa "Familia ya Hamburg", ujenzi wa "mji mpya wenye bandari" wa Hamburg, ambao ni mradi mkubwa kabisa wa ujenzi wa sehemu ya mji katika Ulaya uliofuata wazo hilo. Bw Lars Anke alisema, Hamburg inatarajia kuwaonesha watazamaji kuhusu uvumbuzi wa wazo hilo la maendeleo ya miji kwenye maoensho ya kimataifa ya Shanghai. Alisema:

    "Tunaona, 'mji mpya wenye bandari' ni mfano mzuri unaoambatana sana na kauli mbiu ya maoensho ya kimataifa ya 'miji bora, maisha bora'. Kwa hiyo, tunatarajia kuwaonesha watazamaji wazo la maendeleo ya miji ya kisasa kwenye sehemu hii, kufungamanisha mahali pa ofisi na mahali pa kuishi ili kutatua suala la mawasiliano katika maendeleo ya miji."

    Hivi sasa, ujenzi wa mradi wa "Familia ya Hamburg" unaendelezwa vizuri, na ulikamilika mwishoni mwa mwezi Machi na kuingia kipindi cha kupanga vitu vya maoensho. Kuhusu vitu vinavyooneshwa kwenye maonesho, kazi kubwa itakuwa ni kuweka mti mkubwa unaoitwa "Mti wa Matumaini". Mti huu mkubwa unaooneshwa kwa teknolojia ya 3D na kupitiliza kwenye jengo hilo zima kutoka chini hadi juu, licha ya kuwaonesha watazamaji mandhari nzuri ya mji wa Hamburg, utaonesha kwa mbinu ya multimedia matumaini ya wakazi wa Hamburg kuhusu maisha ya miji ya baadaye. Bw Lars Anke alisema:

    "Kitu muhimu kinachooneshwa ni mti wa matumaini, tunataka mti huu ukusanye matumaini ya watazamaji, na kuwaza pamoja nao namna ya kutimiza matumaini hayo. Matumaini hayo pengine yanahusiana na maisha na maendeleo ya miji ya kisasa. Tutatumia njia ya multimedia ili kuwawezesha watazamaji wafanye majadiliano na kufikiri namna ya kutimiza matumaini yao."

    Baada ya kumalizika kwa maoensho ya kimataifa ya Shanghai, jengo la "Familia ya Hamburg" litabaki kama jengo la kudumu mjini Shanghai, ili kuonesha mafanikio mapya ya maendeleo ya mji na ustaarabu wa Hamburg. Bw Lars Anke alisema, anatarajia kuwa "zawadi" hiyo maalumu ya maoensho ya kimataifa itaweza kuwa daraja la urafiki na maingiliano kati ya China na Ujerumani, na kati ya Shanghai na Hamburg. Alisema:

    "Hadi sasa, Hamburg na Shanghai zimekuwa na uhusiano wa kirafiki kwa miaka karibu 25, kitu hiki ni muhimu sana kwa Hamburg, tunazingatia sana uhusiano wa kirafiki na China pamoja na Shanghai. Kwa maoni yetu, China ni nchi nzuri kwa wenzi wa ushirikiano iwe katika uchumi, utamaduni au elimu. Katika maandalizi ya maoensho ya kimataifa ya Shanghai, tumefanya ushirikiano vizuri na kufurahia sana, tunataka kuizawadia Shanghai 'Familia ya Hamburg', ili kuimarisha maingiliano ya miji yetu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako