• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kasri la Potala la Tibet lahifadhiwa vizuri

    (GMT+08:00) 2010-04-29 16:15:26

    Mkoa wa Tibet uko katika uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet. Mkoani humo si kama tu kuna mandhari nzuri ya asili, bali pia kuna mabaki mengi ya utamaduni. Tangu mageuzi ya demokrasia yafanyike mwaka 1959 mkoani Tibet, serikali kuu ya China na serikali ya mkoa wa Tibet zimefanya juhudi kubwa za kuhifadhi mabaki ya kale ya utamaduni mkoani humo.

    Kasri la Potala liko juu ya Mlima Hongshan ulioko kaskazini magharibi mwa mji wa Lhasa. Kasri hilo lenye mtindo wa kitibet lilianza kujengwa katika karne ya 7, na kukarabatiwa katika karne ya 15. Katika kasri hilo, kuwa hazina nyingi zinazohifadhiwa.

    Waandishi wetu wa habari walikwenda kwenye kasri hilo kwa kufuata njia yenye umbo la "Z" inayoelekea juu ya Mlima Hongshan. Walipoinua vichwa waliona kuwa kasri la Potala kama liko juu ya mawingu. Baada ya kuingia katika kasri hilo, waandishi wetu wa habari waliona picha za ukutani zimewekwa vizurizi. Mfanyakazi wa kasri hilo Bw. Jor Dan alisema

    "Tumeweka vizuizi hivyo ili kuhifadhi picha kutani. Kwa kuwa kila siku watalii wengi wanakuja kutembelea, ambao wanapenda kugusa picha hizo kwa mkono, kama hakuna vizuizi, picha zitaharabiwa."

    Bw. Jor Dan ni fundi wa ukarabati, na kazi yake ni kuhifadhi mabaki hayo ya utamaduni yenye thamani kubwa. Katika miaka mingi iliyopita, Bw. Jor Dan pamoja na wafanyakazi wenzake wamefanya juhudi kubwa ili kuhifadhi majengo ya kasri la Potala, hata wameweka utaratibu kuhusu tambi za taa za mafuta katika vyumba mbalimbai kasrini. Bw. Jor Dan alisema,

    "Picha hizo zilichorwa miaka mingi iliyopita. Taa za mafuta zinaweza kuchoma picha na kuzifanya ziwe na rangi nyeusi. Kwa mfano katika chumba hicho, idadi ya tambi kwenye taa za mafuta haziruhusiwi kuzidi 17. Katika baadhi ya vyumba venye picha nyingi, taa za mafuta zinapigwa marufuku kuwashwa."

    Bw. Jor Dan aliwaambia waandishi wetu wa habari kuwa, hivi sasa wafanyakazi wa kasri la Potala wanarekodi maelezo ya picha yaliyochowa ukutani pamoja na picha hizo. Alisema,

    "Tumeanza kazi yetu kutoka ngazi ya kwanza, na katika ngazi hiyo, kuna picha 700 pamoja na maelezo 700. Lakini maelezo hayo si kamili, tunalazimika kuyatafuta katika vitabu vya kale."

    Kazi ya uhifadhi katika kasri ya Potala si kama tu inahusu picha ukutani, bali pia inahusu vitabu vya dini ya kibudha vyenye historia ndefu ambavyo idadi yake ni kubwa mno. Jumba la magharibi ni jumba kubwa zaidi katika majengo ya kasri la Potala. Ndani ya jumba hilo, kuna vitabu vingi vya kidini, na wafanyakazi wanasoma na kuviweka kwa utaratibu. Bw. Jor Dan alisema,

    "Kwa kuwa miaka mingi imepita tangu vitabu hivyo viandikwe, hata kamba za kufunga vitabu hivyo zimeoza. Wafanyakazi hao wanaangalia kama ubao wa kuhifadhi vitabu umepotea na kuwepo kwa wadudu au la. Halafu watavirekodi kimoja baada ya kingine. Kazi hii imetuchukua miaka zaidi ya 20, na bado haijakamilika."

    Jengo la kale zaidi katika kasri la Potala limekuwa na historia ya miaka zaidi ya 1,300. Ili kulifanya kasri hilo liendelee kung'aa katika uwanda wa juu wa Qinghai-Tibet, serikali kuu ya China haikusimamisha kazi ya ukarabati na uhifadhi. Mkurugenzi wa ofisi ya uendeshaji ya kasri hilo Bw. Champa Kelzang alisema,

    "Serikali kuu ilitenga yuan milioni 53 ili kukarabati kasri la Potala kwa mara ya kwanza kati ya mwaka 1989 na mwaka 1994, na ukarabati wa mara hii ulikuwa ni kwa ajili ya kuimarisha msingi wa majengo ya kasri hilo na kuondoa hali ya hatari. Baada ya miaka michache, ukarabati wa mara ya pili ulifanyika, na mara hii, serikali kuu ilitenga yuan milioni 170."

    Mwezi Agosti mwaka jana, mradi wa ukarabati wa majengo matatu ya kale mkoani Tibet yakiwemo kasri la Potala, hekalu la Norbu Lingka na hekalu la Sagya ulikamilika rasmi. Ukarabati huo ulioanzishwa mwezi wa Juni mwaka 2002 uligharama yuan milioni 380. Katika miaka hiyo saba, mafundi waliondoa hatari nyingi zilizojificha kutoka majengo hayo, na pia walivumbua teknolojia nyingi mpya, ambazo zitakuwa msingi nzuri kwa kazi ya kuhifadhi mabaki ya utamaduni mkoani Tibet.

    Kiongozi wa kikundi cha uongozi wa mradi wa uhifadhi na ukarabati wa mabaki matabu ya utamaduni mkoani Tibet Bw. Hao Peng, ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa mkoa unaojiendesha wa Tibet alisema,

    "Tumeweka kanuni ya kukarabati mabaki ya kale ya utamaduni. Kutokana na kanuni hiyo, tunajitahidi kudumisha sura ya zamani ya mabaki hayo. Wakati tulipokarabati majengo hayo, tumetumia teknolojia za kisasa pamoja na mbinu za jadi, ili kutoharibu thamani ya historia, sanaa na sayansi, na pia tumechukua hatua nyingi ili kukinga mabaki ya utamaduni kuibwa au kuharibiwa. Kazi hizo zimesifiwa na watu wa hali mbalimbali."

    Hivi sasa mradi mkubwa zaidi wa kukarabati mabaki ya utamaduni mkoani Tibet umefunguliwa. Serikali kuu imeamua kutenga yuan nyingine milioni 570, ili kukarabati majengo 22 ya kale mkoani humo. Pamoja na fedha zilizotenga katika miongo kadhaa iliyopita, serikali kuu ya China imetenga yuan bilioni 1.3 kwa ajili ya ukarabati wa mabaki ya kale ya utamaduni mkoani Tibet.

    Hadi sasa sehemu karibu 800 za mabaki ya kale ya utamaduni mkoani Tibet zimepata uhifadhi maalumu wa ngazi mbalimbali. kutokana na ufuatiliaji wa pamoja wa serikali kuu, serikali ya mkoa wa Tibet na wakazi wa Tibet, mabaki ya kale ya utamaduni yanayoeleza machozi na busara ya watibet yanang'aa tena, na kuwavutia watalii kutoka sehemu mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako