• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kauli mbiu ya Maonesho ya kimataifa ya Shanghai

    (GMT+08:00) 2010-04-28 17:30:08

    Maonesho ya kimataifa ya mwaka 2010 yatakayofanyika huko Shanghai, mji uliopo mashariki ya China yatafanyika kwa siku 184 kuanzia tarehe 1 Mei hadi tarehe 31 Oktoba,. inakadiriwa kuwa maonesho hayo yatavutia watembezi wapatao milioni 70 kote duniani, na kauli mbiu ya maonesho hayo ni "Miji bora zaidi, maisha bora zaidi". Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa China kuandaa maonesho ya kimataifa, na kauli mbiu hiyo ina umuhimu mkubwa katika hali halisi kwa hivi sasa.

    Toka mwaka 2007, zaidi ya nusu ya idadi ya jumla ya watu duniani wanaishi mijini. Kama nchi zilivyopita zilizoendelea, hivi sasa miji mikubwa na nchi zinazoendelea ambazo uchumi wake unaendelezwa kwa kasi pia zinapita kwenye mageuzi ya miji, lakini kasi ya mageuzi ya miji ya hivi sasa ni mara tatu kuliko kasi ya mageuzi ya miji ya nchi zilizoendelea hapo awali.

    China inashuhudia mageuzi ya miji, pia ni mfano mzuri wa mageuzi hayo. China ina idadi kubwa zaidi ya watu duniani, hivi sasa idadi ya watu nchini China imezidi bilioni 1.3. China pia ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani. Nchini China kuna miji zaidi ya 80 ambayo kila moja kati yao ina idadi ya watu zaidi ya milioni moja. Katika miaka 30 iliyopita, kila mwaka wakulima zaidi ya milioni 100 walihamia mijini. Wakati huo huo asilimia 65 ya watu bado wanaishi vijijini, baada ya miaka 20 huenda asilimia 65 ya watu wataishi mijini nchini China.

    Baada ya kuingia kwenye karne mpya, mchakato wa utandawazi wa miji duniani unaendelezwa kwa kasi, miji inaonesha umuhimu mkubwa katika kukusanyika kwa watu, kuinua ufanisi wa kazi, na kufanya uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia. Miji na maisha ya watu vinaungana kwa karibu zaidi na zaidi, miji inaleta mabadiliko kwa maisha ya watu, pia inaelekeza maisha ya watu. Wakati huo huo katika mchakato wa utandawazi wa miji, matatizo mengi pia yametokea katika maisha ya watu, kama vile matatizo ya mazingira, matibabu, elimu na ukosefu wa ajira, ambayo yanakwamisha maendeleo ya miji. Miji inahitaji kutumia nishati, huku ikitoa takataka nyingi, na miji ni chanzo cha uchafuzi unaotokana na magari na viwanda, uchafuzi huo ni sababu moja ya kuongezeka kwa hali ya joto duniani.

    Uchafuzi unaathiri vibaya nchi nyingi, na nchi zinazoendelea zinaathiriwa vibaya zaidi na uchafuzi huo, hasa nchi zile zenye matatizo ya kiuchumi. Hivi sasa watu wote duniani wanazingatia na kufanya utafiti kuhusu masuala hayo, ambayo yanafuatiliwa na dunia nzima.

    Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yameweka "miji bora, maisha bora" kuwa kauli mbiu yake, ili watu kutoka sehemu mbalimbali duniani waoneshe uzoefu na mifano yao mizuri katika mchakato wa utatuzi wa matatizo yanayotokea katika utandawazi wa miji. Maonesho hayo yanataka kuelekeza watu wengi zaidi wafuatilie masuala muhimu yanayohusiana na maendeleo ya miji, ili kuwasaidia watu kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kipindi cha mwanzo cha karne ya 21.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako