• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu wenye upofu wanaoshughulikia usingaji wanawaletea watu furaha kwa mikono yao

    (GMT+08:00) 2010-04-29 16:59:00

    Katika eneo la makazi la Chongwen mjini Beijing, kuna watu wenye upofu wanaoshughulikia kazi ya usingaji, ambao sio tu wanatumia mikono yao kuondoa maumivu ya wengine, bali pia wanawaletea watu furaha.

    Usingaji ni njia muhimu ya kulinda afya katika matibabu ya jadi ya China. Watu wengi huwa wanawaamini zaidi watu wenye upofu wanaoshughulikia kazi ya usingaji, kwani wanaona kuwa wasingaji hao sio tu wana ustadi mkubwa, bali pia wanafanya kazi kwa makini zaidi kuliko watu wa kawaida.

    Bw. Huang Xin mwenye upofu anafanya kazi katika sehemu ya kutoa huduma ya usingaji, alisema anaridhika na kazi yake hiyo. Alisema,

    "Kila mtu anafanya juhudi na kuwa na matumaini kwa kazi yake. Mimi naona hii ni nadharia ya pembetatu, kwa kuwa umbo la pembetatu ni wa imara zaidi, basi sehemu ya kutoa huduma ya usingaji, wafanyakazi na watu tunaohudumia pia tunaunda umbo la pembetatu, maslahi ya watu wote yanahakikishwa, na shughuli hizo zinaweza kuendelezwa kwa utulivu na kwa kasi."

    Mkuu wa sehemu ya kutoa huduma ya usingaji bibi Hou Yan pia ni mtu mwenye uwezo mdogo wa kuona, na amekuwa na uzoefu wa usingaji kwa miaka 25. Alisema hivi sasa maisha ya watu wenye upofu hayafungwi tena, kompyuta na simu za mkononi pia ni vifaa wanavyotumia kwa kufanya mawasiliano na wengine.

    Bibi Hou alisema sehemu hiyo ya kutoa huduma ya usingaji ni sehemu ya mfano mjini Beijing, wasingaji zaidi ya 20 wa hapa wengi walihitimu katika vyuo na vyuo vikuu ambao wote ni wenye upofu. Anaona kuwa watu wenye upofu wana uwezo maalum wa kushughulikia kazi ya usingaji. Alisema,

    "Watu wenye upofu huwa wanafanya kazi kwa makini zaidi, watu husema Mungu anapomfungia mlango mtu mmoja, anamfungulia dirisha. Ingawa macho yao yana matatizo, lakini hisia za kugusa na kusikiliza ni nzuri zaidi, na uwezo wao wa kufikiri hauna matatizo."

    Kuwasaidia watu wenye upofu kupata ajira ni kama kuwafungulia dirisha watu hao. Bibi Hou alisema kazi ya usingaji inawasaidia watu wengi wenye upofu kujiamini tena. Alisema,

    "Watu wenye upofu wanaofanya kazi ya usingaji wote ni hodari sana, kwani si rahisi kwao kufanya kazi. Kwa kupitia kufanya kazi wenyewe na kupata mapato watajiamini, na hadhi zao zitakuwa tofauti katika familia na jamii. Msingaji mmoja anatoka kijijini, kutokana na kufanya kazi, sio tu anaweza kujitegemea, bali pia anaweza kutoa fedha kwa ajili ya kuwasaidia wadogo zake kusoma na kuwatunza wazazi wake. Hata baadhi ya watu wenye upofu wanatoa fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wengine wenye matatizo ya kiuchumi kusoma vyuo vikuu."

    Hivi sasa, watu wenye upofu wanaoshughulikia kazi ya usingaji mjini Beijing wamezidi 1,500. Mwaka 2001 Shirikisho la walemavu la Beijing liliwashirikisha wataalam waanzishe kituo cha kuwafundisha watu wenye upofu usingaji mjini Beijing, ili kuwasaidia watu hao waoneshe thamani yao. Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Liu Hongbo alisema,

    "Kazi yetu ni kutoa huduma, kusimamia na kuelekeza shughuli za usingaji za watu wenye upofu, kuwapa watu wenye upofu wanaoanza kushughulikia kazi ya usingaji mafunzo ya ufundi, ikiwemo mitihani na uthibitishaji wa ufundi, halafu tunawajulisha katika sehemu mbalimbali za kutoa huduma za usingaji, ili kuwasaidia kupata ajira."

    Kwa mujibu wa sera husika za mji wa Beijing, watu wenye upofu wanapotaka kuanzisha shughuli za usingaji, serikali ya mji inawapa uungaji mkono wa kifedha, na kuwapatia sehemu na vifaa vya usingaji bure.

    Hivi sasa sera nyingi zaidi zenye unafuu za kuunga mkono shughuli za walemavu zimetolewa, jamii pia inafuatilia na kutoa misaada mingi zaidi kwa walemavu. Watu wa kawaida waliowasiliana na walemavu hutiwa moyo kutokana na jinsi walivyo. Msingaji mwenye upofu Bw. Huang Xin alisema, wateja wengi wanamjia, sio tu wanataka kuondoa maumivu ya mwili, bali pia wanataka kuzungumza naye. Bw. Huang Xin alisema,

    "Watu wa kawaida wanapokuja hapa wanaweza kufikiri kuwa, sisi ni walemavu, hakika tuna matatizo mengi zaidi maishani, kama tunaweza kushinda matatizo hayo, basi ni rahisi zaidi kwa watu wa kawaida kushinda matatizo. Rafiki yangu ambaye pia ni mtu mwenye upofu anayeshughulikia kazi ya usingaji aliniambia kuwa, mtu mmoja alikuwa akilalamika kila siku, siku moja rafiki yangu huyo alimwambia mtu yule kuwa si rahisi kuchukua glasi anapofumba macho yake, mwishoni kweli hakuweza kuchukua glasi, baadaye alilia na kusema hatalalamika katika siku za baadaye. "

    Bibi Hou alisema, walemavu wanaoweza kujitegemea huwa na moyo mkubwa na maono ya mbali, na wanawashukuru moyoni watu wanaowafuatilia na kuwasaidia. Bibi Hou alisema, mtu anapaswa kujua kuwashukuru wengine, sisi tunawashukuru wateja na wagonjwa, nao pia wanatushukuru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako