• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maisha ya Maria: mrembo wa dunia nchini China

    (GMT+08:00) 2010-05-06 14:40:30

    Bibi Maria anaimba kwenye maonesho ya michezo ya sanaa

    Bibi Maria, ambaye ni mrembo wa dunia kutoka Sierra Leone ameishi nchini China kwa miaka sita au saba hivi. Anaipenda China, na alisema China ni maskani yake ya pili. Alisema,

    "Nilikuja nchini China mwaka 2004, ambapo nilikwenda mjini Weifang kushiriki kwenye tamasha la kimataifa la tiara, baada ya mashindano, nilikwenda kumtembelea rafiki yangu mjini Shenzhen, lakini niliumwa wakati nilipokuwa katika garimoshi. Bibi mmoja kutoka Xi'an alipoona hali hiyo, alinisaidia na kunipelekea hospitalini, na alilipa pesa zote. Baadaye nilimwuliza bibi 'kwa nini unitendee vizuri namna hii?' alisema 'kwa sababu mimi pia nina mtoto, hivyo ninakuchuma kama kutunza mtoto wangu, napenda kukusaidia.' Nikasema 'asante sana, wewe ni mama yangu.' Baadaye niliporudi barani Afrika nilimwambia mama yangu kuwa, nimefika kwenye maskani yangu ya pili."

    Bibi Maria alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, alipomwambia mama yake kuwa ataondoka barani Afrika na kuishi nchini China, mama yake alishangaa sana, kwa sababu Maria alitembelea nchi nyingi, lakini hajawahi kusema kuwa anataka kuishi katika nchi fulani, hata hivyo uamuzi huo wa Maria uliungwa mkono na mama yake. Kama walivyo watu wengi wa Serra Leone, mama yake anayeishi mjini Freetown pia anaipenda sana China, na anapenda kutazama filamu za China, Gongfu ya China na opera ya China.

    Kabla ya kuja nchini China, bibi Maria alijua tu kuwa China ni nchi yenye historia ndefu, na makabila mengi madogo madogo ya China yanadumisha utamaduni wao wa asili hadi hivi leo. Kwa hiyo ana matumaini kuwa atakuwa na fursa ya kujiona mwenyewe utamaduni wa makabila mbalimbali ya China. Lakini jambo pekee linalomtia wasiwasi ni kuwa hajui tabia ya Wachina ni ya namna gani, na kama yeye anaweza kukaa nao vizuri. Baada ya kuja nchini China kwa mara ya kwanza mwaka 2004, bibi Maria alikuwa na kumbukumbu nyingi kuhusu uchangamfu wa Wachina.

    Baada ya kurudi nchini Serra Leone, bibi Maria alijenga uhusiano na Wachina wa huko. Anawasiliana nao mara kwa mara, na anafuatilia sana maendeleo ya China. Alisema,

    "China ilitusaidia kujenga jumba la michezo na kituo cha polisi. Nyumba ya familia yangu iko karibu na jumba la michezo, kwa hiyo ninawafahamu sana Wachina wa huko, lakini wakati ule nilikuwa sijui kuongea Kichina. Nilipokuja nchini China mwaka 2004 nilijifunza kidogo lugha ya Kichina, na baada ya kurudi barani Afrika nikaongea nao kwa Kichina, niliwaambia kuwa mimi ni Mchina kama nyinyi. Wakasema 'a, wewe ni Mchina?' nikasema 'ndiyo, mimi ni Mchina.' Kwa hiyo walifurahi sana. Wachina ni wachangamfu, hivyo nafurahi sana kuongea nao."

    Hivi sasa bibi Maria ameishi nchini China kwa muda mrefu, anaweza kuongea Kichina vizuri, na anapendwa na Wachina wengi. Anawasiliana na Wachina, siku hadi siku anajiunga na jamii ya China, na mustakabali wake unaungana na wa nchi hii.

    Tarehe 12 Mei mwaka 2008, tetemeko kubwa la ardhi lenye nguvu ya 8 kwa kipimo cha Richter lilitokea katika wilaya ya Wenchuan mkoani Sichuan China. Kama walivyo Wachina, bibi Maria pia alisikitika sana moyoni. Siku ya pili baada ya kutokea kwa tetemeko hilo, alipeleka mwenyewe kilo 10 za dawa na kwenda katika sehemu zilizokumbwa na maafa wilayani Wenchuan. Bibi Maria alisema,

    "Tarehe 13 Mei mke wa rais wa nchi yetu aliitembelea China, niliwaambia kuwa siwezi kushiriki kwenye sherehe ya kuwakaribisha, kwa sababu nilikuwa nakwenda mkoani Sichuan. Nina matumaini kuwa atanisamehe, kwa kuwa shughuli za pale zilikuwa muhimu pia. Nikafika pale siku ya pili baada ya kutokea kwa tetemeko hilo, watu wengi walinifahamu, lakini mimi sikuwafahamu. Nilipofika Wenchuan, barabara za huko zilikuwa zimefungwa. Wakati ule mtu mmoja aliuliza, nani anataka kuwapelekea dawa watu wa sehemu zilizokumbwa na maafa, nikasema mimi nataka kwenda, lakini walisema mimi ni mgeni, tena ni mwanamke, lakini nilisema moyoni mwangu mimi ni Mchina."

    Uzoefu wa kufanya uokoaji wakati wa maafa mkoani Sichuan ndio uliomfanya bibi Maria awe na nguvu, pia umemfanya aweze kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa urahisi katika maisha yake ya siku za usoni. Katika mashindano ya urembo ya dunia yaliyofanyika nchini Afrika Kusini mwaka 2009, bibi Maria alipata ushindi. Alisema,

    "Nilipanga kushiriki kwenye mashindano ya urembo duniani mwaka 2008, lakini kutokana na kutokea kwa tetemeko la ardhi mkoani Sichuan nchini China, nikasema sitakwenda kushiriki kwenye mashindano hayo. Niliwaambia kuwa, kutokana na China kukumbwa na tetemeko la ardhi, hivyo siwezi kushiriki kwenye mashindano hayo, kwani kama China ina matatizo, na mimi naona pia ni kama mwenyewe matatizo. Nitashiriki kwenye mashindano ya mara nyingine. Wakaniambia kuwa ni sawa, kama una nafasi unaweza kuja kushiriki kwenye mashindano mwaka 2009, kwa hiyo nilishiriki kwenye mashindano ya mwaka huo."

    Madhumuni ya bibi Maria kushiriki kwenye mashindano ya urembo duniani ni kuwataka watu wote duniani waweze kufahamu utamaduni wa kikabila wa China na ukarimu wa Wachina, kuchanganya utamaduni wa China na wa Afrika na kuuonesha kwenye jukwaa la dunia. Alisema,

    "Niliweza kupata taji, hii ni kwa sababu ya kuchanganya utamaduni wa China kwenye maonesho yangu, nina majaliwa na China, China ni maskani yangu ya pili."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako