• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kujionea mji wenye masikilizano katika jumba la maonesho la Ujerumani

    (GMT+08:00) 2010-05-10 19:18:54

    Mkuu wa jumba la maonesho la Ujerumani Bi Urte Fechter ni mwangalifu na ni mtu makini, wakati ujenzi wa jumba la Ujerumani ulipokaribia siku za mwisho, alifanya kazi kwa saa zaidi ya 12 kila siku. Ili kufahamu mawazo ya watazamaji wa China, alianza kujifunza lugha ya Kichina na utamaduni wa China tangu miaka miwili iliyopita, kwa hiyo jumba la maonesho la Ujerumani lilianza kipindi cha majaribio tarehe 20 mwezi Aprili kama ilivyopangwa.

    Kauli mbiu ya maonesho hayo ya Ujerumani ni "miji yenye masikilizano", kwa hiyo vitu vyake vyote vinaonesha uzuri wa mji mwafaka iwe kwa umbo la jumba la maonesho au vitu vinavyooneshwa ndani yake. Jumba hilo la maonesho lina eneo la mita za mraba 6,000, majengo yake manne makubwa yenye maumbo mbalimbali yanaendana vizuri, na kuonekana imara na kuafikiana. Bi Urte Fechter alisema,

    "Umbo la jumba la maonesho ya Ujerumani linavutia sana. Umbo lake ni la siku za baadaye, na linapendeza sana, ndani ya jumba hilo kuna vitu vingi vya kuvutia, ambavyo vinaonesha kauli mbiu ya jumba la maonesho la Ujerumani ya 'miji yenye masikilizano'."

    Jina la Kingereza la jumba hilo la maonesho ni Balancity, ambalo linawaambia watu kuwa endapo mji mmoja unaweza kufikia hali ya mapatano kati ya mji mpya na wa zamani, uvumbuzi na jadi, mji na maumbile, umma na mtu binafsi, kazi na mapumziko, basi kuishi katika mji huo ndiyo kuishi maisha ya mji wenye masikilizano.

    Jumba zima la maonesho la Ujerumani linafunikwa kwa nguo ya plastiki yenye mita za mraba elfu 12. Msanifu wa jengo hilo alisema, nguo hiyo ya plastiki inafanya kazi ya kuzuia mwangaza wa jua na joto, na itakapotolewa kwenye jengo hilo, itaweza kutumiwa kutengeneza mbao za kuzuia mwangaza wa jua, miavuli ya jua, au mifuko ya plastiki ya kuwekea vitu. Baada ya maonesho kumalizika, vifaa vya chuma cha pua tani zaidi ya 1,200 vilevile vitaweza kutumiwa tena.

    Watazamaji wanapoingia ndani ya jengo hilo, wanakuwa kama wameingia baharini, watazamaji wanaingia taratibu katika maisha ya mjini wakiwa kwenye ngazi ya umeme, huku wakisikia sauti ya maji ya baharini, na kuona video. Huko wanaweza kuona uvumbuzi mpya kabisa wa Ujerumani na kuona maisha mazuri yanayoletwa na uvumbuzi wa sayansi na teknolojia wa Ujerumani.

    Kivutio kikubwa kabisa katika jumba la maonesho la Ujerumani ni tufe kubwa la madini linaloitwa "chanzo cha nguvu", tufe hilo linaweza kutembea na kutoa mwangaza. Tufe hilo lenye uzito wa tani 1.2 na kipenyo cha mita 3, lilitengenezwa na idara kadhaa kikiwemo chuo kikuu cha Stuttgart, nje ya tufe hilo kuna taa za LED zinazota mwanga zipatazo laki 4, ndani yake kuna zana maalumu inayoweza kukuitikia sauti kubwa inayotoka nje. Endapo watazamaji mia kadhaa wakitoa sauti kubwa kwa pamoja, tufe hilo litatikisika kwa mfululizo, wakati huo huo video kuhusu mandhari ya sehemu mbalimbali za Ujerumani na dunia itaoneshwa ndani ya tufe hilo, na kuonesha uhamasa wa maisha ya miji. Bi Urte Fechter alisema, tufe hilo la madini lilitengenezwa nchini Ujerumani na kuletwa hapa China, na liko moja tu duniani. Alisema,

    "Chanzo cha nguvu" ni kivutio kikubwa zaidi cha jumba la maonesho la Ujerumani. Chanzo hicho ni tufe moja kubwa, na linaweza kuzunguka kwa kufuatana na sauti ya makofi na ushangiliaji wa watu. Tunajaribu kuwafikishia ujumbe wa "Tujitahidi pamoja" kutokana na usanifu huu, hebu tujitahidi pamoja kwa ajili ya kutimiza lengo la 'miji bora, maisha bora'."

    Tufe hilo la madini pia linafanana na "moyo wa mji na mapigo yake", ili liwe linatikisika au kuzunguka, inahitaji nguvu inayolisukuma na kudhibiti ulingano wake, na yote hayo yanatokana na ushiriki na mchango wa watu wote, hii vilevile ni tafsiri kuhusu kauli-mbiu ya "miji mwafaka" ya jumba la maonesho la Ujerumani.

    Watazamaji wapatao 600 wanaweza kuitikiana na tufe hilo kila mara, ambayo inachukua dakika 7 hivi, ambapo vijana wawili wa Ujerumani wanawaongoza watazamaji kushuhudia chanzo cha nguvu za mapatano katika eneo la mwangaza na sauti. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya magari ya Volkswagen ya sehemu ya China Dr. Winfried Vahland na watu walioambatana naye walishuhudia vivutio vya maonesho ya Ujerumani: Alisema,

    "Maonesho la jumba la Ujerumani yamenipa kumbukumbu nyingi. Kwanza, umbo la jumba hilo linanishangaza sana. Kabla ya hapo sikufahamu lolote kuhusu maonesho ya Ujerumani, ingawa nimewahi kuona baadhi ya picha zake, lakini sikufahamu ndani kukoje. Katika jumba hilo la maonesho, unaweza kuona namna wajerumani wanavyoishi nchini Ujerumani, maisha yao ya mijini, na namna wanavyofanya maisha yao kuwa mazuri zaidi. Mbali na hayo, katika maonesho hayo wanaonesha teknolojia ya kisasa na mambo kuhusu magari ya Ujerumani."

    Ili kuwavutia watazamaji, na kutoa huduma nzuri zaidi kwa ajili yao, wafanyakazi wote wa jumba la maonesho la Ujerumani wanafahamu lugha za aina mbili za Kichina na Kijerumani. Msemaji wa jumba la maonesho la Ujerumani Bi Marion Conrady alisema,

    "Wafanyakazi wote wa jumba la maonesho la Ujerumani wanaweza kuongea na watazamaji kwa lugha za Kichina na Kijerumani. Baadhi ya wachina kati yao wamewahi kuishi au kusoma nchini Ujerumani, wanafahamu sana China na Ujerumani pamoja na utamaduni wa nchi hizi mbili, licha ya hayo wanaweza kuongea lugha ya Kingereza."

    Katika jumba la maonesho la Ujerumani, kuna kitu kingine kinachowavutia sana watazamaji. Ndani ya jumba hilo kuna ukuta mmoja ulioko katika kando ya barabara, endapo watazamaji wasipoangalia kwa makini maelezo yake, wataukosoa. Watu fulani walichonga picha za baadhi ya wayahudi waliouawa katika vita kuu ya pili kwenye vipande vyembamba, na kuvitia kwenye sehemu ya juu ya barabara, wakitarajia watu wasisahau historia ile ya vita katili kadiri siku zinavyopita.

    Habari zinasema katika jumba la maonesho la Ujerumani, kuna waimbaji na kundi la wanamuziki wa Ujerumani, ambao wanafanya maonesho ya michezo ya sanaa katika eneo la maonesho ya kimataifa ya Shanghai. Katika ukumbi wa chakula ulioko ndani ya jumba la maonesho la Ujerumani, watazamaji pia wanaweza kupata chakula halisi cha kijerumani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako