• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhusiano kati ya Ufaransa na Afrika kuzingatia zaidi mambo halisi

    (GMT+08:00) 2010-05-31 15:31:14

    Mkutano wa 25 wa viongozi wa Ufaransa na Afrika unafanyika kuanzia tarehe 31 Mei hadi tarehe mosi Juni huko Nice, Ufaransa. Rais Nicolas Sarkozy amewaalika kwa mara ya kwanza wafanyabiashara wa Ufaransa na Afrika kuhudhuria kwenye mkutano huo ambao zamani ulihudhuriwa na viongozi wa serikali na wajumbe wa mashirika ya kimataifa tu, na ajenda za mkutano huo zimeongezwa kuwa tatu kutoka moja.

    Habari kutoka wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa zinasema, kwa ujumla nchi 52 za Afrika zimealikwa, inakadiriwa kuwa viongozi zaidi ya 40 wa Afrika na wajumbe wa Umoja wa Ulaya, Jumuiya ya nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, kamati ya Umoja wa Afrika na Benki ya Dunia watahudhuria mkutano huo. Kutokana na mwaliko wa rais Sarkozy, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon pia anahudhuria mkutano huo.

    Mkutano wa kwanza wa viongozi wa Ufaransa na Afrika ulifanyika mwaka 1973 kutokana na pendekezo la Ufaransa. Hii ni mara ya kwanza kwa rais Sarkozy kuendesha mkutano huo tangu achaguliwe kuwa rais wa Ufaransa. Rais Sarkozy alisema mara kwa mara kuwa Ufaransa haina nia ya ya kuwa polisi barani Afrika, na inapenda kuanzisha uhusiano wa kiwenzi wa aina mpya na nchi za Afrika. Amefanya mageuzi mawili kuhusu mkutano huo.

    Kwanza, mkutano huo unawashirikisha wafanyabiashara wa Ufaransa na Afrika kwa mara ya kwanza. Wajumbe kutoka makampuni 80 ya Ufaransa na makampuni 150 ya Afrika wamealikwa. Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imesema jambo hilo limeonesha kuwa uhusiano kati ya Ufaransa na Afrika hauhusu mawasiliano ya kiserikali tu, bali pia unahusu mambo ya uchumi na utamaduni.

    Makongamano matano kuhusu mambo ya uchumi ambayo yatawashirikisha mawaziri wa uchumi wa nchi mbalimbali yatafanyika wakati wa mkutano huo, ili kujadili masuala ya kuyapa makampuni madogo na ya kati urahisi wa kukusanya mtaji barani Afrika, kuimarisha utoaji mafunzo ya ufundi wa kazi kwa Waafrika, kutumia vizuri maliasili na kuendeleza nishati endelevu.

    Katibu wa mambo ya taifa wa Ufaransa Bw. Alan Joyant alipohojiwa hivi karibuni na mwaandishi wa habari wa shirika la habari la China Xinhua alisema Ufaransa inajaribu kuimarisha mawasiliano na wanaviwanda na vijana wa Afrika, na kuanzisha utaratibu mpya wa ushirikiano kati ya Ufaransa na Afrika kwa kupitia kazi ya kujipatia maendeleo ya uchumi.

    Licha ya hayo, mkutano wa mwaka huo una ajenda tatu, zikiwemo "hadhi ya Afrika kwenye kazi ya kushguhuliwa ya dunia", "kuimarisha kwa pamoja amani na usalama", na "hali ya hewa na maendeleo". Rais Sarkozy na viongozi wa nchi mbalimbali watafanya mkutano ili kujadili ajenda hizo.

    Mtaalamu wa kituo cha utafiti wa mambo ya kimataifa cha Chuo cha Siasa cha Paris Prof. Roland Marshall anaona kuwa, ingawa Afrika na Ufaransa zina uhusiano wa kihistoria, lakini vijana wa Afrika wana nia kubwa ya kujitawala na kujiamuliwa. Licha ya Ufaransa, nchi nyingi zinafuatilia na kushughulikia mambo ya Afrika, Ufaransa ikitaka kuhakikisha haki na maslahi yake barani Afrika, inatakiwa kuacha mtizamo wa jadi, na kufanya ushirikiano zaidi katika mambo halisi badala ya mambo ya kisiasa na kijeshi.

    Prof. Marshall alisema, "Afrika inabadilika siku hadi siku kwa kufuata mawimbi ya zama, sera za mambo ya nje za Ufaransa zinatakiwa kufuata mabadiliko hayo. Ufaransa inatakiwa kusikiliza sauti ya Afrika, na kufanya mazungumzo na Afrika kwa usawa." Watu wanafuatilia kama mkutano huo wa viongozi wa Ufaransa na Afrika utabadilisha sura ya Ufaransa ya polisi barani Afrika, na kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili ushughulikie mambo halisi na mambo mengi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako