• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutembelea maonesho ya jumba la Barcelona yenye uzoefu mzuri kabisa wa mji

    (GMT+08:00) 2010-05-31 16:13:19

    Mji wa Barcelona nchini Hispania uko kwenye sehemu ya kaskazini mashariki mwa peninsula ya Iberian, mji huu unasifiwa kama "lulu iliyoko kwenye sehemu ya Bahari ya Mediterranean" kutokana na kuwa na mandhari nzuri ya mwangaza wa jua, bahari safi na anga ya buluu, pamoja na hali nzuri ya hewa. Barcelona vilevile ni mji wa pwani unaounganisha ustaarabu wa kale na teknolojia za kisasa, wakati mji huo unapohifadhi vizuri mabaki ya utamaduni kwenye sehemu ya mji wa zamani, pia unaendeleza vizuri sehemu mpya ya mji. Katika maonesho ya kimataifa ya Shanghai, mji wa Barcelona inawafahamisha watazamaji mji huu wenye utamaduni wa aina nyingi kwa mambo mawili.

    Jumba la maonesho la Barcelona liko kwenye sehemu ya miji yenye uzoefu mzuri kabisa ya maonesho ya kimataifa ya Shanghai, ambalo ni mji pekee wa nchi ya nje inayoonesha kwa pamoja mambo mawili, yakiwa ni "Marekebisho ya sehemu ya mji wa kale" na "Ujenzi wa sehemu ya mji wenye uvumbuzi". Msanifu wa jumba la maonesho la Barcelona Bw Ignacio Anoveros alisema"Sehemu muhimu ya maonesho yetu inaitwa 'kisiwa', maonesho yetu yana visiwa hivyo vitano, ambavyo kauli-mbiu zake ni nafasi ya umma, barabara na miundo-mbiu, nyumba, mshikamano wa jamii na kufufuka kwa uchumi. Kwenye pande mbili za kila kisiwa kuna vioo vyenye kimo cha mita 7 ili kuwafanya watazamaji waone visiwa vikubwa. Hivyo, watazamaji wakiwa katika maonesho yetu, wanajiona kama wao wenyewe wako kwenye mitaa ya Barcelona."

    Katika visiwa hivyo vitano vyenye kauli-mbiu mbalimbali, msanifu alitumia skrini mbili kubwa akionesha hali nzuri zaidi ya kuungana kwa ustaarabu wa kale na wa sasa, skrini moja inahusu ukarabati wa sehemu ya mji wa kale, na nyingine inahusu ujenzi wa uvumbuzi wa mji mpya, watazamaji wanaweza kuona mji halisi wa kisasa duniani wenye mambo ya jadi na ya kisasa kutokana na mambo mawili tofauti yenye kauli-mbiu moja. Je, ni vipi walichagua mada mwafaka zaidi kati ya mambo chungu nzima yenye umaalumu wa miji kwa watazamaji? Bw Ignacio Anoveros alisema"Mada kuu ya usanifu ya Barcelona katika sehemu ya maonesho inayoitwa sehemu yenye uzoefu mzuri kabisa wa miji ni 'kioo'. Kioo ni moja ya alama ambazo watu wanaweza kuhisi matarajio mazuri zaidi kuhusu siku za baadaye kutokana na kutafakari kuhusu historia. Kwa hiyo uzuri wa aina nyingi za utamaduni wa mji huu unaonekana katika usanifu wa jumba la maonesho kwa kuangalia kutoka kwenye vioo. Barcelona ni mji wenye wakazi wa makabila mbalimbali na utamaduni wa aina mbalimbali. Tunatarajia kuwa vitu vingi vionekane kwenye vioo, ili kuonesha umaalumu wa Barcelona wenye utamaduni wa aina nyingi."

    Kuhusu alama ya mji wa Barcelona inayovutia zaidi, msanifu wa majengo Bw Antonio Gaudi na urithi wa dunia wa majengo aliyoyasanifu, yanastahili sifa hiyo. Kati yake 'Dragon wa Gaudi' iliyoundwa kwa mtindo wa mosaic na vigae vya kauri kwenye bustani ya Guell inavutia zaidi. Ili kufanya maonesho ya kimataifa ya Shanghai yavutie zaidi, serikali ya mji wa Barcelona iliipa China zawadi ya nakala ya 'Dragon ya Gaudi', ambayo ukubwa wake ni sawasawa kabisa na ile ya asili, na itabaki milele nchini China ikiwa ni zawadi kwa maonesho ya kimataifa ya Shanghai. Mkuu wa jumba la Barcelona Bw Ignacio Anoveros alisema, "Sababu ya sisi kuchagua 'Dragon ya Gaudi' ni kuwa hii ni alama ya majengo na mambo ya kisasa ya mji wa Barcelona. Vitabu vingi vya Kichina vimeiweka katika jalada lake la mbele, hii inaonesha kuwa alama hiyo inapendwa na watu wengi. Dragon ni sehemu muhimu ya utamaduni wa jadi wa China, vilevile ni moja ya alama 12 za mzunguko wa miaka ya kuzaliwa kwa watu, tunatarajia kuwa dragon wa Barcelona ataleta heri na baraka kwa watu wa China. Kwa hiyo tumemkabidhi meya wa Shanghai zawadi ya 'Dragon wa Gaudi', tunatarajia kuwa Dragon huyo ataweza kuleta bahati nzuri kwa Shanghai."

    Barcelona ni mji muhimu wa kimataifa, mpango wa ujenzi na mchakato wa maendeleo ya mji huo vinastahili kupongezwa na kuigwa na nchi nyingine. Licha ya kuhifadhi vizuri mabaki ya kihistoria na kiutamaduni, Barcelona inafanya ujenzi wa maendeleo endelevu na ujenzi wa mambo ya kisasa. Bw Ferran Ferrer alitufahamisha uzoefu wa maendeleo ya mji huu, akisema"Michezo ya 25 ya Olimpiki ya mwaka 1992 ilileta nafasi nzuri ya maendeleo kwa Barcelona. Wakati Barcelona ilipopewa nafasi ya kuandaa michezo ya Olimpiki miaka 6 kabla ya kufanyika kwa michezo ya Olimpiki ya Barcelona tulisema, tutatumia fursa hiyo kutekeleza mpango wa kubadilisha mtindo wa maendeleo ya mji. Tokea hapo mpango wa ujenzi wa mji ulifuata njia moja mpya. Katika ujenzi wa mji, hatukuharibu mji wa zamani, bali tulijenga sehemu mpya ya shughuli za biashara, tulitumia mbinu ya kuunganisha sehemu hizo mbili, na kuratibu mambo ya maeneo mbalimbali yakiwa ni pamoja na ya makazi, ofisi na maendeleo ya viwanda. Maendeleo ya ujenzi wa mji si kama tu yalidumisha umaalumu wa jadi wa mji, bali pia yaliunganisha ipasavyo uwezo wa mji wa kisasa, tena yalipata uzoefu kwa maendeleo ya ujenzi wa Barcelona katika siku za baadaye na kwa maendeleo ya ujenzi wa miji ya nchi nyingine."

    Katika sehemu ya uzoefu mzuri kabisa wa mji wa Barcelona, licha ya kuona nguvu kubwa za maendeleo, vilevile tunaona vizuri kauli-mbiu ya "miji bora, maisha bora". Vitu vingi vilivyoonekana kwenye vioo vinaonesha maisha yenye utamaduni wa aina nyingi pamoja na hali ya maendeleo ya sehemu mpya na ya zamani ya mji, watazamaji wanapokuwa kati ya vioo hivyo, wanaweza kuona historia na mustakabali wa mji. Mkuu wa jumba la maonesho la Barcelona Bw Ferran Ferrer anapenda sana kauli-mbiu ya maonesho ya kimataifa ya Shanghai, alisema, kauli-mbiu hiyo ya Miji bora, maisha bora ni muhimu sana kwa maendeleo ya binadamu: " Kauli-mbiu ya 'Miji bora, maisha bora' imeonesha kwa usahihi lengo la China la kuandaa maonesho ya kimataifa. Hivi sasa zaidi ya nusu ya idadi ya watu wa duniani wanaishi katika miji, hivyo namna ya kuishi maisha bora katika miji inastahili kuwa kitu muhimu kinachofuatiliwa na watu. Kauli-mbiu ya maonesho ya kimataifa ya Shanghai imesisitiza umuhimu wa miji katika maisha ya watu. Mbali na hayo, maonesho ya Barcelona vilevile yana kauli-mbiu yake: 'Barcelona, msingi wa miji'. Katika kipindi cha maonesho ya kimataifa cha miezi 6, mbali na maonesho ya sehemu mbili zenye uzoefu mzuri kabisa za mji, tutaifahamisha China kuhusu Barcelona, kuwaeleza watu na viwanda vya China kuhusu hali nzuri ya uchumi wa mji na mazingira bora ya maendeleo ya shughuli za biashara, ili kuvutia watalii wengi waje kutembelea Barcelona, kuhimiza viwanda vingi vya China vije kuwekeza mjini Barcelona, na kujenga msingi imara wa kuwepo ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako