• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya kimataifa ni zawadi kwa watoto

    (GMT+08:00) 2010-06-03 14:25:51

    mtoto mmoja wa China anafurahi sana

    Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yamejaa ubunifu na kuwapa watu taswira nyingi nzuri kuhusu dunia, hivyo yanafaa zaidi kutembelewa na watoto, kwani watoto ni watu wanapenda kutimiza ndoto, na ni matumaini ya siku za baadaye. Kwenye eneo la maonesho ya kimataifa, watoto wameona busara za watu kutoka sehemu mbalimbali duniani, huenda hawaelewi wanachoona, lakini wanafurahia sana.

    "Napenda maonesho ya kimataifa, karibuni mtembelee maonesho ya kimataifa ya Shanghai!"

    Unapokuwa kwenye maonesho ya kimataifa utasikia sauti za mshangao za watoto. Wanapotembelea kwenye eneo la maonesho ya kimataifa na kuona majumba ya maonesho yenye ubunifu tofauti na wageni kutoka sehemu mbalimbali duniani, wanafurahi sana.

    Majumba mengi ya maonesho pia yanazingatia mahitaji ya watoto ili waweze kupata furaha kubwa zaidi. Kwa mfano kwenye jumba la maonesho la China, picha nyingi zilizochorwa na watoto zinawafanya watoto waone ndoto za wenzao wa rika lao; na jumba la maonesho la Qatar pia limeandaa shughuli za uchoraji kwa ajili ya watoto, ambapo watoto wanaweza kuchora picha zao kuhusu jumba la Qatar.

    Jumba la maonesho la Russia limepambwa kama ngome zinazosimuliwa kwenye hadithi, ambalo linapendwa sana na watoto. Mifano kwenye ghorofa ya kwanza ya jumba hilo inaonesha miji iliyopo kwa taswira za watoto wa Russia. Baadhi ya mifano imetengenezwa kwenye msingi wa michoro ya watoto, ambapo baadhi ya miji imejengwa juu ya gamba la kobe, na inatembelea dunia nzima wakati kobe anapotembea pole pole. Naibu ofisa wa habari wa Russia bibi Alina Suslova alisema,

    "Kwanza utaona mifano iliyotengenezwa kwa kufuata michoro ya watoto wa Russia, ambayo ni mawazo yao kuhusu siku za baadaye. Walichora jinsi wanavyofikiri miji itakavyokuwa katika siku za mbele, na tulitengeneza mifano kwa msingi wa michoro yao. Watoto wana mawazo mengi sana ya ajabu kuhusu siku za baadaye, na wazo la jumba letu ni kuwafanya watoto waishi katika miji yenye furaha. Tunaona kuwa tunapaswa kufanya mambo mengi zaidi kwa ajili ya watoto, kwani wao ni matumaini ya siku za baadaye."

    jumba la maonesho la Russia

    Ukifika kwenye ghorofa ya pili ya jumba la maonesho la Russia, maua makubwa yanayozunguka kwenye nguzo yanawashangaza watu. Matunda makubwa ya stroberi, litchi na anga vinawafanya watu wajione kama wameingia katika ngome zinazosimuliwa kwenye hadithi za zamani. Kwenye skrini kubwa, watoto wa Russia wanatumia lugha ya Kichina kujulisha uvumbuzi mpya wa wanasayansi wa Russia. Mvulana wa China mwenye umri wa miaka 7 Shen Jialong alisema,

    "Jumba hilo linapendeza sana, vitu vyote vinakuzwa, maua yamekuwa makubwa kuliko tikitimaji. Hapa ni kama dunia inayoelezewa kwenye katuni na vitabu. Nalipenda sana."

    Kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai, shughuli za kujifanya kama walivyo watu wazima zinapendwa na watoto na wazazi wao, ambapo watoto wanaweza kujifanya kama waandishi wa habari, wanamitindo na wahasibu ili kujionea maisha ya kazi baada ya kukua. Meneja mkuu wa idara ya mpango wa shughuli hizo Bibi Jin Shuyu alisema,

    "Tunataka kupitia shughuli hizo kufanya hisia za watoto ziguswe na jamii halisi na mambo watakayokutana nayo watakapokua watu wazima. Aidha tunachagua kazi mbalimbali zilizopo hivi sasa, ili kuwafanya watoto wajionee dunia wanayoikabili wazazi wao kila siku."

    Kama inavyoimbwa kwenye wimbo huo kuwa maonesho ya kimataifa ni tamasha kubwa linalotarajiwa na watoto, yanatupa matumaini kuwa maisha yataifanya dunia izidi kuwa nzuri.

    Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na maonesho ya kimataifa ya awamu iliyopita, watoto wenye umri wa miaka chini ya 15 walichukua asilimia 60 ya watalii wote. Na kwenye eneo la maonesho ya kimataifa ya Shanghai, mwandishi wetu wa habari aliwakuta watoto wengi, ambao wanashikana mkono na kutembelea maonesho hayo yanayokusanya busara za watu wa sehemu mbalimbali duniani.

    Mwalimu Yuan Xudong wa shule ya msingi ya Sitangxincun ya Baoshan mjini Shanghai alisema,

    "Kwa kuwa katika shule yetu kuna watoto wengi wa wafanyakazi vibarua, na wazazi wao wengi labda hawana nafasi ya kuja kutembelea maonesho ya kimataifa pamoja nao, hivyo tunawaleta watoto wote kutembelea maonesho hayo, ili wajionee busara za watu wa sehemu mbalimbali duniani na kuongeza ujuzi wao."

    Tarehe 9 Mei kundi la maonesho kutoka nchi za Ulaya lilifika na kufanya maonesho kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai, watoto kutoka nchi mbalimbali waliona kwa pamoja utamaduni tofauti wa sehemu mbalimbali duniani. Msichana mwenye umri wa miaka 11 kutoka Marekani Colleen Mccan alisema,

    "Nafurahi sana, kwani hapa naweza kuona utamaduni wa kipekee wa nchi tofauti."

    Msanifu mkuu wa eneo la maonesho ya kimataifa ya Shanghai Bw. Wu Zhiqiang alisema, maonesho ya kimataifa ni zawadi kwa watoto. Alisema,

    "Tumeona kuwa kwenye kishikio cha funguo cha msanifu wa jumba la maonesho la Osaka la Japan bado kuna kumbukumbu ya maonesho ya kimataifa ya Osaka ya mwaka 1970. Wakati ule alipotembelea maonesho hayo alikuwa na umri wa miaka 10. Baada ya miaka 40, amekuwa msanifu wa maonesho ya kimataifa ya Shanghai, matembezi kwenye maonesho ya kimataifa ya awamu ile yalimpatia mengi katika maisha yake. Hivyo naamini kuwa baada ya miaka 30 au 40, pia watajitokeza wasanifu kati ya watoto wanaokuja kutembelea maonesho ya kimataifa ya Shanghai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako