• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuona maajabu ya maumbile kwenye delta ya mto Manjano

    (GMT+08:00) 2010-06-07 16:23:45

    Mto Manjano ni mto mama wa China, kwenye sehemu ambayo maji ya mto huu yanaingia baharini, kuna delta moja kubwa yenye rasilimali nyingi na mazingira ya kipekee ya kimaumbile. Kwenye ardhi ya sehemu hiyo kuna mji mmoja mpya wa Dongying, ambao ni kituo cha pili kwa ukubwa cha usafishaji wa mafuta ya petroli nchini China, mji huu wenye vivutio vingi vya kimaumbile, umethibitishwa kuwa hifadhi ya maumbile ya ngazi ya taifa kutokana na mfumo wa kimaumbile wa ardhi oevu.

    Mji wa Dongying uko kwenye sehemu ya delta ya mto Manjano, kaskazini mwa mkoa wa Shandong, ambapo maji ya mto Manjano yanapita na kuingia kwenye bahari ya Bo. Mandhari ya maumbile ya sehemu hii ni nzuri ajabu, naibu mkurugenzi wa ofisi ya ujenzi ya delta ya mto Manjano ya mji wa Dongying Bw Xue Rongjian alisema, "Maji ya mto Manjano yanaingia baharini katika sehemu moja tu, hali hii inawavutia watu sana. Mto Manjano ni maarufu sana katika dunia, huu ni mto mama kwetu na sote tunaupenda, kwenye sehemu ambayo maji ya mto yanaingia baharini, tunaweza kuona rangi mbili za manjano na buluu kwenye maji ya mto na bahari katika sehemu moja."

    Hali maalumu ya kimaumbile ya delta inapendeza sana, delta hiyo ilijitokeza kutokana na kulundikana kwa udongo na mchanga unaokokotwa na maji ya mto. Kwenye ardhi ya kando mbili za mto Manjano, kuna mfumo mpya wa kimaumbile wa ardhi oevu, ambao ni mkubwa na ulio kamili kabisa duniani, pamoja na malisho makubwa ya asili na vichaka, sehemu hii ni hifadhi ya kimaumbile ya ngazi ya taifa. Mkurugenzi wa ofisi ya uenezi ya mji wa Dongying Bw Ren Zengqing alisema, "Eneo la hifadhi hiyo ni kiasi cha hekta laki 1.53, ambalo limehifadhiwa vizuri sana. Katika majira ya mpukutiko kuna ndege wengi wazuri sana, na kufanya mandhari ya wakati huo iwe ya kipekee. Ardhi ya sehemu hii mpya ni ya kipekee nchini China, na ardhi ya Dongying inapanuka kwa mfululizo. Hii ni zawadi tuliyopewa na mto Manjano."

    Katika hifadhi hii kuna wanyama na ndege wa zaidi ya aina 1,500, kati ya hao ndege wanakaribia wa aina 300, ikiwa ni pamoja na aina 10 za ndege adimu wakiwemo korongo wenye utosi mwekundu, na korongo weupe wa mashariki. Chen Junlin, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Anhui anayefanya utafiti wa elimu ya mazingira ya kimaumbile ya korongo mweupe wa mashariki, toka mwanzoni mwa mwaka huu amekuwa akifanya utafati kwenye hifadhi ya maumbile kuhusu ndege wanaokabiliwa na hatari ya kutoweka, alisema, "Korongo mweupe wa mashariki ni ndege anayekabiliwa na hatari ya kutoweka, hivi sasa analindwa kitaifa kwa ngazi ya kwanza. Ndege huyu ni mkubwa na ana\eishi kwenye sehemu yenye maji, anachagua sana mahali pa kuishi. Hivi sasa idadi ya ndege hao ni ndogo sana, ambayo haijafikia 3,000 katika dunia nzima, hivyo ndege hao ni adimu sana. Delta ya mto Manjano imekuwa mahali pa kupumzika wakati wanapohamia sehemu ya kusini au sehemu ya kaskazini kwa kufuata mabadiliko ya hali ya hewa, zamani ndege hao hawakuzaliana huko, lakini hivi sasa ndege hao wamechagua kuzaliana huko."

    Mbali na kuweko kwa makundi makubwa ya ndege adimu kwenye sehemu hiyo, mimea inayoota kwenye ardhi oevu ya huko vilevile ni kivutio kikubwa. Sehemu hii ina mimea zaidi ya aina 300 yakiwemo matete, bitter flea bane na maharagwe pori, ambayo 55% ya ardhi inafunikwa na mimea. Hususan katika majira ya mpukutiko, mimea ya bitter flea bane inayoota kwenye eneo kubwa inabadilika kuwa na rangi nyekundu, kama ikitazamwa kutoka mbali, inaonekana kama ni zulia kubwa jekundu lililotandikwa hadi mwisho wa upeo wa macho.

    Mbali na mazingira mazuri ya asili, Dongying pia ni sehemu, ambayo wakazi wanazingatia sana mapishi ya chakula, sehemu hii ina aina mbalimbali za chakula zenye umaalumu wa huko, na watalii wanavutiwa sana. Kwa kuwa Dongying iko kwenye delta, kwa hiyo sehemu hii ina mazao mengi ya majini. Mkurugenzi wa ofisi ya uenezi ya mji wa Dongying alisema, kaa wa sehemu hiyo ni chakula kitamu sana cha Dongying, kaa wa sehemu hiyo wanahitajiwa sana katika soko la nchini, na pia wanapendwa sana katika masoko ya nchi za nje. Alisema"Kaa wa kwetu hapa, wanaishi katika mazingira ya asili, sisi hatuwalishi, wanatafuta chakula wao wenyewe, kwa hiyo nyama yao ni tamu sana."

    Habari zinasema, kwenye sehemu mbalimbali karibu na bandari ya Dongying, kuna mikahawa mingi inayouza chakula cha baharini, bei ya chakula katika mikahawa hiyo ni ya chini, kwa hiyo ina wateja wengi. Meneja wa mkahawa wa chakula cha baharini ulioko kwenye kando ya kaskazini ya bandari ya Hongguang, Dongying, Bw Zhang alisema, "Mkahawa wetu hasa unauza chakula cha baharini, ambacho kinapatikana hapa kwetu. Kaa wa aina ya Suozi ni chakula maalumu cha kwetu. Supu ya samaki aina ya Kailingsuo vilevile ni supu maalumu ya kwetu hapa. Samaki wa Kailingsuo ni wazuri sana, wanapatikana tu kwenye sehemu hii, ambayo maji ya mto yanaingia baharini na kwenye ghuba ya bahari ya Bo, bahari nyingine hazina samaki wa aina hii. Licha ya kuuza chakula cha baharini, vilevile tunauza vitoweo vingine vya mazao maalumu ya kwetu hapa, wanyama pori na mboga za porini. Vitoweo vya chakula cha baharini vya hapa ni vitamu na vinauzwa kwa bei rahisi."

    Meneja Zhang alisema, mazao ya baharini yanapatikana kwa wingi kutoka wakati huu hadi mwezi Novemba, joto likiingia watalii wengi wanafika huko kwa ajili ya kuonja chakula cha baharini na kuangalia mandhari nzuri ya maumbile. Mvuvi mmoja wa huko alisema, supu ya samaki wa huko inajulikana sana, mwenye mkahawa alisema, "Supu ya samaki ni chakula maalumu cha hapa, kuna supu ya samaki wa aina nyingi, supu ya samaki wa hapa ni ya rangi nyeupe, ni tamu na inaburudisha sana. Tunawakaribisha mje kuonja supu ya samaki wa hapa Dongying.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako