• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Rotterdam waendelezwa pamoja na miradi ya maji

    (GMT+08:00) 2010-06-18 11:16:55

    Uholanzi inayojulikana kuwa nchi yenye ardhi iliyo ya chini, robo ya ardhi yake iko chini ya usawa wa bahari, ikiwa ni pamoja na mji wa Rotterdam, ambao bandari yake inachukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa duniani. Mji huu ni kama askari wa doria kuhusu maafa ya maji. Hali ya kuwa na bandari kubwa imeuletea mji wa Rotterdam fursa nyingi za kibiashara na kuhimiza maendeleo ya mji; lakini maji pia ni tishio kubwa linaloukabili mji huo. Kutokana na kuathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani, hali ya maji kuwa mengi, na maji ya baharini kuingia katika mto wa mji imezidisha tishio hilo, kwa hiyo mji wa Rotterdam hauna budi kubuni sera mpya na kurekebisha mara kwa mara mkakati wa kudhibiti hali hiyo.

    Mvutano huu umeleta fursa kubwa kwa mji wa Rotterdam, na kuufanya mji huo uwe na mradi wa maji unaoongoza duniani pamoja na mpango wa maendeleo ya mji, katika maonesho ya kimataifa ya Shanghai, Rotterdam ni mfano wenye sifa nyingi kwenye sehemu ya miji yenye uzoefu mzuri kabisa.

    Mara tu baada ya kuingia kwenye jumba la maonesho la Uholanzi, watu wanaweza kugundua mara moja tofauti ya maonesho hayo na maonesho ya majumba mengine, karibu robo ya eneo la maonesho yake ni ya kuinama. Huu ndiyo uwanja wa maji, silaha nzuri ya Rotterdam ya kukabiliana na maafa ya mafuriko.

    Uwanja wa maji una madimbwi kadhaa yenye maumbo na ukubwa tofauti, madimbwi hayo yameunganishwa kwa mfereji. Katika nyakati za kawaida, sehemu ya hapo ni uwanja wenye shughuli za burudani, pindi inaponyesha mvua kubwa, maji yanatiririka kwenye sehemu iliyoinama, uwanja wa maji unabadilika kuwa mfumo wa kuzuia mafuriko, kwa kuwa maji ya mvua yanatiririka kuelekea kwenye uwanja wa maji, ambayo ni sehemu iliyoinama zaidi, hivyo kwenye mitaa mbalimbali ya mji huo hakuna maji mengi. Maji ya mvua yaliyoko kwenye uwanja wa maji, yanaweza kutiririka kwenye madimbwi mbalimbali, tena yanaweza kuhamishiwa sehemu nyingine na kutumiwa kama maji baridi.

    Mtaalamu wa hifadhi ya mazingira ya hali ya hewa ya Uholanzi Bw Arnaud Moluna alisema, mji wa Rotterdam hauna budi kukabiliana na changamoto nne za maji ya bahari, maji ya mto, maji ya mvua na maji ya ardhini, mifereji na mito iliyopo hivi sasa imeshindwa kutatua tatizo la ongezeko la kasi la maji ya mvua. Hivyo mji huo una wazo la kutumia viwanja vingi zaidi ya mji wakati wa kuuendeleza mji, katika nyakati za kawaida vinatumiwa na watu kwa kuegesha magari au kwa shughuli nyingine za umma, wakati inaponyesha mvua kubwa, viwanja hivyo vinabadilika kuwa vya kulimbikiza maji ya mvua.

    Bw Arnaud Moluna alisisitiza kuwa licha ya kulimbikiza maji ya mvua, uwanja wa maji vilevile ni kivutio cha mji, pia unaweza kuwa na ufanisi wa kubadilisha sura ya mji na kuboresha sehemu zenye hali duni za mji huu. Mto Rhine unapita nchi 7 za Ulaya, mwisho unaingia baharini nchini Uholanzi, mto Rhine uliwahi kuuletea mji wa Rotterdam vitu vingi vyenye uchafuzi baada ya kupita sehemu ya viwanda ya Ruhr nchini Ujerumani. Ili kutatua suala hilo, Uholanzi imetenganisha kabisa sehemu ya maji ya kunywa na mfumo wa kusafishia maji taka, ilijenga kiwanda kikubwa cha kusafishia maji chini ya ardhi, na kutumia teknolojia ya kisasa kabisa ya kuondoa ammonia na nitrate, wala siyo mbinu ya kawaida inayotumika sana ya kuua vijidudu katika maji kwa kutumia chlorine, kwa hiyo maji yanayotumiwa kwa kunywa ni maji safi ya hali nzuri sana.

    Hivi sasa katika sehemu yoyote ya Uholanzi, watu wakifungua bomba la maji, wanaweza kupata maji safi sana ya kunywa yasiyo na chlorine, haya ni mafanikio ya Uholanzi, ambayo watu wa nchi hiyo wanajivunia sana. Kutenganisha kabisa sehemu ya kuchukua maji ya kunywa na mfumo wa kusafishia maji taka, kunapunguza sana hatari ya kuibuka maradhi ya kuambukiza, pia kunaboresha mito na mifereji ya mji wa Rotterdam, na kuboresha maisha ya mji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako