• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji 0622

    (GMT+08:00) 2010-06-22 17:07:29

    Msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija wa S.L.P 1067 Kahama Shinyanga Tanzania, ametuma barua akisema awali ya yote napenda kutumia wasaa huu kuwajulia hali watangazaji wote wa idhaa ya Kiswahili ya CRI. Ni dhahiri kuwa mwaka jana mkuu wa shirika la utangazaji Tanzania TBC na sauti ya Tanzania Zanzibar STZ, walifanya ziara ya kuitembelea CRI na kufanya mazungumzo na mkuu wa Redio China Kimataifa ili idhaa ya Kiswahili ya CRI ijenge mtambo wa masafa mafupi ya FM ili matangazo yake yaweze kusikika kupitia TBC na STZ je mpango huo umefikia wapi?

    Hata hivyo nawaomba wahusika wote muharakishe mapema iwezekanavyo ushirikiano huo wa kuboresha usikivu wa matangazo ya idhaa ya Kiswahili ya Redio China Kimataifa ili matangazo yenu yasikike vizuri zaidi hapa Afrika Mashariki hususan nchini Tanzania. Pia nawaomba mturahishie namna ya kutuma salamu zetu kwa kutumia namba yenu ya simu, kwani kufanya hivyo wasikilizaji kutoka Tanzania wataongezeka zaidi, kwani wengi wetu tunashindwa kutumia kwa njia ya barua pepe kutokana na nchi zetu za Afrika bado gharama ni kubwa kutumia mtandao wa intenet.

    Tunakushukuru sana msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija kwa barua yako, kwanza tunapenda tukutoe wasiwasi kuhusu urushaji matangazo huko Tanzania, kwa kweli mpaka sasa hatua iliyofikia ni nzuri, kwani Zanzibar tayari matangazo yetu yameanza kurushwa kwa majaribio na hivi karibu yataaanza kurushwa rasmi, kwa upande wa Tanzania bara juhudi bado zinaendelea lakini haitachukua muda mrefu sana.

    Msikilizaji wetu mwingine ni Kaziro Dutwa wa S.L.P 209 Songea Ruvuma Tanzania anasema nafurahi sana kupata fursa hii kuandika barua nikitumai kuwa nyote ni wazima na mnaendelea kuchapa kazi zenu kama kawaida. Ama kwa leo nina machache ya kuzungumza kwa nia ya kutoa dukuduku langu moyoni kuhusu kipindi chenu maarufu cha sanduku la barua kwa kweli kimefanyiwa marekebisho mengi makubwa baadhi ni mazuri na mengine siyo ya kuridhisha kwa upande wangu.

    Mathalan kipindi hicho kimekatwakatwa kama samaki, awali kipindi hiki kilikuwa kinachukua sehemu kubwa kwa kushughulika na barua, maoni mahojiano na mambo mengine muhimu yaliwahusisha wasikilizaji moja kwa moja, wageni walotembelea China, wanafunzi wanaosoma China nakadhalika. Lakini leo msikilizaji ambaye ndie mdau mkubwa wa kipindi hiki amepewa nafasi ndogo tu ndio maana hata barua zinasomwa kwa ufupi na ni barua chache tu hii siyo sawa na maudhui ya kipindi hiki ndio uga mwanana wa wasikilizaji kutoa yote aliyonayo moyoni ya kukosoa, kupongeza, kushauri na kutoa maoni mbalimbali juu ya vipindi vyenu husika.

    Hapa ndio wasikilizaji huongea nanyi wahusika wa CRI, hutega masikio, lakini kuingiza vipindi vingine kwa kweli hakutoi fursa kwa wasikilizaji kutoa mawazo na kutambuana kifikra baina ya msikilizaji na msikilizaji.

    Mifano ya hayo niliyoyataja iko mingi lakini nitagusia kipindi husika cha tarehe 3 mwezi wa 4 mwaka huu, sina shaka kwa yeyote aleyesikiliza kipindi hiki ataafiki haya ninayoyasema atajua kipindi kilianza na nini na kilimalizika na nini, na kibaya zaidi huhusisha matukio ya nchi moja pekee (siwezi kuitaja). Ni ukweli usiopingika kuwa binadamu tu wagumu kupokea mabadiliko lakini kwa hisani yenu tunaomba kipindi cha sanduku la barua sehemu kubwa iachwe kwa barua za wasikilizaji tu nitashukuru sana iwapo hili litazingatiwa.

    Mwisho nawapa pongezi kwa ubunifu wenu mzuri katika kupanga, kurekebisha na kutangaza kwa ustadi vipindi vyenu, hakika sote tupo pamoja kwa lengo moja tu kuijenga CRI, ahsante sana.

    Nasi tunakushukuru sana msikilizaji wetu Kaziro Dutwa kwa dukuduku lako na maoni uliyotoa, kwani tunaamini kuwa yote hayo ni kwa lengo la kuboresha vipindi vyetu, ila kwa kukujibu ni kuwa kwanza barua huwa hatuzisomi kwa ufupi karibu zote tunazisoma kwa ukamilifu wake, isipokuwa kuna baadhi ya barua ambazo zinakuwa na kurasa 4 au tatu kwa kweli hizo ni nyingi na ndipo tunapojaribu kufupisha kidogo kwani tukisema tuisome barua yote wengine hawatapata nafasi, na lengo la kipindi hiki ni kuwashirikisha wasikilizaji mbalimbali sio mmoja tu, lakini kweli tunasikitishwa na barua tulizotumiwa ambazo ni chache zinazostahili kusomwa, ni matumaini yetu kuwa wasikilizaji wetu wataendelea kutuandikia na kutoa maoni na mapendekezo. Pili kipindi hiki kina sehemu ya barua na makala au maelezo ambayo tunatumiwa na watangazaji wetu wa Kenya na hii ndio sababu kuwa maelezo hayo mengi yanahusu Kenya. Hata hivyo maoni yako tumeyasikia na tutayafanyia kazi zaidi, ni matumaini yetu kuwa utaendelea na juhudi za kutoa maoni na mapendekezo kuhusu vipindi vyetu .

    Na sasa ni barua ya Franz Manko Ngogo anuani yake ya barua pepe ni rasmanko2003@yahoo.com, anasema ninafuraha na ninawashukuru kwa moyo wenu wa kunisaidia. Nashukuru sana kwa kunitumia vitabu vya jifunze kichina. Fursa hii ya vitabu itanisaidia mimi na wanachama wa club yetu ya Kemogemba. Tayari tilishaanza mikakati ya darasa la masomo ya kugha za kigeni. Tutazidi kupeana marejesho ya maendeleo ya mpango huu mahsusi.

    Ahsante sana Bw. Franz Manko Ngogo kwa barua yako fupi, sisi tunakutakieni mafanikio makubwa katika darasa lenu, na muendelee na moyo huohuo wa kupenda kujifunza zaidi, ahsante.

    Msikilizaji wetu Abdi Saidi Iyulu wa SLP 816 Kondoa, anasema ninawaombea Mungu watu wa China awajaalie waendelee kushika hatamu ya kuutetea ujamaa, pia ninawaombeni mjihadhari na ujanja wa mataifa ya kibepari wa kuwataka ninyi muwapeleke wananchi wenu kwenda kwao kusoma elimu ya mambo ya uchumi, biashara, utawala, uongozi na sheria, kwasababu mambo haya matano yanayotumika katika utawala wa ofisi za mataifa yote ya dunia hii yanalenga mataifa ya kibepari na kifalme. Ndiyo maana mataifa yote yenye mfumo wa kijamaa yanashindwa kuendesha serikali kwasababu yanalenga tawala za mifumo ya kibepari na kusababisha siasa kushindwa au kupishana na serikali zao.

    Kwa sababu unapohitimu shahada yoyote katika fani hizo tayari unakuwa umeshaingia kwenye mfumo wa kibepari bila kujijua na elimu hii ndio wanayojivunia zaidi katika kueneza ubepari kwa mataifa mengine hapa duniani. jambo kubwa wanalosisitiza ni umuhimu wa kuendelea kifedha, badala ya kutafuta mfumo wa uchumi unaorahisisha maisha ya watu katika kukidhi mahitaji yao. kwasababu hii ndio njia kuu ya kuwawezesha kuwatawala na kuwahujumu watu wa mataifa mbalimbali. Bila kuona kwamba sasa umefika wakati wa kutafuta mbadala wa kitu kingine badala ya pesa kwani maovu yote yanayotokea hapa duniani yanasababishwa na matumizi ya pesa, kwa mfano wizi, hongo za kudhulumu haki za watu, majeshi yanayokodiwa kuvamia mataifa mbalimbali n.k.

    Kwa hiyo kunapokuwa na uwezeshaji wa kukidhi mahitaji ya watu hata mambo maovu pia yatapungua. Kwahiyo taifa la China msije mkajiingiza kwenye utawala huo wa kibepari kwani nyie ndio tegemeo la mataifa ya kijamaa.

    Shukrani nyingi msikilizaji wetu Abdi Saidi Iyulu kwa maoni yako, tunakuomba tu uendelee kutuandika maoni mengine mbalimbali kuhusu mada tofauti. Ahsante sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako