• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazo jipya la kujenga mji unaofaa kuishi

    (GMT+08:00) 2010-07-15 17:54:29

    Bibi Liu Fangfang ana umri wa miaka 28, yeye ni mmoja kati ya waliohamia mjini Shanghai. Sasa anafanya kazi katika shule ya kifaransa huko Shanghai, na anaridhika na kazi hiyo. Jambo moja tu linalomsumbua ni nyumba. Alisema,

    "Kazi yangu inanifanya nijione kuwa nimejiunga na jamii. Nilirudi kutoka Ufaransa, na maisha ya sasa ni sawa na yale ya miaka mitano iliyopita. Ninaridhika na kazi hii. Lakini sasa umri wangu utakaribia miaka 30, tungeunda familia na baadaye tukiwa na mtoto, ni lazima tununue nyumba, hivyo tunapaswa kuzingatia jambo hili."

    Kabla ya kununua nyumba huko Shanghai ni lazima kuzingatia bei, urahisi, zana zinazoambatana na mahitaji ya wakazi na mazingira ya karibu. Bibi Liu Fangfang na mume wake wanataka kununua nyumba kusini mwa Shanghai. Bibi Liu alisema,

    "Sehemu hiyo iko mbali kidogo, na sasa subway haijafika huko, lakini katika miaka miwili ijayo subway itafika huko, na majengo yanayoambatana na mahitaji ya wakazi yatakamilika zaidi, hivyo maisha yatakuwa rahisi."

    Maskani ya bibi Liu Fangfang ni mji wa Luoyang, mji mdogo nchini China, ambao utamaduni na mazingira yake ni tofauti sana na mji wa Shanghai. Katika miji mikubwa wahamiaji wengi wapya wanakabiliwa na tatizo la kupata nyumba. Tofauti na watu wa nchi za magharibi, Wachina wengi wanadhani kuwa kumiliki nyumba na kuwa na familia mjini ni jambo muhimu.

    Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yamechagua "miji bora, maisha bora" kuwa kauli mbiu yake, na yanataka kujadili ufumbuzi wa busara zaidi, ambao sio tu utakidhi mahitaji ya nyumba ya watu wanaoongezeka siku hadi siku mijini, bali pia utaweka mazingira mazuri na rahisi yanayofaa kuishi. Eneo lenye hekta 15 kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai, ambalo linaonesha sehemu za mjini zenye uzoefu mzuri, linatoa wazo jipya la kutafuta ufumbuzi kuhusu suala la nyumba.

    Katika majumba mengi ya eneo hilo, jumba la Madrid la Hispania linafuatiliwa zaidi. Jumba hilo linawaonesha watalii "nyumba maalum inayojengwa kwa mianzi" mjini Madrid. Nyumba ya aina hiyo licha ya kuweza kuzuia joto la jua katika majira ya joto, na kuzuia badiri katika majira ya baridi, pia inapitisha vizuri mwanga na hewa kuingia ndani wakati wa mchana, vilevile gharama za kujenga nyumba zinapunguzwa. Kila mwaka serikali ya Hispania inajenga nyumba mpya, ili kukidhi mahitaji ya watu na familia mbalimbali.

    Mkuu wa jumba la Madrid Bw. Pedro Berraondo alisema, watalii wa China wanafuatilia sana miradi yao, wanataka kujua jinsi Madrid inavyokidhi mahitaji ya watu wengi zaidi. Bw. Pedro alisema,

    "Nchini Hispania, watu wanaweza kuomba nyumba za aina hiyo zinazojengwa na serikali, lakini serikali itazingatia hali ya familia za watu hao na mapato yao, watu wakiwa na mapato makubwa na kama tayari wana nyumba, basi hawawezi kuomba nyumba hizo. Ni rahisi zaidi kwa wanafunzi wanaohitimu, wataliki na walemavu kupata nyumba hizo."

    Bw. Pedro alisema katika miaka ya hivi karibuni, bei ya nyumba mjini Madrid pia imekuwa inapanda kwa kasi, lakini nyumba zilizojengwa na serikali, bei zake hazina mabadiliko makubwa, na serikali imeweka sheria kuhusu majengo yanayoambatana na mahitaji ya wakazi, ili kuhakikisha kuwa wanaweza kuishi vizuri.

    Katika miaka ya hivi karibuni, China pia imekuwa inaimarisha utekelezaji wa mradi mkubwa wa kuhakikisha ujenzi wa makazi, ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi wanaohitimu na watu wenye pato la chini. Kwa mujibu wa mpango wa serikali ya China, mwaka huu itajenga nyumba milioni 3 kwa ajili ya watu hao. Mwaka jana Shanghai pia ilitoa sera maalum kuhusu ujenzi, utoaji na usimamizi wa nyumba za serikali za bei nafuu.

    Kuweka mazingira yenye urahisi yasiyo na uchafuzi ni kiini cha maendeleo ya miji katika siku za usoni. Ofisa wa serikali ya mji wa Vancouver bibi Wendy Au alisema, baada ya kuandaa maonesho ya kimataifa ya mwaka 1986, Vancouver iligundua "njia ya Vancouver", na inashughulikia kwa ufanisi uhusiano kati ya ongezeko la idadi ya watu mijini na mazingira na maendeleo ya uchumi. Bibi Wendy Au alisema,

    "Tulifuatiliwa zaidi kutokana na maonesho ya kimataifa ya mwaka 1986, kwa kutumia fursa hiyo, tuliujenga mji wa Vancouver kuwa mji unaofaa kuishi, hivi sasa jumuiya ya kimataifa inauchukua kuwa ni mji usio na uchafuzi. Tunafuatilia mawasiliano, ambayo ilikuwa ni kauli mbiu ya maonesho ya kimataifa ya mwaka ule, na tulifanya juhudi kuongeza urahisi wa mawasiliano. Tulipokumbuka historia tumegundua kuwa idadi ya watu mjini iliongezeka kwa asilimia 25, lakini idadi ya magari ya binafsi ilipunguzwa kwa asilimia 17, tumepata mafanikio katika kueneza usafiri wa umma na baiskeli. Nafasi za ajira pia zinaweza kupatikana kutokana na kushughulikia mambo yasiyo na uchafuzi, tuna matumaini kuwa mji wetu utakuwa mji unaotoa uchafuzi kidogo zaidi kwa mazingira duniani ifikapo mwaka 2020."

    Kwa mujibu wa takwimu mpya, upanuzi wa miji nchini China umezidi asilimia 46, na unaendelea kuharakishwa. Msanifu mkuu wa eneo la kuonesha sehemu mjini yenye mwenendo mzuri Bw. Tang Zilai anaona kuwa, mchakato wa kuendeleza miji nchini China unakabiliwa na changamoto nyingi. Alisema,

    "China ni nchi inayoendelea yenye idadi kubwa zaidi ya watu duniani. Hivi sasa mchakato wa kuendeleza miji unaharakishwa, na umepata mafanikio mengi, lakini pia unakabiliwa na changamoto nyingi. Naona kuwa kuheshimu wakazi, maumbile, historia, sayansi na teknolojia ni mambo muhimu zaidi katika kujenga miji bora na maisha bora."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako