• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barua za wasikilizaji

    (GMT+08:00) 2010-07-20 16:54:02

    Msikilizaji wetu Hilali Nassor Zahor Alkindy wa S.L.P 22, P.C 119 Oman ametuletea barua akisema Radio Uchina natoa shukrani nyingi sana kwenu kwa kadi na picha, kwakweli zina maonesho mengi sana. Basi sijapata kalenda ya 2010.

    Barua nyingine inatoka kwa Bwana Anari Bob (arts) wa S.L.P 1246, Kisii, Kenya. Anasema pokea salamu nyingi za mwaka mpya 2010. Ningependa kuchukua fursa hii kwa kusema pongezi kwa watangazaji wa radio CRI kwa kazi yenu mnayotufanyia kama sisi wanachama wa CRI Radio Kimataifa.

    Mimi hapa ningependa mnitumie kalenda, bahasha na kadi za salamu. Mungu awabariki.

    Shukrani za dhati wasikilizaji wetu Hilali Nassor Zahor Alkindy na Anari Bob kwa barua zenu fupi, kwakweli kalenda tumezituma kwa wasikilizaji wetu wengi, sijui kwanini nyinyi bado hamjapata, hata hivyo tutajitahidi kufanya utaratibu wa kukutumieni tena hizo kalenda za mwaka huu pamoja na kadi na bahasha.

    Msikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija wa S.L.P 1067 Kahama Shinyanga Tanzania, anasema wafanyakazi wa Redio China Kimataifa natumai kwamba hamjambo sana na mnaendelea kuchapa kazi kama kawaida huko mjini Beijing China. Mimi huku naendelea kufuatilia matangazo ya redio China kimataifa ya kila siku pamoja na kutuma barua mara kwa mara.

    Aidha naomba kuchukua wasaa huu ili kuwapa pole sana wananchi wa Haiti pamoja na Chile huko Amerika ya kati na kusini kwa kuwapoteza wapendwa wao kutokana na matetemeko ya ardhi yaliyotokea katika nchi hizo. Ambapo watu wengi sana walifariki kutokana na maafa hayo na wengine wengi kupoteza makazi pamoja na mali zao. Hata hivyo naomba viongozi mbalimbali wa nchi za Haiti na Chile pamoja na wananchi waliopoteza ndugu zao waendele kuwa na subira, poleni sana kwani kazi ya Mungu haina makosa, kwa msiba huo tuko nanyi na mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi amin. Vilevile kwa upande mwingine natumia fursa hii ili kuzipongeza nchi pamoja na mashirika mbalimbali yaliyojitolea katika kutoa misaada ya aina mbalimbali katika nchi hizo ambazo ni pamoja na China, Japan, Marekani, Ujerumani, Russia, India, Hispania, Uingereza, Ufaransa na shirika la umoja wa mataifa. Ambapo nchi pamoja na mashirika hayo yamejizatiti katika kutoa wataalamu wa fani ya uokoaji, ambao pia wanatoa vyakula, dawa, fedha n.k. na ninazipongeza sana kwa msaada wao kwa Chile na Haiti kwani misaada hiyo imeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa. Ahsante sana.

    Na sasa ni zamu ya Bwana Geofrey Wandera Namachi wa Eveready Security Guard S.L.P 5733 Nairobi Kenya, anasema kutokana na tetemeko lililotokea nchini Haiti mapema mwaka huu na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ya haiti pamoja na vifo na majeruhi ya watu wengi, tukio hilo liliwashangaza walimwengu wengi, ingawa inaarifiwa kuwa taifa la Haiti ni miongoni mwa mataifa duni ama masikini duniani lakini shida haijali masikini wala tajiri, muhimu ni kutafuta njia ya kurejesha sura ama taswira ya Haiti lakini tangu tukio hilo litokee china imekuwa mstari wa mbele kutoa msaada, china imeonesha moyo wa ndani na nje kwa kutoa kila aina ya usaidizi uliohitajika kwa Haiti. Hatua ya kwanza china ilijifunga kibwebwe na kutuma kwa haraka iwezekanavyo makundi ama vikosi vya uokoaji. Pili china ilituma shehena kubwa ya vitu mbalimbali vya msaada kama vile chakula, maji dawa mahema pamoja na majenereta. Sio hayo tu china imetuma watu wa kujitolea madaktari pamoja na wakalimani wa lugha. Isitoshe china ilitoa msaada wa kifedha na kuahidi kuendelea kuisaidia Haiti ili irejee katika hali yake ya kawaida, natumai kuwa usaidizi wa china ni ishara tosha ya amnai na umoja duniani. Mwisho bendera ya China ya urafiki amani na umoja itaendelea kunyanyuliwa siku hadi siku. Hongera china na kila la kheri.

    Tunawashukuru sana wasikilizaji wetu Stephen Magoye Kumalija na Geofrey Wandera Namachi kwa maoni yao kuhusu matetemeko ya ardhi yaliyotokea Haiti na Chile, ni muda sasa umepita tokea nchi hizo zikumbwe na majanga hayo, na tumeshuhudia nchi nyingi zikijitolea kupeleka waokoaji na kutoa misaada ya aina mbalimbali, hii yote ni kuonesha umoja na mshikamano duniani hasa nchi moja inapokumbwa na tatizo kubwa kama hilo la tetemeko la ardhi. Ahsante sana.

    Na barua ya mwisho inatoka kwa msikilizaji wetu Kilulu Kulwa wa S.L.P 161 Bariadi Shinyanga Tanzania anasema ni matumaini yangu kwamba nyote hamjambo na mnachapa kazi barabara, ninawashukuru kwa vipindi vyenu murua mnavyotuandalia pamoja na habari za kila siku zenye kutusisimua na zinazoaminika.

    Aidha redio China kimataifa imekuwa karibu na wasikilizaji kwa kuwa na vipindi maalumu vinavyotuhusisha moja kwa moja sisi wasikilizaji wenu. Zaidi ya hayo kila mwaka redio China kimataifa kwa kushirikiana na wadau wengine wa mikoa, miji, taasisi na mashirika mbalimbali ya China imekuwa ikiandaa mashindano ya chemsha bongo kuhusu ujuzi wa mambo na matukio kadha wa kadha ya China na dunia nzima. Kwa kweli utaratibu huo ni mzuri sana mimi ninaupenda na kuupigia upatu msikilizaji wenu na rafiki wenu wa dhati wa China.

    Ni ukweli wa mambo kuwa China ni nchi kubwa inayoendelea ambayo imekuwa na diplomasia nzuri sana inayohimiza amani na ushirikiano baina ya nchi na mataifa kote duniani. Sera ya China katika masuala mengi ya kimataifa na kikanda inakubalika na kuungwa mkono sana na watu wengi katika pembe zote za dunia. Afrika ni sehemu ambayo ushirikiano na misaada ya China inathaminiwa, inakubaliwa na kupewa kipaumbele, hii ni kutokana na historia na nia nzuri ya China kwa nchi za bara la Afrika, ambapo ushirikiano huo na urafiki wa kindugu umekuwa na rekodi ndefu ya kihistoria tangu enzi na dahari. Kwa mantiki hiyo nchi ya China imejipatia heshima na umaarufu mkubwa barani Afrika na duniani. China pia imesimama imara katika masuala mengi ya msingi ikiwa ni pamoja na kulinda kwa ukamilifu maslahi ya nchi nyingi zinazoendelea katika jukwaa la kimataifa, yakiwemo masuala ya uchumi na biashara, mabadiliko ya hali ya hewa au tabia nchi, utunzaji wa mazingira, masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano duniani ukiwemo mtandao wa internet, mambo ya utandawazi n.k.

    Lengo la China ni kujenga dunia ya amani, maendeleo na masikilizano kwa watu wote duniani, hilo ni jukumu na azma ya watu wote wapendao amani na maendeleo duniani. Hivyo basi naipongeza sana China kwa mipango mikakati hiyo ambayo inamanufaa makubwa katika kujenga dunia yetu hii nzuri, asanteni sana.

    Shukrani nyingi msikilizaji wetu Kilulu Kulwa kwa maoni yako, kwa kweli China ni nchi inayopenda amani na utulivu wa dunia, pia haipendi kuingilia kati mambo yanayohusu nchi nyingine, hii ni sera ambayo inajitahidi kuifuata na kuitekeleza kila siku. Ni matumaini yetu kuwa, nchi nyingine pia zitajitahidi kuheshimu maamuzi ya nchi pamoja na kutoingilia kati mambo ya nchi nyingine ili kuifanya dunia iwe mahali pa amani daima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako