• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Islamabad-Mjumbe wa balozi wa China nchini Pakistan awatembelea wafanyakazi wa China waliokumbwa na mafuriko

    (GMT+08:00) 2010-08-03 19:16:29

    Kansela wa ubalozi wa China nchini Pakistan Bw. Huang Xilian ambaye ni mwakilishi wa balozi Liu Jian asubuhi ya tarehe 3 akiwa kwa niaba ya balozi Liu Jian amewatembelea wahandisi wa China waliokumbwa na mafuriko ambao wamehamia ubalozi wa China .

    Tarehe 29, Julai, mradi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa maji cha Khyber Pakhtunkhwa ulikumbwa na mafuriko hayo, ambapo watu 268 wa kampuni ya China walikumbwa na maafa na wengine watatu hawajulikani walipo, sasa wachina hao wamehamishwa kwenye sehemu iliyo salama.

    Bw. Huang amesema ubalozi wa China na serikali ya Pakistan zinazingatia sana wafanyakazi wa China waliokumbwa na mafuriko hayo, na kutokana na juhudi za uokoaji, wamenusurika. Amewaagiza viongozi wa kampuni ya China kuwa ni lazima kuwahakikisha wachina 14 wanaoendelea kufanya kazi kwenye sehemu ya mradi huo wanakuwa salama na kuzuia maafa isitokee tena, aidha, ni lazima kujikinga na maradhi ya maambukizi yanayoweza kutokea baada ya mafuriko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako