• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijana anayetoa huduma nchini Liberia

    (GMT+08:00) 2010-08-05 17:06:49

    Bw.Meng Xiangwei

    Katika miaka mitatu iliyopita, China iliwatuma watu wanaojitolea kwenda katika nchi mbalimbali za Afrika kutoa mafunzo. Mwaka 2009 mwanafunzi wa shahada ya pili wa kitivo cha hisabati na sayansi ya upashanaji wa habari cha chuo kikuu cha Yantai Bw. Meng Xiangwei alikuwa mmoja kati ya vijana 12 wanaojitolea wa mkoa wa Shandong, China kwenda nchini Liberia. Bw. Meng Xiangwei hatasahau alioishi barani Afrika.

    Kwenye mkutano wa wakuu wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2006 hapa Beijing, China iliahidi "kuwatuma watu 300 wanaojitolea kwenda nchi za Afrika katika miaka mitatu iliyofuata". Na katika mwaka 2007 mkoa wa Shandong ulituma kikundi cha kwanza chenye watu 15 wanaojitolea nchini Zimbabwe.

    Mwezi Aprili mwaka 2009 mkoa wa Shandong ulituma kikundi cha pili cha vijana wanaojitolea wa China nchini Liberia. Vijana hao 12 wanashughulikia kazi mbalimbali zikiwemo utoaji mafunzo ya lugha ya Kichina, huduma ya kilimo, teknolojia ya kompyuta, mafunzo ya michezo na huduma za matibabu, Bw. Meng Xiangwei alikuwa mmoja wao. Wakati mwandishi wetu wa habari alipomuuliza ni kitu gani kilichomhimiza achague kuwa mtu anayejitolea, Bw. Meng Xiangwei alisema,

    "Tokea utotoni nilikuwa na ndoto ya kutembelea nchi nyingine, hivyo nilifurahi sana kupata fursa hii. Baada ya kufikiri kwa muda mrefu, nilikabidhi taarifa ya kujisajili tarehe 16 Aprili mwaka 2009, halafu baada ya mtihami mgumu, nilibahatika kuwa mmoja kati ya watu 12 wanaojitolea."

    Bw. Meng Xiangwei alisema katika mwaka mmoja aliotoa huduma nchini Liberia, alishughulikia kazi za kuondoa matatizo ya kompyuta na kuongeza habari mpya kwenye mtandao katika idara ya teknolojia ya mawasiliano ya habari ya wizara ya mambo ya nje ya Liberia. Wakati mwingine pia alikwenda katika vyuo vikuu vya Liberia kutoa mafunzo kwa wanafunzi kuhusu elimu ya kompyuta.

    Bw. Meng Xiangwei alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, watu wa huko bado hawana ufahamu wa kutosha kuhusu mtandao wa internet, na kompyuta zao nyingi walipewa na nchi nyingine. Bw. Meng alisema, wiki ya tatu baada ya kufika nchini Liberia, alianza kushughulikia kazi za kuondoa matatizo ya kompyuta na kuongeza habari mpya kwenye mtandao wa wizara ya mambo ya nje ya Liberia kuwa wa kisasa. Kila wakati rais wa Liberia anapofanya ziara au kuwa na habari muhimu, alitakiwa kuweka habari mpya kwenye tovuti haraka iwezekanavyo. Ili kuweka upya mfumo wa visa, Bw. Meng Xiangwei alitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa huko, alisema,

    "Baada ya kukagua njia ya wizara ya mambo ya nje ya Liberia ya kushughulikia kazi na mtandao wa wizara hiyo, nilitoa wazo la kuendeleza mtandao wa wizara hiyo, lakini kutokana na uhaba wa fedha, niliweza tu kushughulikia mtandao wa ofisini wenye vyombo viwili vya kupokea ujumbe, ingawa sikuweza kufanya mambo mengi, lakini bado nilifurahi sana, kwa kuwa nilifanya mambo kwa ajili ya watu wa huko kadiri nilivyoweza."

    Bw. Meng Xiangwei alisema baada ya kufika katika nchi ngeni, alibabaika na hakujua la kufanya, lakini urafiki wa watu wa huko ulimfanya aone furaha moyoni. Alisema,

    "Mwanzoni watu wote, watoto kwa watu wazima walituangalia kwa kutaka kujua mambo mbalimbali, na baadhi ya wakati watoto walikuja kutuomba peremende, niliona wanapendeza sana. Baadaye tulifahamiana na tulicheza mpira wa kikapu na soka pamoja na marafiki wa Afrika. Wakati mwingine pia niliwafundisha kucheza chess, na tukawa marafiki wakubwa."

    Bw. Meng Xiangwei alisema wakati alipoishi na watu wa huko, alitambua kuwa urafiki kati ya watu hauhusiani na tofauti za nchi au rangi ya ngozi. Alisema,

    "Siku moja nilishiriki kwenye mashindano ya soka, na wakati ule jua lilikuwa kali sana, pia nilikimbia sana, hivyo nilikuwa nimechoka kupita kiasi, baada ya kutoka uwanjani, nilijisikia vibaya, nilisikia kizunguzungu hata nilishindwa kusimama vizuri, nilitaka kutapika na kuona nyota. Marafiki wa Afrika walipoona hali hiyo walikuwa na wasiwasi, wakanisaidia nipumzike chini ya mti mkubwa, na mmoja wao alininunulia maji, hivyo nilipata faraja."

    Bw. Meng Xiangwei alisema katika sehemu aliyofanya kazi nchini Liberia, wenzake wengi ni "wanaopenda kujua mambo ya China", vilevile alipenda kuongea nao kuhusu mila, desturi na utamaduni wa China. Pia alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, wanathamini sana zawadi alizowapa. Alisema,

    "Niliwapa zawadi za vitu vyenye umaalumu wa kichina, vikiwemo vinyago vya wahusika wa mchezo wa opera ya Beijing na alama ya baraka ya Zhongguojie iliyosukwa kwa nyuzi nene ya rangi nyekundu, na walifurahi kupokea. Waliweka vinyago vya wahusika wa mchezo wa opera ya Beijing nyumbani kwao, kama wageni wanapowatembelea, huwa wanafurahi kuwaambia, walipewa vinyago hivyo na Meng, kijana kutoka China, wanajivuia sana. Vilevile walitundika Zhongguojie katika milango yao, wakiona kitu hicho kinaweza kuleta baraka kwao. Nilifurahi sana kuona kuwa wanafurahia zawadi zangu, pia walinipa vitu vyenye umaalum wa huko."

    Bw. Meng Xiangwei alisema ingawa sasa amerudi nchini China, lakini bado anawakumbuka marafiki wa Liberia. Alisema,

    "Baadhi ya wakati ninapolala huwa naona kuwa bado niko barani Afrika, kama kuna fursa ningependa kwenda tena Liberia kuwatembelea marafiki zangu. Hivi sasa ninaendelea kuwatumia dawa wanazohitaji mara kwa mara. Moyoni mwangu Heze ni maskani yangu ya kwanza, Yantai naichukulia kuwa maskani yangu ya pili, na Liberia ninaichukulia kuwa maskani yangu ya tatu. Nataka watu wengi zaidi waifuatilie Liberia, na kuwatakia marafiki wa huko waishi maisha mazuri zaidi, na uchumi wao upate maendeleo zaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako