• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumba la maonesho la Colombia si lina kahawa na zumaridi tu

    (GMT+08:00) 2010-08-09 14:56:06

    Kahawa ya Colombia

    Mnaposikia jina la nchi ya Colombia, mnakumbuka nini? Kahawa, zumaridi au muziki wa kilatin? Ikiwa unataka kuona utamaduni maalumu wa nchi za Amerika ya kusini na kutotumia pesa nyingi, basi jumba la Colombia lililoko kwenye maonesho ya kimataifa ya Shanghai ni chaguo zuri.

    Jumba la maoensho la Colombia liko kwenye sehemu C ya eneo la Pudong la maonesho ya kimataifa ya Shanghai. Kwenye mnara wa upande mmoja wa kuta za jumba hilo wamechorwa ndege maarufu wa Colombia wa macaw wenye rangi maridadi sana. Ukiangalia kutoka mbali inaonekama kama ni upinde kwenye anga ya sehemu ya C. Huko kuna mkahawa unaouza kahawa iliyotengenezwa kwa mbegu za buni za Colombia zilizosagwa palepale. Harufu nzito ya kunukia inavutia watu wengi.

    "Hamjambo? Karibuni katika jumba la Colombia! Hapa ni ukumbi mkuu wa maonesho wa jumba la Colombia, unaitwa moyo wa Colombia. Hebu niwaeleze kuhusu sehemu mbalimbali za Colombia. Sasa tazameni upande wa kushoto, hii ni sehemu ya Andean

    Wafanyakazi wa jumba la Colombia wanaweza kutoa maelezo kuhusu maonesho yao kwa watazamaji kwa lugha ya Kichina, licha ya hayo wanawafundisha watazamaji sentensi chache rahisi za Kihispania. Baada ya kuingia kwenye ukumbi mkuu wa maonesho, watazamaji wanaweza kuwasalimia Wacolombia walioko huko mara moja, na kama wakiweza kuongea vizuri, basi zawadi yao ni paketi ndogo ya mbegu za mbuni za Colombia au kipepeo.

    Karibu na mlango wa ukumbi mkuu wa maonesho kuna maporomoko ya maji yaliyotengenezwa, hewa nyevu inawafanya watu wajione kama wako katika nchi ya sehemu ya joto. Ukumbi wa mviringo umegawanyika katika sehemu 6 kwa kufuata maeneo makubwa 6 ya Colombia, kila moja ya sehemu hizo ina mazingira na maonesho maalumu.

    Kwa mfano, mazingira ya "sehemu ya Pasifiki" ni bahari ya rangi ya buluu, makontena yenye maneno ya "kutengenezwa Colombia" pamoja na sauti ya mawimbi ya baharini vinaonesha sura ya nchi hiyo iliyoko kwenye sehemu ya pwani ya bahari ya Pasifiki na uwezo wa maendeleo. "Sehemu ya Caribbean" ina ufukwe wenye mchanga wa kutengenezwa ikiwa pamoja na kielelezo cha ngome kubwa ya kulinda usalama wa pwani, inaonesha mandhari nzuri ya Caribbean. "Sehemu ya Andean" ni mahali ulipo mji mkuu wa Bogota na sehemu muhimu kwa uzalishaji wa kahawa, watazamaji wanaweza kufahamu hali ya usafiri maalumu wa Bogota wa cable car kutokana na picha kubwa zinazooneshwa, wanaweza pia kugusa mbegu za kahawa, ambazo hazijakaangwa. Sehemu inayovutia zaidi ni "sehemu ya Amazon", ambapo inaoneshwa miti mikubwa, mihenzirani, maua, vipepeo na ndege za aina nyingi, inaonekana kama sehemu moja ya msitu wa Amazon kuhamishwa nchini China. Bila shaka hii ni kielelezo, hata hivyo watazamaji wengi wanapiga picha ili kuweka kumbukumbu.

    Jumba la maonesho la Colombia

    Wakati wafanyakazi wa jumba la Colombia walipoona maonesho yao yanapendwa na watazamaji wa China, mtoa maelezo mmoja kijana Javier alisema

    "Kila siku tunapokea watazamaji 15,000 hadi 20,000. Wanapenda sana jumba la Colombia, vilevile wamekuwa na kumbukumbu nyingi kuhusu nchi yetu. Wakati tunapowaeleza umaalumu wa kila sehemu, kwa mfano wana shauku kubwa kuhusu mibuni na jengo kubwa lenye ngome. Wanaona Colombia ni nchi nzuri sana, na wanataka kutembela huko."

    Katika jumba la Colombia, watu wanaweza kubonyeza skrini ya Multimedia kufahamu uzoefu wa nchi hiyo katika mchakato wa ujenzi wa miji pamoja na uwezo wa uwekezaji na mambo ya biashara ya nchi hii iliyoko Amerika ya kusini, na inafanya watazamaji wawe na ufahamu zaidi kuhusu nchi hii. Bw Hu kutoka mkoa wa Zhejiang alifurahia sana vitu vingi vilivyooneshwa katika jumba la Colombia, akisema:

    "Nimepata kumbukumbu nyingi kuhusu zao la kahawa, misitu ya asili ya Colombia, pamoja na mambo waliyotueleza kuhusu aina nyingi za uzalishaji mali na utamaduni. Ninaona maonesho ya jumba hilo yametueleza kwa kirefu kuhusu nchi hiyo."

    Bibi Juana Rodrigues ni mtalii kutoka Colombia, alipanga mahususi kutembelea maoensho ya kimataifa ya Shanghai katika ratiba ya safari yake ya nchini China. Ni dhahiri kuwa hajasahau kutembelea jumba la Colombia, anataka kuona kama maonesho ya Colombia yanaonesha vizuri mambo ya nchi yake. Alisema

    "Maonesho mazuri sana! Jumba la Colombia ni zuri sana, wamefanya maandalizi mazuri. Nimeongea na wafanyakazi wa jumba hilo, wao ni wachangamfu sana, ninaona kama nimerejea kwetu. Kasoro moja tu kuwa wafanyakazi wanapoeleza kuhusu sehemu zao wangevaa nguo zenye umaalumu wa sehemu mbalimbali za Colombia."

    Katika duka linalouza vitu vya kumbukumbu lililoko ndani ya jumba la Colombia, watu wanaweza kuona baadhi ya nguo zenye umaalumu wa kisehemu. Mbali na hayo, mazao kadhaa ya Colombia, ambayo ni maarufu na maalumu sana katika dunia, kama vile kahawa, vito vya emerald na dhahabu pia yanauzwa huko. Naibu msimamizi mkuu wa jumba la Colombia Bi Laura Gaviria alisema, maonesho ya kimataifa yametoa fursa nzuri kwa Colombia kuwafahamisha watu kuhusu maliasili na utamaduni wake murua. Alisema

    "Tunafanya shughuli mbalimbali za kiutamaduni kila mwezi, kwa mfano, kufundisha ngoma halisi za kilatin na Salsa. Tutawafundisha wachina kucheza ngoma za kilatin zikiambatana na muziki wenye mtindo wa jadi na kisasa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako