• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Twende kuona maonesho ya kuruka kwenye jumba la Latvia

    (GMT+08:00) 2010-08-16 17:19:22

    Inapotajwa Latvia, nchi iliyoko kwenye pwani ya bahari ya Baltic, wachina wengi huona ni nchi ngeni sana. Lakini maonesho ya kuruka ndani ya bomba kubwa la upepo wa jumba la maoensho la Latvia kwenye eneo la maonesho ya kimataifa huko Shanghai, China unavutia watu wengi.

    "Msimamizi: Endelea!

    Watazamaji: Loo!

    Msimamizi: Vizuri sana!

    Watazamaji: Loo!

    Msimamizi: Mnaonaje?

    Watazamaji: vizuri sana!

    Msimamizi态watazamaji: Shime, shime!"

    Wapendwa wasikilizaji, mliyokuwa mkisikiliza ni kwenye maonesho ya kuruka kwenye jumba la maoensho la Latvia. Kila siku katika saa tatu na nusu asubuhi jumba la Latvia linafanya maonesho ya kuruka kwa ajili ya watazamaji ndani ya bomba kubwa la upepo lililosimama wima kwenye ghorofa ya pili la jengo hilo, ambapo marubani wawili kutoka Latvia wanafanya maonesho ya kuruka kwa dakika 10. Bomba hili la upepo limetengenezwa kwa kioo, upepo katika bomba unatokana na mtambo ulioko chini yake ukiigiza upepo ulioko nje ya ndege au chombo cha anga wakati zikiruka kwenye anga. Teknolojia ya upepo katika bomba ilivumbuliwa zaidi ya miaka 30 iliyopita, mwanzoni ilitumika kwa ajili ya mafunzo ya wanaanga na marubani wa ndege, ili kuwapa mazoezi ya kuwa katika mazingira maalumu ambayo vitu havina uzito. Kiongozi wa jumba la Latvia Bw Ansis Egle alisema, wanatarajia watazamaji wafurahi kutokana na maonesho hayo ya "Ninataka kuruka kwa juu zaidi". Alisema"Kauli-mbiu ya jumba hilo ni kuhusu watu waliopata mafanikio makubwa tofauti na wengine katika kazi zao. Hiki ni kitu tunachonufaika pamoja na watu wote duniani. Endapo unaruka utajisikia vizuri sana, na unaweza kuwaza kufanya mambo mengi zaidi. Kauli-mbiu yake ni kufanya uvumbuzi. Sababu ya watu hao, ambao ni tofauti na watu wengine, kuwa na furaha, ni kwa sababu wamefikia kiwango wanachotaka. Hiki ndio tulichotaka kuwaonesha na kuwafurahisha watazamaji wetu."

    Marubani wa jumba la Latvia wanajitahidi sana kuyafanya maonesho yawe mazuri zaidi. Wanaonesha miondoko mipya ya kuruka na ushirikiano wa kuruka, kwa hiyo maoensho ya kuruka wanayotazama watazamaji ni maonesho mazuri ya kipekee. Watazamaji wanavutiwa sana na maonesho yao, baada ya maonesho kumalizika, wanataka kupiga picha pamoja na marubani, na hawataki kuondoka mara moja, na wanawasifu sana marubani wanaofanya maonesho.

    "Ajabu sana!"

    "Sikuwahi kuona!"

    "Ajabu kweli kweli, watu wanaweza kuelea juu kama majini!"

    "maonesho ya kuruka" si kitu cha kuvutia kabisa, kitu kinachovutia zaidi katika jumba la Latvia ni watazamaji wenye bahati ya kupata kura ya kwenda kupata uzoefu ndani ya bomba la upepo, ambapo watazamaji baada ya kupewa maelekezo na marubani wataruka wao wenyewe kwa dakika kadhaa ndani ya bomba la upepo. Watazamaji waliochaguliwa, licha ya kuangalia video husika, wataelekezwa na marubani kuhusu mambo muhimu yanayopaswa kukumbukwa. Marubani huwaambia watazamaji wakisema: "Kitu muhimu ni kuwa uwe unalala chali au kifudifudi, usikaze mikono na miguu yako, wa usitumie nguvu."

    Bw Li kutoka Beijing na Bw Liu kutoka Anhui walibahatika kuwa watu wanaopata nafasi ya kuruka ndani ya bomba la upepo. Kutokana na maelekezo ya marubani, hawakujikaza tena bali wakalegea na kuondoka chini polepole na kupaa juu tena. Baada ya kuruka kwa dakika chache watu hao wawili walipata kumbukumbu nyingi, na walionekana hawataki kuondoka mle ndani. "Safi! Safi sana! Mimi ni mara ya kwanza kupata uzoefu wa namna hii, nilijiona kama ninaruka angani kabisa."

    "Sijatosheka bado, dakika ni chache sana, nitafurahi sana kama nitapata nafasi ya kuruka tena."

    Ingawa jumba la Latvia halioneshi vitu vingi vya kiutamaduni kama majumba mengine ya maonesho, na wala halioneshi utamaduni na historia ya nchi, lakini kuona maonesho na kupata uzoefu wa kuruka angani, inawafanya watazamaji wawe na kumbukumbu nyingi sana. Kiongozi anayeshughulikia uhusiano na watu wa jumba hilo Bw Wang Weihua alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema, usanifu wa jumba la Latvia ulizingatia sana "teknolojia ya furaha". Alisema"Wazo tunalotaka kuonesha kwenye jumba letu la maonesho ni kuwa maumbile yanaweza kuwepo pamoja na sayansi na teknolojia. Tunatumia teknolojia ya furaha kuboresha mazingira na maisha ya watu, teknolojia hiyo inaweza kuongeza furaha ya watu."

    Maonesho ya kimataifa ya Shanghai yanapokea watazamaji laki kadhaa kwa siku, kadiri watu wanavyotembelea maonesho ya kimataifa, ndivyo jumba la Latvia linavyopokea watazamaji wengi kila siku. Ingawa wafanyakazi wanachoka zaidi kutokana na ongezeko la watazamaji, lakini wanapenda kutembelewa na watazamaji wengi zaidi na kuona maoensho ya kufurahisha. Kiongozi mratibu wa jumba la Latvia Bw Ansis Egele alisema, watu wanaopenda furaha, njooni katika jumba la maonesho la Latvia."Ikiwa mnapenda furaha, msikose kufika katika maoensho yetu. Karibuni katika jumba la Latvia!"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako