• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumba la maoensho la Bilbao la Hispania

    (GMT+08:00) 2010-08-23 17:35:01

    Mji wa Bilbao ulioko sehemu ya kaskazini ya Hispania ni mji maarufu kwa mambo ya sanaa na utamaduni, lakini mwanzoni mwa karne ya 20, mji huu ulikuwa kituo muhimu cha viwanda vizito vikiwemo viwanda vya chuma na chuma cha pua, pamoja na viwanda vya meli. Katika miaka ya 80 ya karne ya 20 mji huu wa kale ulipita njia ngumu ya marekebisho na mabadiliko ya mtindo wa maendeleo. Kwenye eneo la miji yenye uzoefu mzuri kabisa la maonesho ya kimataifa ya Shanghai ya mwaka 2010, jumba la Bilbao liliwaonesha watu namna ya mji huu wa viwanda ulivyobadilika kuwa mji wa utoaji wa huduma wa kisasa.

    Mji wa Bilbao wenye historia ya miaka karibu 800 uko kwenye sehemu ya kaskazini ya Hispania. Mbele ya mji huu kuna bahari, na unazungukwa na milima katika pande nyingine tatu, mto mmoja mkubwa unapita katikati ya mji. Katika jumba la maonesho la Bilbao, msanifu akitumia vielelezo alionesha hali ya mji huu. Mkuu wa jumba la maonesho hilo Bi He Chen alisema, "Kielelezo hicho cha plexiglass ni kazi iliyofanywa na msanii wa Hispania Bw Ester Pizarro, ndani yake zimewekwa taa za LED, rangi ya kielelezo inabadilika kwa kufuatana na mandhari zinazooneshwa kwenye sinema."

    Ili kuonesha vitu vingi katika kielelezo kidogo, umaalumu wa kijografia na mabadiliko ya historia ya mji huu yanaoneshwa kwa alama tu. Kwa mfano, kielelezo hicho cha mji kimewekwa juu ya nguzo moja ya kukwaruza, kwenye pande mbili za kielelezo hicho kuna skrini mbili. Mtu akiangalia kwa makini anaweza kugundua tofauti kwenye skrini hizi mbili. Bi He Chen alisema, usanifu wa namna hii una maana yake: "Skrini ya upande huu inayowakilisha bahari ni angavu, na ya upande mwingine inawakilisha milima. Nguzo hii ya madini iliyoko chini ya kielelezo inawakilisha vitu vya nyakati zilizopita, yaani viwanda vya chuma na chuma cha pua, ambavyo ni nguzo yake na historia. Mali za mji zinajengwa juu ya msingi wa viwanda hivyo vya zamani."

    Kuna milima mingi kwenye pande zote za mji wa Bilbao, ambayo ina maliasili nyingi za madini ya chuma, hali hii maalumu ilifanya mji huu kuendeleza uzalishaji wa chuma na chuma cha pua na uundaji wa meli katika karne ya 18. Lakini ilipofika kipindi cha katikati na mwishoni mwa karne ya 20, mji huu wa kale ulikumbwa na maafa ya mafuriko, mbali na hayo msukosuko wa kiuchumi uliotokea hapo baadaye ulikuwa na athari mbaya kwa msingi wa viwanda vizito, ambao ulikuwa ni uhai wa mji. Bi Chen alisema "Bilbao ulikuwa ni mji maarufu wa viwanda ukishughulikia kazi za jadi za uzalishaji wa chuma na chuma cha pua, pamoja na uundaji wa meli. Kutokana na kukabiliwa na msukosuko wa fedha uliotokea katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, viwanda vingi vya mji vilifilisika, au kuhamishiwa kwenye sehemu nyingine."

    Ilipoelezwa kuhusu msukosuko wa miaka ya 80, hali mbaya ya mafuriko ilionekana kwenye skrini ya ukumbini, wakati huu taa nyingi za LED za rangi ya buluu zilizoko kwenye kielelezo cha mji wa Bilbao ziliwaka na kuonesha sehemu za mji zilizokumbwa na mafuriko. Wakati ilipooneshwa skrini kuhusu maandamano ya wafanyakazi na hata kukabiliana na serikali kutokana na kufilisika kwa viwanda na msukosuko wa uchumi, taa hizo ziliwaka kwa rangi nyekundu, na kuwafanya watu wawe na wasiwasi kuhusu hali ya mji huo. Lakini msukosuko huo vilevile unaonesha kupata fursa. Bi He Chen alisema: "Hali hii ilizifanya kampuni za zamani ziondoke kwenye mji wa Bilbao, na kuleta fursa inayouwezesha mji huu kujengwa kuwa mji mzuri wa hivi sasa, na kuwa na uwezekano wa kubuni mpango mpya kabisa."

    Watu wa Bilbao waliamua kutupilia mbali mtindo wa maisha wa zamani, na kujenga mji wao mpya wa utoaji huduma, na kufanya shughuli za utamaduni kuwa msingi wake. Mwaka 1992, sehemu za kando za mto Bilbao zilianza kuwa na shughuli nyingi. Baada ya kupita miaka 6, lilijengwa jengo moja adhimu ambalo kwa sasa ni jumba maarufu la makumbusho la Guggenheim, ambalo ni alama ya mji wa Bilbao. Katika muda huo mji mzima ulipita katika mageuzi makubwa: kufanya matengenezo kuhusu majengo ya kale, na kutumia ipasavyo rasilimali za utamaduni za majengo hayo ya kale; kufanya marekebisho makubwa kuhusu sehemu ya mji, kuboresha mawasiliano, kujenga mfumo wa usafiri wa umma, ambao wakati ule ulionekana ni mfumo mzuri kabisa; sambamba na jumba la makumbusho la Guggenheim, yalijengwa majengo mengi ya makumbusho, pamoja na majengo mengi ya kiutamaduni, mambo ya elimu na burudani.

    Kuhusu mabadiliko ya mtindo wa Bilbao, Bi He Chen aliyaita kuwa ni "mapinduzi" kabisa, akisema "Mchakato wa mageuzi ya mji wa Bilbao unaitwa mapinduzi ya mji, mapinduzi hayo yanalenga siku za baadaye, kufikiria mpango mzima wa maendeleo endelevu juu ya msingi wa kuhifadhi urithi wa kihistoria, mpango huu unaozingatia siku za baadaye ni mpango mzuri wa mageuzi ya mji mzuri wa siku za baadaye."

    Mpango huu kabambe unaongozwa na nani? Mji wa Bilbao una mbinu zake, Bi He Chen alisema, "manispaa ya mji huo haiwezi kumudu mpango huu mkubwa peke yake, kwa kila mradi iliundwa kampuni ambayo inashughulikia mradi huo peke yake, kampuni hii inaundwa kwa pamoja na viongozi wa manispaa, serikali ya wilaya, viwanda vya serikali na binafsi, hususan viwanda vikubwa vinavyohusiana na mambo ya miundombinu na mawasiliano. Kwa hiyo pande mbalimbali zinaweza kufanya kazi kwa hatua moja wakati wanapotekeleza mpango mkubwa."

    Baada ya juhudi za miaka zaidi ya 20, mji waBilbao wa leo umekuwa mji mkubwa wa shughuli za utamaduni barani Ulaya na duniani, kila mwaka kuna maelfu ya watalii wanaovutiwa kutembelea huko, kujionea vitu vyenye thamani kubwa vinavyohifadhiwa katika jumba la makumbusho la Guggenheim, na kujionea vivutio vya mji huo wenye urithi wa viwanda na msingi madhubuti wa utamaduni. Mwezi Mei mwaka 2010, mji wa Bilbao ulipata tuzo iliyotolewa kwa mara ya kwanza ya mji wa dunia wa Lee Kuan Yew. Tuzo hii inatolewa ili kutoa pongezi kwa shirika au mtu binafsi anayeweka mpango wa mji au kufanya usimamizi kuhusu mji kwa mtazamo wa mbali na wazo la uvumbuzi. Lakini Je, watalii wanapotoka kwenye jumba la Bilbao baada ya kuangalia maonesho, watakuwa na mawazo gani kuhusu mafanikio ya mabadiliko ya mji huo wa viwanda? Bi He Chen alisema"Maendeleo ya China yanasifiwa na watu. Kwa hiyo katika hali hii nzuri, tunapaswa kufikiria mambo mengi zaidi kuhusu namna ya kufanya miji yetu ya baadaye iwe mizuri zaidi, na kufikiria kwa ajili ya wananchi na vizazi vyetu vya baadaye. Kama meya wa mji wa Bilbao alivyosema, mji wa Bilbao unatarajia kunufaika na watu wa China kuhusu mafanikio na wazo la mageuzi ya mji ya miaka 25 iliyopita."

    Bi He Chen alisema hivi sasa miji mingi ya viwanda ya China inakabiliwa na suala la kubadilisha mtindo, namna ya kujenga mji mpya wa utoaji huduma kwa kuunganisha msingi wa viwanda vya zamani na shughuli mpya za uzalishaji mali ni suala ambalo kila mji unapaswa kulifikiri na kulifanyia utafiti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako