• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kujifunza lugha ya Kichina kunaimarisha urafiki

    (GMT+08:00) 2010-08-26 15:09:39

    Katikati ya mwezi Julai mwaka huu, mashindano ya 9 ya "daraja la lugha ya Kichina" ya wanafunzi wa vyuo vikuu duniani yalifunguliwa rasmi huko Changsha mkoani Hunan, China.

    "Sisi wawili tunawasalimia, na kuwatakia kila la heriā€¦"

    Je, kwa kusikia tu, unajua watu hawa wanaofanya maonesho ya ngonjera wanatoka nje ya China?

    Je, unaamini kuwa hawa watu wanaoimba wimbo wa China sio Wachina?

    Kama tukisema kuna daraja ambalo linawawezesha vijana wa China kuwasiliana na wale wa nchi mbalimbali duniani, kuonesha utamaduni unaong'ara wa lugha ya Kichina wenye historia ya zaidi ya miaka elfu moja, na kueleza msimamo wa China wa kuishi pamoja kwa amani na nchi majirani, basi hili ndilo "daraja la lugha ya Kichina".

    Usiku wa tarehe 15 Julai maonesho ya ufunguzi wa mashindano ya 9 ya "daraja la lugha ya Kichina" ya wanafunzi wa vyuo vikuu duniani yalifanyika huko Changsha mkoani Hunan. Wanafunzi 107 wa vyuo vikuu kutoka nchi 62 duniani walikuja mkoani Hunan, na watashiriki kwenye mashindano ya robo fainali na fainali katika wiki 5 zilizofuata. Naibu mkuu wa mkoa wa Hunan Bw. Guo Kailang kwenye ufunguzi huo alisema, ni jambo la kufurahisha kwa marafiki kutoka mbali kuja hapa? Aliwakaribisha marafiki kutoka nchi mbalimbali duniani wajione mila, desturi na utamaduni wa mkoa huo. Bw. Guo alisema,

    "Leo wamekuja mkoani Hunan kushiriki kwenye mashindano ya lugha ya Kichina, na wataonesha mvuto wa lugha ya Kichina. Haya hakika yatasaidia kuvutia fikra na mawazo mengi mapya, kuhimiza kufahamisha ustaarabu na utamaduni wa China kwa dunia, na mawasiliano kati ya utamaduni na ustaarabu wa China na wa nchi mbalimbali duniani."

    Mshiriki kutoka Russia bibi Wang Xiaoni alitoa hotuba akiwa kwa niaba ya washiriki wote akisema,

    "China ni nchi yenye mandhari nzuri, na Wachina ni wachangamfu. Mimi pamoja na washiriki wengine tumekuja hapa China kutokana na kuipenda lugha ya Kichina. Tunafurahi sana, na tuna matumaini kuwa katika mashindano hayo tutafanya vizuri zaidi."

    Katika mashindano yaliyofuata, marafiki kutoka nchi za nje walifanya maonesho ya muziki ya michezo ya sanaa ya China:

    Wachina wanapokula chakula wanatumia vijiti vya kulia, na watu wa nchi za nje hawajui kutumia vijiti. Lakini si tatizo kwa washiriki hao. Mshiriki mmoja alisema,

    "Mwanzoni nilipokuja China nilikuwa siwezi kutumia vijiti vya kulia, lakini sasa naweza kula kwa kutumia vizuri vijiti hivyo."

    Washiriki wa mashindano ya "lugha ya Kichina" sio tu wanaongea vizuri kwa Kichina, bali pia wanafahamu vizuri maana ya maneno ya Kichina. Mshiriki mmoja alisema,

    "Unajua maana ya 'chu shou'?

    Naona kuwa maana ya 'chu shou' ni kuwasaidia marafiki, wakati wowote rafiki yako anahitaji msaada wako unapaswa kumsaidia."

    Tofauti na mashindano ya "lugha ya Kichina" ya awamu zilizopita, mashindano ya awamu hii yanahusu "utamaduni wa kifamilia", ambayo yanaunganisha utamaduni wa China na kauli mbiu ya maonesho ya kimataifa ya Shanghai. "Utamafuni wa kifamilia" ulikuwa uzoefu wa kiutamaduni katika mashindano hayo. Washiriki 107 walishiriki kwenye shughuli za kuishi katika familia 63 zilizoko katika sehemu tatu za Changsha, Zhangjiajie na Fenghuang, na katika mashindano ya mwisho, vijana hao wageni pia walitakiwa kufanya maonesho na "jamaa zao" wa China.

    Safari katika mkoa wa Hunan wenye mandhari ya kuvutia na mila na desturi maalum iliwafanya wageni hao wafahamu zaidi utamaduni wa China hasa ule wa mkoa wa Hunan. Utamaudni huo ni kama maji yanayotiririka chini ya daraja dogo, ni mila na desturi ya kuvutia, pia ni moyo wa kujiendeleza. Shughuli hiyo ya kujionea utamaduni imewapa washiriki wa mashindano hayo kumbukumbu nyingi zisizowezakusahaulika. Mshiriki mmoja kutoka Australia Bw. Wei Tao alisema,

    "Hivi sasa uchumi wa China unaendelezwa kwa kasi, China hakika ni nchi muhimu duniani. Hivyo ni lazima kufahamu utamaduni, lugha na mawazo yao."

    Mashindano ya "daraja la lugha ya Kichina" ya wanafunzi wa vyuo vikuu duniani yanaandaliwa na ofisi ya uongozi wa utoaji wa mafunzo ya lugha ya Kichina ya China. Kuanzia mwaka 2002 ofisi hiyo imefanikiwa kuandaa awamu 8 za mashindano hayo, na washiriki karibu 70,000 wa nchi mbalimbali duniani wamepitia "daraja la lugha ya Kichina" kufahamu historia ya miaka 5,000 ya ustaarabu ya China, na hivyo kuwahimiza watu wa nchi na sehemu mbalimbali duniani kutoa mchango wao kwa ajili ya maendeleo yenye masikilizano duniani bila kuchafua mazingira ya maumbile.

    Jifunze lugha ya Kichina kwa furaha na kujenga daraja la urafiki. "Daraja la lugha ya Kichina" sio tu ni dirisha la China la kujionesha mvuto wake, bali pia ni daraja linaloiwezesha China kuwasiliana na dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako