• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakazi waliohamishwa kutokana na ujenzi wa eneo la maonesho ya kimataifa watembelea sehemu ya makazi yao ya zamani

    (GMT+08:00) 2010-09-02 14:37:34

    Katika miaka mitano iliyopita, ili kuunga mkono ujenzi wa eneo la maonesho ya kimataifa, wakazi wa huko walihamishwa, na hivi karibuni walitembelea sehemu iliyokuwa ya makazi yao ya zamani.

    Siku moja ya mwezi Agosti, mjomba Jin, bibi Xu na mtoto wao Xiao Jin walikwenda kutembelea eneo la maonesho ya kimataifa. Hisia zao za kutembelea maonesho ya kimataifa ni tofauti na za watalii wengine, kwani wao waliwahi kuishi katika sehemu hiyo kwa miongo kadhaa, ambayo sasa imekuwa eneo la maonesho ya kimataifa ya Shanghai, hivyo wana hisia za ndani na eneo hilo. Mjomba Jin alisema,

    "Jumba la Shanghai limejengwa katika sehemu ilipokuwa nyumba yetu ya zamani, tunaona fahari, kwa hiyo tumemleta mtoto wetu kutembelea hapa."

    Mtoto wa mjomba Jin na bibi Xu amekuwa na umri wa miaka 20, kutokana na shughuli nyingi za masomo, hakukuwa na muda wa kutosha kutembelea eneo la maonesho ya kimataifa. Lakini mjomba Jin alitaka kutembelea maonesho ya kimataifa pamoja na familia yake, maana alitaka kuhisi furaha ya matembezi pamoja na familia yake katika sehemu iliyokuwa nyumba yao ya zamani. Bibi Xu alisema,

    "Xiao Jin anasuribi kwenye msururu, tumekuja leo kutembelea maonesho ya kimataifa kwani tulimsubiri hadi shule zifungwe."

    Eneo la maonesho ya kimataifa lina kilomita za mraba 5.28, na wakazi 18,000 na makampuni 272 yalihamishwa kutoka sehemu ya eneo hilo. Ili kuwashukuru wakazi wa Shanghai kuunga mkono maonesho ya kimataifa, kabla ya kufunguliwa kwa maonesho ya kimataifa, serikali ya mji wa Shanghai iliipa kila familia ya Shanghai "zawadi ya maonesho ya kimataifa", ambayo ni pamoja na barua ya kuwashuruku wakazi wa Shanghai, tikiti moja ya maonesho ya kimataifa, kadi ya mawasiliano ya kumbukumbu, ramani ya eneo la maonesho ya kimataifa na beji ya kileta bahati ya "haibao".

    Alipozungumzia zawadi hiyo, bibi Xu alifurahi sana, kwa sababu familia yake ilipata zawadi nyingi zaidi kuliko wakazi wengine wa Shanghai. Alisema,

    "Sisi tuliohamishwa kutokana na ujenzi wa eneo la maonesho ya kimataifa, kila familia ilipewa tikiti mbili za maonesho ya kimataifa."

    Bibi Xu alikumbusha wakati ule walipopata habari ya kuhama alifurahi sana, kwa kuwa walijua wataenda kuishi katika nyumba mpya. Lakini mjomba Jin alikuwa hafurahi, kwani aliishi katika nyumba yao kwa miaka mingi, tena aliona kuwa sehemu waliyoishi ni nzuri zaidi kuliko sehemu wanayoishi sasa. Lakini siku hadi siku mjomba Jin alikubaliana na uamuzi huo. Kwa hiyo mjomba Jin na familia yake waliondoka kutoka kwenye nyumba ndogo waliyoishi kwa miongo kadhaa, na kuhamia kwenye eneo la makazi mapya ya Pujiang Shibo.

    Ili kuwapanga wahamiaji elfu 18, serikali ya mji wa Shanghai iliweka maeneo mawili ya makazi maalum kwa ajili ya watu wanaohamishwa, yaani makazi ya Pujiang Shibo na makazi ya Sanlin Shibo. Makazi ya Sanlin Shibo yako umbali wa kilomita 3 tu kutoka eneo la maonesho ya kimataifa, na makazi ya Pujiang Shibo yako umbali wa kilomita 15 hivi kutoka eneo la maonesho ya kimataifa. Baada ya kuhamia kwenye nyumba mpya, mjomba Jin alijihisi mwenyewe ubora wa kuhamia. Alisema,

    "Mazingira ya nyumba yameboreshwa, na mazingira ya mji pia yameboreshwa."

    Kwa hiyo alianza kufuatilia maonesho ya kimataifa ya Shanghai. Kila siku anafuatilia habari kuhusu ujenzi wa eneo la maonesho ya kimataifa, na hali ya maonesho, kwani anataka kutembelea tena eneo la makazi yao ya zamani pamoja na familia yake. Hivi sasa ndoto yake imetimizwa, wamekuja kutembelea eneo la maonesho ya kimataifa, na jumba wanalotaka kutembelea si jumba ambalo watalii wengine wanapenda kutembelea, bali ni Jumba la Shanghai linalojengwa katika eneo ilipokuwepo nyumba yao ya zamani. Bibi Xu alisema,

    "Bila shaka tutakwenda kutembelea Jumba la Shanghai, kwani zamani tulikuwa tunaishi katika sehemu hiyo, hivyo tunapenda kuona sehemu hiyo imejengwa kwa namna gani."

    Jumba la Shanghai liko katika eneo la uzoefu mzuri wa kuendeleza miji la sehemu ya Puxi, ambalo kauli mbiu yake ni "ujenzi wa kiikolojia, maisha bora". Mtoa maelezo kwenye Jumba la Shanghai Bw. Li Dongbin alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, anapopokea watalii wanaotembelea jumba hilo, anakutana na watalii wengi kama mjomba Jin ambao walihamishiwa sehemu nyingine kutokana na ujenzi wa eneo la maonesho ya kimataifa na wanarudi kutembelea sehemu ilikuwa ya makazi yao ya zamani. Alisema,

    "Waliwahi kuishi na kufanya kazi katika sehemu hiyo kwa miaka mingi, hivyo wana hisia nyingi kuhusu sehemu hiyo. Hivi sasa tunaandaa maonesho ya kimataifa hapa, ili watu waweze kuona sayansi na teknolojia za hali ya juu na vitu vinavyohifadhi mazingira vya nchini na vya nchi za nje, kwa hiyo watu wote wanafurahi sana."

    Bw. Li Dongbin alifahamisha kuwa Jumba la Shanghai linawakaribisha wakazi waliohamishiwa sehemu nyingine warudi kutembelea ili kupata furaha tofauti. Bw. Li alisema,

    "Watu wanaweza kuona kuwa maisha yetu ya siku za mbele yatakuwa mazuri na urahisi, na yatakuwa mazuri zaidi siku hadi siku."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako