• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hali ya maisha ya wakazi wa sehemu ya Magenge Matatu

    (GMT+08:00) 2010-09-06 16:03:26

    Mashua za kale zenye matanga zikitia nanga majini, nyumba za kupendeza zinazoonekana kwenye mazingira ya misitu, ndege wanaoruka angani, makundi ya bata na bata wa bukini wanaotembea majini, wanawake wakifua nguo kwenye mfereji, wavuvi wanatupa nyavu kuvua samaki, mandhari hiyo nzuri haikubuniwa kwenye mchoro, bali hiyo ni hali halisi ya maisha kwa wakazi wanaoishi kwenye sehemu ya Magenge Matatu iliyoko kati ya ukingo mkubwa wa Magenge Matatu na ukingo wa majini wa Gezhou, mkoani Hubei, sehemu hii ni nzuri zaidi kwenye sehemu ya Magenge Matatu ya mto Changjiang. Sauti kubwa na yenye nguvu ya wimbo wa kazini unaoimbwa na wafanyakazi wanaovuta mashua kubwa kwa kamba inawatia watu kusimama na kusikiliza. Wafanyakazi wanaovuta mashua kwa kamba wanapenda kuimba wimbo huu wanapovuta mashua ili kutumia nguvu kwa wakati mmoja na kupunguza uchovu. Wakazi wa Magenge Matatu wanaishi kwenye sehemu kati ya ukingo mkubwa wa majini wa Magenge Matatu na Gezhou, sehemu hiyo iko kwenye sehemu ya katikati ya eneo la mashariki la mtiririko wa mto Changjiang. Vitu vilivyoonekana kwenye sehemu hiyo ni utamaduni halisi wa wenyeji wa huko.

    Longjinxi ni eneo la makazi ya watu wanaoishi kwenye Magenge Matatu. Baada ya kuingia sehemu ya Longjinxi, milima iliyoko mbali ni kama mgongo wa dragon anayeingia katika mfereji, maji ya mfereji huo ni maangavu sana, watu wanaposhangazwa na maji hayo safi pia wanaburudishwa na sauti ya filimbi. Aliyepiga filimbi ni kijana mmoja aliyesimama kwenye mashua, msichana mmoja aliyevaa nguo na mapambo ya kabila la Watuja aliyeko kwenye mashua alikuwa akiwapungia mkono watalii. Watalii walipoona milima yenye miti mingi, maji maangavu ya mfereji na kusikia sauti nzuri ya filimbi, walisikia raha sana.

    Mbele kwenye njia iliyotandikwa mawe, watu waliona wavuvi wakivua samaki, wasichana waliokuwa wanafua nguo kando ya mfereji, vyombo vya kuchukulia maji kwenye mfereji na nyumba zilizoko mbali kwenye mlima. Hii ni mandhari ya utamaduni inayooneshwa na wakazi wa Magenge Matatu kwa watalii. Mwongoza watalii Liao Mengxing alisema,

    "Kwa sababu wakazi wa zamani wa Magenge Matatu waliishi kwa kutegemea uvuvi, sisi tunawaalika 'familia za kwenye maji'; licha ya wakazi hao, kuna wakazi wengine wanaoishi kwenye kando za mfereji au mto na wakazi wanaoishi milimani.

    Aidha kuna watu wa 'familia za siku hizi', ambao wamekuwa na mapato mazuri kutokana na kutegemea shughuli za utalii za 'familia za Magenge Matatu'. Popote wanapopita na kila mandhari wanayoona watalii, zote ni moja ya sehemu za utamaduni wa Magenge Matatu, zikionesha hali ya maisha ya wakazi wanaoishi kwenye eneo la Magenge Matatu, watalii wanaweza kujionea hali hiyo. Watu wanasema, mkazi yeyote wa huko anayeweza kuongea anajua kuimba, na anayeweza kutembea anajua kucheza ngoma, kwenye bonde kubwa la mlimani, na karibu nyimbo zote za kienyeji za huko zinavutia watu.

    Pengine wakati huu watalii wanakaa kimya na kusikiliza, na baada ya muda kidogo watajiunga nao. Kwani "utalii wa uzoefu" ni mtindo unaoendelezwa sana na familia za Magenge Matatu, wakati watalii wanapoburudishwa wanavutiwa na kujiunga nao na kuimba pamoja nao, hii ni njia nzuri zaidi ya kujionea utamaduni wao.

    Wakati wasichana wa kabila la Watuja walipoimba wimbo kwa sauti kubwa, bila kujifahamu utajiunga nao bila kusitasita, hakuna haya, kila mtalii anajiunga nao huku akipiga makofi na kuimba pamoja nao.. Licha ya kuimba pamoja na wasichana wa kabila la Watuja, watalii wanaweza kujionea sherehe ya harusi ya jadi ya kabila hilo, ambayo inaitwa kuolewa kwa kulia machozi. Wakati jamaa za bibi harusi wanapoimba huku wakilia, bibi harusi atachagua mtalii mwanaume kuwa 'bwana harusi', huyu 'bwana harusi' atavaa kanzu nyekundu na kuvaa ua jekundu na kumwoa huyu bibi harusi. Watalii wengi waliofika kwenye familia za Magenge Matatu, wanapenda sana kuona shamrashamra hizo.

    Bi Wang kutoka Beijing, ambaye ilikuwa mara yake ya kwanza kufika kwenye familia za Magenge Matatu, alisema ana kumbukumbu nyingi kuhusu kila mandhari na kila wimbo wa huko akisema"Ninaona hapa pana umaalumu wa kipekee, ikiwa ni pamoja na kumuoza msichana kwa kulia machozi. Wenyeji wanaimba nyimbo kwa sauti kubwa, watu wanaweza kusikia vizuri sana hata wakiwa mbali, na mazingira pia ni mazuri sana. Kumbukumbu nyingi nilizokuwa nazo ni wakati nilipoingia kwenye eneo hilo, kuna mashua moja, msichana mmoja mrembo alikuwa akiimba, huku akiwapungia mkono watalii, ninaona hali hii inavutia sana."

    Toka zamani za kale, wasomi wengi waliandika makala na mashairi kuhusu hali hii, wakiwemo Li Bai wa enzi za Tang, You Yangxiu wa enzi za Song ya kaskazini, Lu You wa enzi za Song ya kusini, Zhang Zhidong wa enzi za Qing, na Guo Moruo wa zama zetu, ambao walisimulia hali ya maisha na utamaduni wa huo kwa vipaji vyao. Mwongoza watalii Bi Liao Mengxing amewaongoza watalii mara nyingi sana kutembelea familia za Magenge Matatu, hata hivyo hajachoka kuangalia na kusikiliza, alisisitiza kuwa vitu vinavyovutia zaidi ni "vitu vya asili na halisi" akisema. "Sehemu tuliyopita, haikuathirika na kazi za kulimbikiza maji kwa mradi wa Magenge Matatu, kwa hiyo mandhari yake ni ya asili kabisa, tunaweza kuona jadi ya wenyeji wa kabila la Watuja, hii ni hali ya maisha ya asili kabisa ya wakazi wanaoishi katika eneo la Magenge Matatu."

    Kwenye eneo la familia za Magenge Matatu, kuta nyeupe za nyumba, vigae vya kuezeka mapaa, njia iliyotandikwa mawe, madaraja madogo, mifereji pamoja na nyumba zenye mtindo maalumu, zote zina uzuri wa aina yake." Tulipoondoka huko, tuliweza kusikia sauti ya nyimbo za wenyeji na filimbi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako