• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutalii kwenye mji wa Shaoxing wa sehemu ya vijijini

    (GMT+08:00) 2010-09-20 15:53:14

    Mji mdogo wa Shaoxing ulioko katika sehemu ya kusini ya China ulikuwepo toka kabla ya zaidi ya miaka 2,500 iliyopita, mji huu ulijulikana kutokana na mandhari yake nzuri ya sehemu ya vijiji na kujitokeza watu wengi mashuhuri katika historia. Makazi ya zamani ya watu hao mashuhuri yaliyoko katika mji huo pamoja na mabaki ya kiutamaduni, ni vitu ambavyo siku hizi wakazi wa Shaoxing wanajivunia na kuonea fahari, na ni sehemu ambayo watalii kutoka sehemu nyingine hawapendi kukosa kuitembelea. Watalii wengi waliofika Shaoxing hushauriwa kutembelea kwanza makazi ya zamani ya Lu Xun. Watu wanapotembea sehemu ya kati ya barabara ya Luxun iliyoko katikati ya mji, ambayo imetandikwa vipande vikubwa vya mawe ya rangi ya kijivu iliyokolea, wanaona nyumba zilizopambwa kwa mtindo wa kale zenye kuta za rangi nyeupe na mapaa yaliyoezekwa vigae vidogo vya rangi ya kijivu iliyokolea, na kuwaona wafanyabiashara wakipaza sauti kuchuuza brashi za jadi za kuandikia zenye umaalumu wa huko.

    Kuanzia barabara hiyo yenye jina na Lu Xun, njia wanazopita watalii, vitu wanavyoona, hata chakula wanachokula, vyote vina uhusiano mkubwa na Lu Xun. Bw Lu Xun alikuwa ni mwanafasihi, mwanafikra na mwanamapinduzi mashuhuri nchini China katika karne iliyopita, aliwahi kwenda kusoma nchini Japan, aliacha kazi ya udaktari, alipinga mambo maovu kwenye jamii ya kimwinyi kwa kalamu, na kuinua mwamko wa wananchi. "Hamjambo! Karibuni kwenye makazi ya zamani ya Bw Lu Xun, sasa tunawaletea maonesho ya opera ya Yue iliyotungwa kutokana na kitabu cha hadithi kilichoandikwa na Bw Lu Xun kuhusu utamaduni na maisha ya wenyeji wa Shaoxing."

    Opera nzuri ya Yue iliwapeleka watazamaji katika utamaduni na maisha ya wenyeji wa Shaoxing. Kitu cha kwanza chenye uhusiano na Bw Lu Xun kwenye barabara ya mtaani iliyotandikwa vipande vya mawe, ni baa inayoitwa "Xianheng", baa hii bado inadumisha desturi ya zamani, meza za mraba zimeenea ukumbini, wateja walijazana mle ndani na kuna makelele ya watu, watu wanakunywa pombe ya aina ya Huadiao huku wakila kidogo "huixiangdou", ambayo ni aina moja ya maharage mapana yaliyopikwa pamoja na kiungo cha star anise, nyama ya bata iliyopikwa kwa pombe, vitu hivi vinawafanya watu kujiona kama wako katika mazingira yaliyoelezwa katika kitabu cha hadithi cha Bw Lu Xun. Naibu meneja wa baa ya Xianheng Bw Mao Tianrao alisema, kuna msemo wa huko unaosema, watu wasipofika Xianheng ni sawa na watu ambao hawajafika Shaoxing, alisema"baa hii ni dirisha la Shaoxing, watalii wa nchini na wa nchi za nje wakifika Shaoxing, hawakosi kutembelea baa yetu, wanataka kuangalia utamaduni na jadi yetu, kuonja pombe ya Shaoxing, kula "Huixiangdou" pamoja na vitoweo maarufu vya kwetu. Hivi sasa baa yetu ina ushawishi mkubwa na umaalumu wa kiutamaduni katika sehemu yetu Shaoxing."

    Mbele zaidi kwa kufuata njia moja kuna nyumba ya ukoo wa Bw Lu Xun, Jina la ukoo la Lu Xun ni Zhou, ukoo wao ni ukoo wenye heshima, mapaa ya nyumba yao yana umbo la kofia la ofisa wa zamani, mwongoza watalii Bi Cao Shengyan alisema, hili ni dirisha la kufahamu hali ya maisha ya koo kubwa za jadi za Shaoxing: Alisema"Sasa tumefika kwenye nyumba ya ukoo wa Bw Lu Xun, familia kadhaa zinaishi pamoja, lakini Bw Lu Xun hakuwahi kukaa katika nyumba hii. Hivi sasa nyumba kama hiyo zilizoko Shaoxing ni zaidi ya 30."

    Baada ya kupita sebuleni kunan uwa ulio wazi, watu walioko huko wanaweza kuona anga, pande mbili zake ni ujia mrefu. Nyumba za matajiri zinakuwa na sehemu tatu hadi tano hivi za ua, profesa wa chuo cha utamaduni na jadi cha Shaoxing, ambaye ni mtaalamu anayefanya utafiti kuhusu utamaduni wa kimkoa Bi Gao Li hua alisema, nyumba hizo zinawakilisha tabia za wenyeji wa Shaoxing za kuvumilia na kutojidai, alisema: "Nyumba za matajiri yanaonesha nguvu zao, nyumba hizo zinajengwa kwenye mistari kadhaa iliyo sambamba kutoka upande wa kusini hadi upande wa kaskazini, mistari ya nyumba inapangana kutoka upande wa kusini hadi upande wa kaskazini, na nyumba zilizoko upande wa nyuma zinainuka zaidi kuliko zile zilizo upande wa mbele, kila nyumba mbele yake kuna ngazi za mawe, watu hawawezi kuona nyumba zilizoko nyuma yake."

    Makazi ya zamani ya ukoo wa Zhou yanavutia watalii wengi zaidi. Mwongoza watalii Bi Cao Shengyan alisema,

    "Mahali mlipo hivi sasa ni mahali penye baridi zaidi katika majira ya joto, hapa ni ua wazi ulioko kati ya nyumba, zamani hapa kulikuwa na miti miwili ya aina ya gold laurel, mti huu ulipandwa upya mwaka 1961. Lu Xun alipokuwa mtoto, katika usiku wa majira ya joto, alikuwa anapenda kuweka meza chini ya mti huu na kulala juu ya meza, huku akimsikiliza bibi akimsimulia hadithi zikiwemo "paka alikuwa mwalimu wa chui mkubwa" na "mlima wa Jin mashariki". Hali ya kuvutia kama hii ilielezwa katika kitabu kilichoandikwa na Bw Lu Xun.

    Hadithi za bustani yenye majani ya aina mia, ambazo wachina wengi wanazifahamu, vilevile zinahusiana na mahali hapa. Bw Lu Xun aliandika: "nyuma ya nyumba yetu kulikuwa na bustani moja kubwa iliyoitwa bustani yenye majani ya aina mia, ingawa yaliota magugu, lakini ilikuwa bustani yangu yenye furaha." Wigo wa mawe laini wa kisima, miti mikubwa ya gleditsia, nyigu wanono walioko kwenye maua ya rapa, chiriku wepesi walioruka angani ghafla kutoka kwenye majani, hali hii imebadilika, lakini sauti za milio ya wadudu aina ya cicada walioko kwenye miti bado inasikika. Watalii walipiga picha mbele ya jiwe kubwa lenye maneno ya "bustani ya majani ya aina mia", wengine wanapangusa mimea iliyopandwa kwenye matuta ya mboga, na kufikiri jinsi hali ilivyokuwa wakati Lu Xun alipocheza huko katika miaka ile.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako